19/07/2026
Taasisi ya Yunus Emre ya Zanzibar ilishiriki katika Maonesho ya Utambulisho na Maonyesho ya Chuo Kikuu cha Zanzibar, ambapo banda letu la utambulisho lilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa wageni. Katika banda letu, ziliwasilishwa kazi za sanaa zilizotengenezwa na washiriki wa kozi zetu katika warsha za utamaduni na sanaa, pamoja na maudhui yanayoakisi utamaduni wa Kituruki, vifaa vya kufundishia lugha ya Kituruki na mawasilisho mbalimbali ya picha.
Wageni walihudumiwa kahawa ya Kituruki pamoja na vyakula na vinywaji mbalimbali; pia walipewa fursa ya kuifahamu kwa karibu zaidi tamaduni ya Kituruki kupitia michezo na shughuli mbalimbali za kitamaduni.
Miongoni mwa viongozi waliotembelea banda letu walikuwa Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu wa Zanzibar, Mheshimiwa Mudrick Ramadhan Soraga; Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Zeyana Abdallah Hamid; na Mkuu wa Wakala wa Uwezeshaji Kiuchumi Zanzibar (ZEEA), Mheshimiwa Juma Burhan Mohamed. Viongozi hao walieleza kufurahishwa kwao na kuvutiwa kwao na lugha ya Kituruki pamoja na utamaduni wa Kituruki. Tunawashukuru wageni wote waliotutembelea na kuonyesha hamu yao kwa utamaduni wetu.
***
Zanzibar Yunus Emre Enstitüsü olarak katıldığımız Zanzibar Üniversitesi Tanıtım ve Sergi Günleri’nde tanıtım standımız yoğun ilgi gördü. Standımızda, kursiyerlerimiz tarafından kültür sanat atölyelerimizde yapılan eserlerin yanı sıra Türk kültürünü yansıtan içeriklere, Türkçe öğretim materyallerimize ve görsel sunumlara yer verildi.
Misafirlerimize Türk kahvesi ile birlikte çeşitli ikramlarda bulunuldu; kültürümüze özgü oyunlar ve etkinliklerle kültürümüzü yakından tanıma fırsatı sunuldu.
Standımızı ziyaret eden Zanzibar İletişim, Bilgi Teknolojileri ve İnovasyon Bakanı Sayın Mudrick Ramadhan Soraga, Tanzanya Birleşik Cumhuriyeti Parlamentosu Üyesi Dr. Zeyana Abdallah Hamid ve Zanzibar Ekonomik Güçlendirme Ajansı Başkanı Sayın Juma Burhan Mohamed, Türkçeye ve Türk kültürüne olan ilgilerini dile getirdiler. Standımıza ilgi gösteren tüm misafirlerimize teşekkür ederiz.
Yunus Emre Enstitüsü