Community Emancipation Organization-Coeo

  • Home
  • Community Emancipation Organization-Coeo
Call

Community Emancipation Organization-Coeo Community Emancipation Organization-COEO is a Non-Government organization registered 25NGO/0009028.

11/10/2025

Wito kwa mahak**a za mwanzo Tanzania

Huu ni mnyororo wa rufaa kwa aina mbalimbali za migogoro. Karibu tupitie kwa pamoja
24/08/2025

Huu ni mnyororo wa rufaa kwa aina mbalimbali za migogoro. Karibu tupitie kwa pamoja

26/10/2024

Tunawatakia Kila la kheri wagombea wetu wa VYAMA vyote waliopitishwa na VYAMA vyao uchukuaji mwema wa fomu na kuzijaza kikamilifu kabisaa.

Kuna mambo ya kuzingatia ambayo yatakupa sifa ya kupitishwa na TAMISEMI wasije wakakuengua. Mambo hayo ni ;-

1. Uraia utajaza - MTANZANIA.
2. Jina la chama,hapa utaandika kwa kirefu; kmf: CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA). CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) nk, Usijaze kwa kifupi wakakuengua kwa makosa k**a hayo.
3. Halmashauri; Hapa utajaza kikamilifu halmashauri unayotokea, halmashauri iliyosajiliwa na zipo za aina 3 kutokana na eneo ulipo halmashauri uliyopo mfano ;-

i. HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA,DAR ES SALAAM,MWANZA,TANGA,MBEYA,DODOMA nk jaza hivyo k**a unatokea kwenye halmashauri za majiji hayo.

ii. HALMASHAURI YA MANISPAA YA KAHAMA, SINGIDA, MOROGORO,IRINGA,MTWARA,MOSHI, SHINYANGA nk utajaza kikamilifu halmashauri unayotokea kwenye hizi MANISPAA.

iii. HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU, SENGEREMA,HAI,KIBONDO,KASULU,UVINZA,KWIMBA,MISUNGWI,MASWA,BAHI,KYERWA,KYELA,MISENYI,BUKOMBE,UKEREWE,BUNDA, SINGIDA VIJIJJNI,KALIUA,URAMBO,NZEGA,IGUNGA,nk utajaza kikamilifu hivyo k**a unatokea kwenye halmashauri za wilaya miongoni mwa wilaya za TANZANIA.

Kingine ni ;

1. Kusoma kiswahili weka alama ya vema kwenye kiboksi Cha NDIYO,Usiweke kwenye HAPANA UTAKOSA SIFA YA KUGOMBEA MAANA UTAKUWA HUJUI KUSOMA
2. Kuandika kiswahili weka alama ya VEMA ✅ kwenye kiboksi Cha NDIYO

Tuwashauri Wananchi huko sisi k**a PARALEGAL ikiwa watahitaji Msaada wetu bila kujali Itikadi

05/01/2023

Ni ndefu ila itakusaidia. IPITIE KWA.UTULIVU

Mambo kumi yakuzingatia wakati unajitetea mahak**ani

1:K**a unahojiwa na Wakili Mahak**ani usijibu bila kutafakari alichokuuliza

2: Wakili asikuogopeshe kwa ukali, anapokuuliza kwani ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha ulichopanga kusema

3: Usilazimishe kujibu kitu ambacho hukijui ni bora kusema sijui kuliko kulazimisha kujibu

4: Usipaniki kiasi cha kutoa neno lolote la kashfa, kejeli, au tusi mahak**ani unaweza kuongeza kosa la kuidharau Mahak**a

5: K**a hukuelewa vizuri kosa ulilosomewa ni bora kukaa kimya, kwakuwa ukikaa kimya unaandikiwa umekataa kosa

6: Kanuni ya sheria ni kuwa, ni kazi ya aliyekush*taki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa na si kazi yako kuthibitisha kuwa haujatenda kosa

7: K**a ulitenda kosa katika harakati za kujitetea usidhuriwe iambie mahak**a kuwa ulitenda kosa ukijilinda (self defence) inaruhusiwa, hata k**a uliua waweza kuachiwa

8: K**a ndugu yako hana akili timamu na ametenda kosa iambie mahak**a. Hii ni kwasababu kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya wasio na akili

9: Inakubalika na ukaachiwa huru kusema kuwa sikuwa eneo la tukio wakati likitokea k**a kweli haukuwapo

10: K**a wanaokushtaki wanashahidi na unamjua kuwa kuna kipindi aliwahi kuchangnyikiwa au kufanya tukio lolote la uhalifu kabla, ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake.

18/12/2022

Sheria ilikwishapitishwa kuwa mawakili kwa sasa watashughulika kuanzia mahak**a za mwanzo.

Kikosi kazi cha wasaidizi wa kisheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara za kutoa elimu katik...
12/12/2022

Kikosi kazi cha wasaidizi wa kisheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara za kutoa elimu katika siku 16 za kupinga ukatili na ukatili wa kijinsia Wilayani Maswa.

Tunaendelea kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria, karibuni sana.
12/12/2022

Tunaendelea kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria, karibuni sana.

Tunawakaribisha wadau wote wa sheria na haki za binadamu katika ukurasa wetu. Tutajifunza sheria mbalimbali kupitia ukur...
02/09/2022

Tunawakaribisha wadau wote wa sheria na haki za binadamu katika ukurasa wetu. Tutajifunza sheria mbalimbali kupitia ukurasa huu

Address

170

09

Opening Hours

Monday 08:30 - 16:30
Tuesday 08:30 - 16:30
Wednesday 08:30 - 16:30
Thursday 08:30 - 16:30
Friday 08:30 - 16:30

Telephone

+255752216090

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Community Emancipation Organization-Coeo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Want your organization to be the top-listed non profit organization?

Share