Jukwaa La Wajamaa Tanzania

  • Home
  • Jukwaa La Wajamaa Tanzania

Jukwaa La Wajamaa Tanzania Lengo la jukwaa hili ni kuendeleza nadharia na mapambano ya kudai Ujamaa na Umajumui wa Afrika. Tuna

10/04/2026
Mshik**ano na watu wa Kyuba sambamba na mapinduzi matukufu ya Kyuba ni Jambo tukufu kwa wote wenye kuamini katika utu, h...
09/04/2026

Mshik**ano na watu wa Kyuba sambamba na mapinduzi matukufu ya Kyuba ni Jambo tukufu kwa wote wenye kuamini katika utu, haki na ustawi wa binadamu.
Kwa niaba ya mavuguvugu ya wavujajasho wa nchi ya Tanzania, sambamba ya yale ya Umajumui wa Afrika kote barani Afrika, salamu za mshik**ano zimewasilishwa kwa watu wa Kyuba kupitia ubalozi wao mjini Dar es Salaam, na kupokelewa na Muwakilishi-Kiongozi(Balozi) wa serikali ya Kyuba nchini Tanzania ndugu. Yordenis Despaigne Vera.
Wawakilishi wa mavuguvugu ya wavujajasho walimpasha habari ndg.balozi ya kwamba, wavujajasho wa Tanzania wanafuatilia kwa ukaribu hali ya Kyuba, hususan matishio yanayotolewa na taifa jeuri la Marekani ya kujaribu kuivamia kijeshi Kyuba, sambamba na hila za taifa hilohilo la Marekani linalozidisha vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Kyuba. Hii inajumuisha kuzuia uagizaji wa bidhaa muhimu k**a mafuta, dawa n.k, lengo likiwa ni kusababisha ugumu wa maisha nchini Kyuba, ili kuzua lawama za wanachi kwa serikali yao na mapinduzi ya Kyuba.
Hali hiyo imekuwepo kwa takribani miaka 64, ila imeongezeka zaidi katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump.
Wawakilishi wa mavuguvugu wamemfahamisha ndg.balozi ya kwamba, sisi watanzania na waafrika tunaheshimu na kutambua mchango wa kihistoria wa nchi ya Kyuba, na watu wake waliomwaga damu zao kwaajili ya kulikomboa bara hili kutoka katika makucha ya wakoloni.
Wakyuba daima wamekuwa mstari wa mbele wa mshik**ano na watu wa Tanzania na Afrika katika mashirikiano katika sekta nyeti k**a sekta ya afya na elimu. Hivyo sisi watanzania na waafrika tunawajibika kutoa mshik**ano katika kuyahami mapinduzi matukufu ya Kyuba, na watu wa Kyuba dhidi ya mahasimu na maadui wa Kyuba, ambao kwakweli ni maadui wa utu wenyewe.
Kwa upande wake ndg.balozi amebainisha kuwa, daima imekuwa ni faraja na heshima kushuhudia 'upenzi' na 'mshik**ano' wa watu wa Tanzania, na Afrika kwa Kyuba, kwa kuwa watu walio wengi kiidadi ndani ya Kyuba wana asili na nasaba ya Afrika, na ni matokeo ya biashara haramu, na ya kishenzi ya utumwa iliyoendeshwa na madola ya Ulaya-Magharibi kwa karne nyingi.
Akasisitiza ndg.balozi kuwa, isivyo bahati wanaokusudia kuingamiza Kyuba pia si marafiki wa Afrika na Tanzania. Daima wamekuwa wakijaribu kukifanya wakifanyacho Kyuba ndani ya Tanzania na Afrika kwa mitindo, na namna tofauti.
Hali hii inalazimisha uwepo wa mshik**ano baina ya watu wa Kyuba na Afrika ili kumkabili adui yao/zao huo.
Ndg.Balozi, amesiitiza kuwa watu wa Kyuba hawana chaguo jingine kwa sasa isipokuwa kujihami dhidi ya hila za Marekani, na watafanya hivyo bila kuona haya. Pia akatoa rai na tumaini lake kuwa watanzania na waafrika hawatoiacha Kyuba ikaonewa, watasimama na kushik**ana na ndugu zao wa damu wa Kyuba hadi ushindi wa kudumu utakapopatikana.
Hasta la Victoria Siempre
Yadumu mapinduzi matukufu ya Kyuba.
Udumu mshik**ano wa watu wa Afrika na Kyuba.
Asanteni

