08/09/2026
📍UVIRA
Kwa lengo la kusherehekea Mwezi wa Vijana, Cercle des Jeunes Musulmans pour le Développement - CJMD Uvira imepanga na kufanikisha mechi ya urafiki na mshik**ano dhidi ya vijana wa Centre Kalimabenge
Mechi hiyo ilifanyika Jumapili tarehe 09/08/2026 saa kumi mchana (16h00) kwenye Uwanja uliopo karibu na Mto Kavimvira, maarufu uwanja wa mafuriko Kavimvira, chini ya kauli :
"ENSEMBLE POUR L'UNITÉ, LE RESPECT ET LA PAIX !"
MGENI RASMI ASIFU HATUA HIYO
Mgeni rasmi wa siku hiyo alikuwa Muheshimiwa Issa MWAKA MUSTAPHA, Kiongozi wa Vijana Mjini Uvira (CUJ-Uvira). Alifungua rasmi mechi hiyo, akisindikizwa na Mwenye Kiti Makamu wa Baraza la Vijana Waislamu Uvira (CJI), Bwana Ir. Songolo Kabenga Suleimani.
Katika hotuba yake, Muheshimiwa Issa Mwaka alionyesha furaha kubwa na kusema:
Mechi hiyo ilimalizika kwa matokeo ya bao 2-1 kwa faida ya CJMD Uvira.
Baada ya mechi, Bwana Ramazani Kwibe Saleh, Mwenye Kiti wa CJMD Uvira alionyesha matumaini yake kuwa:
Kwa upande wake, Bwana Amisi Muhammad Ali, akizungumzia upande wa vijana wa Centre ya Kalimabenge, alifurahishwa na kitendo hicho na kusema:
Hii inaweza kuwa suluhu muhimu na moja wapo ya kumaliza sinto fahamu ndani ya vijana wa jamii ya Kiislamu.
Tukio hili linaonyesha wazi kuwa kupitia michezo, vijana wanaweza kujenga umoja mshik**ano na amani badala ya migogoro. CJMD Uvira imeahidi kuendelea na mipango k**a hii.
IQRA GLOBAL Media
+243 962 825 902