TAAZIA, TAAZIA.Kwa uzito na uchungu tunaiandika taazia ya mwanampambano, Kamaradi Abdallah Lubala.Buriani Kamaradi, Buri...
05/04/2026

TAAZIA, TAAZIA.
Kwa uzito na uchungu tunaiandika taazia ya mwanampambano, Kamaradi Abdallah Lubala.
Buriani Kamaradi, Buriani Kamaradi!.
Jukwaa la Wajamaa Tanzania-JULAWATA, litauenzi mchango wako muhimu katika mapambano ya ukombozi wa wafanyakazi, husani wa sekta ya uchukuzi, na kipekee zaidi Madereva wa Mabasi yaendayo mikoani.
Kwa muda mrefu wa uhai wako ulikubali majukumu ya ziada kuwatetea wafanyakazi wenzako ambao kwa miaka mingi wanapitia 'mbinyo' wa maslahi duni kutoka kwa waajiri, na kubetuliwa na serikali ambayo ilipaswa kuwatetea.
Kwa ushiriki wako katika mapambano hayo ya vyama vya wafanyakazi ulilipishwa gharama nyingi zikiwemo zilizokudhuru wewe binafsi;lakini katu hukususa, wala kukata tamaa kuwaleta pamoja madereva wa mabasi ili kwa pamoja wajitetetee dhidi ya visababishi vya madhila yao.
Jukwaa litaukumbuka mchango wako na kujitolea kwako kushiriki katika mapambano ya wavujajasho wengine, nje ya wale wa kisekta yaani madereva. Uliguswa na ulitambua vema ya kuwa 'uanuai' wa tabaka la wavujajasho si utofauti wao, isipokuwa ni shinikizo na shuruti la umoja wao, kwa kuwa wavujajasho wote wana kisababishi kikuu cha madhila kinachofanana miongoni mwao wote, nacho ni mfumo kandamizi na wa kinyonyaji wa ubepari.
Hivyo, umeishi ukiamini juu ya nguvu ya mshik**ano wa wavujajasho katika kuusaka ukombozi wako.
Kwa mnasaba huo, sisi Jukwaa la Wajamaa Tanzania-JULAWATA daima tumejifunza kwako na kukongwa kwa ugeri juu ya majitoleo yako yasiyokoma hata katika nyakati ngumu.
Ila kwa kuwa kilichozaliwa hufa, basi kutimu kwa safari yako ya maisha kunaendelea kutuwajibisha kujifunza zaidi na kujitolea zaidi, hasa katika nyakati za mashaka na ngumu kwa madhalili na wavujajasho k**a tulizo nazo sasa.
Usitirike ulipo!
Udumu mchango wako wa kimapambano!
Asante kwa muda wako nasi Abdullah mwana wa Lubala.
Mapambano ya Ukombozi wa Wavujajasho yanaendelea.
✊✊✊✊

Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, vilivyoanzishwa na Marekani na Iran, ni "UBEBERU" katika sura take ya "VURUGU...
28/02/2026

Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, vilivyoanzishwa na Marekani na Iran, ni "UBEBERU" katika sura take ya "VURUGU".
Itakumbukwa kuwa kwa miaka zaidi ya 47 Marekani imekuwa ikitekeleza sera za kibeberu dhidi ya Iran,zaidi katika sura ya kiuchumi(vikwazo), minyukano ya kifikra(propaganda) na diplomasia
Hatua ya sasa ni hatua ya juu ya ubeberu ambayo ni vurugu na mabavu.
Lengo la Marekani daima limekuwa ni kuhakikisha Iran haiongozwi na serikali inayoweza kusema hapana dhidi ya Marekani.
Serikali inayopokea maagizo na maamutu kutoka Washington.
Serikali inayoficha kichwa mchangani, mithili ya mbuni, pale Marekani inapofanya jeuri kwa watu wa ukanda ule na kutekeleza sera za uchumi zinqzotoa ahueni kwa makampuni ya kimarekani hata k**a nchi husika zenye rasilimali hazinufaiki.
Marekani inataka viongozi wategemezi na waraibu kwa bidhaa za Marekani(silaha,magari na teknolojia) k**a alivyokuwa Mfalme Reza Pahlavi kabla ya mapinduzi ya Iran ama walivyo wafalme wa Saudia na chi nyingine za ghuba ya bara Arabu.
Zaidi Marekani inataka kuwepo na serikali hewala-hewala na inayopiga magoti kwa Uzayuni.
Serikali ya kimapinduzi ya Iran kwa miaka takribani 50 imeyakataa hayo, na zaidi haikuona haya kuwasaidia wapigania uhuru wa Palestina, ama wale wanaowasaidia wapigania uhuru wa Palestina , ambao wengi Marekani ilichagua kuwapa jina baya la "Magaidi" ili kuhalalisha kuwaangamiza, k**a ambavyo ANC ya Afrika Kusini na kiongozi wake Nelson Mandela walivyoitwa magaidi na Marekani na Israel.
Serikali ya kimapinduzi ya Iran ikaenda mbali na kutetea haki yake kea mujibu wa sheria ya kuwa na teknolojia za nyuklia kwa matumizi ya kibinadamu k**a nishati na tiba. Imeyafanya hayo chini ya uangalizi wa shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za atomic IAEA. Ndo kusema , programu ya nyuklia ya Iran ni halali kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Sifa hizo tajwa zinairuzuku Iran sifa ya kuwa mshirika muhimu wa mapambano dhidi ya ubeberu unaoongozwa na Marekanii.
Na kwa kuwa nchi nyingi ulimwenguni, hasa za Ulimwengu wa Kusini ni wahanga wa moja kwa moja wa ubeberu wa wamagharibi, sitaraji kuona ati nchi hizo(hususan hapa Afrika) zinaona haya kuiunga mkono Iran katika uvamizi uliofanywa dhidi yake. Na zaidi watu tuliopo katika Ulimwengu wa Kusini, hasa hapa Afrika, tunapaswa kutoona haya kabisa kuinga mkono Iran katika hili.

Chimejeje Chugunyamaga Nyakanga
Abahlali baseMjondolo
Booker Ngesa Omole
Thinks Walaya Lbn
Tshisimani - Centre for Activist Education
Bio Diversity Ke
Muhemsi Yimambaga Ya ISsakanga
Faria S Kibwana
Gabii Barraza
Salim Abdul
Irene Asuwa
Asifu Amani
Ado Shaibu
Mutatembwa Atugonza Elliud
Eugene Mulenga
Walter Bgoya
Bubelwa Kaiza
Makucha Ya Chui
Daiane Silva
Didas Gobese
Frank Docta
Ezekia Mgeni
Gaidi WA Kirusi
Gerald Kamau
Mshenga Hussein
Mînt Hăîmoude
Ijembe Zodanga Wambasa
KidoJapa TheArtivist
Joel Ntile
James Kitime
Sadiki Kibugo
Kenneth Matlawe
Bonani Loliwe
Melki Kabalu Lulandala
Teehl Loé Konate
Plate Mdaijasho Sahani
Alieu Bah
Njuki Githethwa

We strongly and unequivocally condemn the arrest and continued detention of Comrade Booker Ngesa Omole, leader of the Co...
25/02/2026

We strongly and unequivocally condemn the arrest and continued detention of Comrade Booker Ngesa Omole, leader of the Communist Party Marxist Kenya (CPMK), by the Kenyan security forces. This arrest is not just an act of injustice, it is also a political message sent to all the subalterns of the Kenyan society encroached by an exploitative system that embodies all sorts of social maladies.The system that the designed to silence a revolutionary voice that speaks boldly against exploitation, imperial domination, and the suffering of the Kenyan working class.

The targeting of Comrade Omole is a direct attack on democratic expression and the fundamental rights of political organization. Reports that he has been subjected to torture, mistreatment, denied engagement with his legal team, as well as accessing proper medical care are deeply alarming and unacceptable. We demand his immediate and unconditional release. We further demand that he be granted urgent access to proper medical treatment and that all forms of harassment, intimidation, and persecution against him and members of CPMK(targeted) cease at once.

History teaches us that repression is the last refuge of a fearful ruling elite. Threats, intimidation, arbitrary detention, and torture cannot silence the spinning wheel of revolutionary change. The struggle for dignity, land, bread, and sovereignty cannot be crushed by batons, prison walls, or fabricated charges. When the state negates justice and serves imperial interests, it exposes itself as a puppet of forces that fear the organized power of the people.

We affirm that the future belongs not to imperial might, nor to its local enforcers, but to the workers, peasants, and youth who dare to dream of a liberated society. The will of the people is stronger than the machinery of repression. No prison can detain an idea whose time has come.
The demand is clear: Free Booker Ngesa Omole now.
Booker Ngesa Omole

Kamaradi Humphrey Polepole arejeshwe akiwa hai sasa!
07/10/2025

Kamaradi Humphrey Polepole arejeshwe akiwa hai sasa!

CONGRATULATION TO ABAHLALI baseMJONDOLO ON YOUR 20TH ANNIVERSARY!For over two decades, you have stood unwavering on the ...
04/10/2025

CONGRATULATION TO ABAHLALI baseMJONDOLO ON YOUR 20TH ANNIVERSARY!

For over two decades, you have stood unwavering on the frontlines of the struggle for land, housing, dignity, and justice in South Africa, a nation scarred by a legacy of systemic injustice and entrenched inequality, now threatened once again by the resurgence of the very apartheid forces that sought to suppress it.
Your extraordinary dedication to amplifying the voices of shack dwellers and marginalized communities both within South Africa and globally has ignited inspiration far beyond your immediate frontiers. You embody the essence of grassroots, people-centered democracy and the unyielding pursuit of human dignity.
Through steadfast resistance, unbreakable resilience, and relentless grassroots organizing, you have revealed to the world the true power of the underprivileged people. You have transformed informal settlements into vibrant hubs of political education, solidarity, food sovereignty through agroecology, and hope, challenging structures of exclusion while forging a future rooted in equality and justice.
These victories have not come without profound sacrifice. You have faced vilification, brutal assaults, and the heartbreaking loss of comrades, heroes who laid down their lives in defense of this revolutionary movement.
Yet, despite these trials, you have resisted the forces of repression and stagnation. With courage and resolve, you have advanced the cause of liberation. We honor all those who have made the ultimate sacrifice, your fallen comrades are immortalized as true heroes of the struggle. As you mark this monumental milestone, know that their legacy endures and their sacrifice was never in vain.
We, the Tanzania Socialist Forum (TASOFO), stand profoundly inspired by the indomitable spirit and visionary work of Abahlali baseMjondolo. We recognize you as the steadfast shield that guards the realm of the underprivileged of the world in that part of our mother continent.
We stand in unshakable solidarity with you, celebrating your relentless pursuit of justice and emancipation.
Long live Abahlali baseMjondolo!
Long live the spirit of Internationalism!
Hongereni Sana.
Tanzania Socialist Forum (TASOFO)
4 October, 2025.
Abahlali baseMjondolo

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jukwaa La Wajamaa Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization?

Share