Tulia Trust

Tulia Trust Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tulia Trust, Nonprofit Organization, Uyole, Uyole.

22/08/2026

BODABODA UYOLE WAAHIDI USALAMA NA AMANI SIKU YA TULIA TRADITIONAL FESTIVAL 2026

Makamu Mwenyekiti wa madereva Bodaboda Mbeya-Uyole Joseph Mbwete ameshukuru na kufurahia ujio wa ngoma za asili katika Jimbo la Uyole huku akisema kuwa ngoma izo zinafunza mambo mengi sana.

Pia ameahidi kuwa bodaboda Uyole watahakikisha wanasafirisha watu kwa amani na utulivu siku zote tatu za tamasha.

Tamasha hili kitafanyika
🗓️ 24-26 Septemba 2026

📍 Viwanja vya Shule ya msingi Gombe-Jimbo la Uyole

⏰ Kuanzia Saa 02:00 asubuhi

Nukta tumeibeba hakuna mwisho
…
🙏

YearJourney

Miaka10YaTuliaTrust

22/08/2026

TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL DANCE NI ZAIDI YA BURUDANI.

Afisa habari Tulia Trust Joshua Edward ameelezea tamasha la Tulia Trust Traditional Dance Festival 2026 kuwa ni zaidi ya burudani kwani kuna maonyesho ya sanaa, historia, mila, destuli, lugha, mavazi, sanaa na maisha ya jamii kiujumla.

Huku tamasha hili likitoa fursa kubwa kwa vijana na watu mbalimbali kuonyesha vipaji vyao katika jukwaa hili la Tulia Traditional Dance Festival.

Tamasha hili litafanyika
🗓️ 24-26 septemba 2026

📍 Viwanja vya Shule ya msingi Gombe-Jimbo la Uyole.

⏰ Kuanzia saa2:00 asubuhi

Nukta tumeibeba hakuna mwisho
…
🙏


YearJourney
TuliaTrustMiaka10
Miaka10YaTuliaTrust

21/08/2026

MADEREVA BAJAJI UYOLE NA FURSA YA TAMASHA LA NGOMA ZA JADI 2026.

Mwenyekiti wa madereva Bajaji Jimbo la Uyole ndugu. Joseph Jackson amemshukuru mkurugenzi wa Tulia Trust ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge Jimbo la Uyole Mh. Dkt. Tulia Ackson kwa kuleta tamasha la ngoma asili litakalo leta fursa mbalimbali za kiuchumi haswa kwa upande wa usafirishaji wa watu mbalimbali kwa kutumia bajaji.

Amesema wapo tayari kwa ujio wa tamasha la ngoma za jadi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Dkt. Tulia katika tamasha hili na kuhakikisha wananchi watakao hudhuria wanapata usafiri wa uhakika.

NUKTA TUMEIBEBA | HAKUNA MWISHO

Historia yenye alama…

🙏


YearJourney

Miaka10YaTuliaTrust

21/08/2026

CHIFU MWASHINGA AFURAHISHWA UWEPO WA TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2026 UYOLE.

Chifu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Chifu Rocket Mwashinga ametoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Tulia Trust ambae ni Mbunge wa Jimbo la Uyole na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mh. Dkt. Tulia Ackson kwa kuanzisha tamasha hili la ngoma za asili.

Amesema kuwa tamasha hili ni muhimu sana kwani linadumisha mila na desturi zetu haswa kwa vijana.

Lakini pia Chief Mwashinga ametumia nafasi hii kuwa alika machifu wengine kuja kushiriki tamasha hili la Tulia Traditional Dance Festival 2026.

21/08/2026

TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2026 KUFANYIKA SEPTEMBA 24–26 | TULIA TRUST KUADHIMISHA MIAKA 10

MBEYA:
Tulia Trust inatarajia kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016 kwa kuandaa Tulia Traditional Dance Festival 2026, tamasha kubwa la ngoma za asili litakalofanyika kwa msimu wa 10.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 24 hadi 26, 2026, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Gombe, Jimbo la Uyole, Jijini Mbeya, likiwa na kauli mbiu:

“TUUENZI UTAMADUNI WETU”

Kwa muda wa siku tatu, tamasha hilo linatarajiwa kuwakutanisha vikundi vya ngoma za jadi, wasanii, wananchi na wadau mbalimbali wa utamaduni kutoka maeneo tofauti, katika kusherehekea na kuendeleza utajiri wa urithi wa Tanzania.

Maadhimisho haya yanafanyika ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya muongo mmoja wa Tulia Trust, huku tamasha likilenga kutoa nafasi kwa jamii kuutambua, kuuenzi na kuurithisha utamaduni wa Tanzania kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kupitia Tulia Traditional Dance Festival 2026, wananchi watapata fursa ya kushuhudia burudani za ngoma za asili, kujifunza kuhusu tamaduni mbalimbali na kushiriki katika juhudi za kuhakikisha urithi wa kitamaduni unaendelea kuwa sehemu muhimu ya utambulisho wa Taifa.

GREENCITY TV ONLINE itaendelea kuwafikishia taarifa zaidi kuhusu maandalizi, vikundi vitakavyoshiriki na matukio mbalimbali kuelekea tamasha hilo kubwa la utamaduni jijini Mbeya.

📌 TAREHE

24–26 SEPTEMBA 2026

📍 UKUMBI

Uwanja wa Shule ya Msingi Gombe, Jimbo la Uyole – Mbeya

🎭 TAMASHA

Tulia Traditional Dance Festival 2026

🗣️ KAULI MBIU

“TUUENZI UTAMADUNI WETU”

GREENCITY TV ONLINE
Habari • Utamaduni • Vijana • Jamii • Maendeleo






Mbeya
Uyole
TuliaTrust10Years
Miaka10YaTuliaTrust
UtamaduniWaTanzania
TanzaniaCulture
GreenCityTVOnline

21/08/2026

TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2026 KUFANYIKA SEPTEMBA 24-26 |TULIA TRUST IKIADHIMISHA MIAKA KUMI TANGU KUANZISHWA KWAKE.

Tulia Trust tunatarajia kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwetu kwa kuandaa Tulia Traditional Dance Festival 2026 kwa msımu wa kumi (10),

Tamasha kubwa la Ngoma za Asili litafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 Septemba 2026 kuanzia saa 02:00 asubuhi kwa msimu wa kumi tangu kuanzishwa kwake.

Tamasha hili lita fanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Gombe Jimbo la Uyole Jijini Mbeya, likiwa na kauli mbiu isemayo “Tuuenzi Utamaduni Wetu”.

Tamasha hili ni sehemu ya maadhimisho ya muongo mmoja wa Tulia Trust tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, likılenga kuwakutanısha wananchı, vikundı vya ngoma za jadi, wasanii na wadau mbalimbali katika kusherehekea utajiri wa utamaduni wa Tanzania.

RASMI TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2026 KUFANYIKA GOMBE-UYOLE.Tulia Trust Traditional Dance 2026 rasmi imetangazwa l...
21/08/2026

RASMI TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2026 KUFANYIKA GOMBE-UYOLE.

Tulia Trust Traditional Dance 2026 rasmi imetangazwa leo tarehe 21 Agosti 2026

Tamasha hili litafanyika Septemba 24 hadi 26, 2026 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Gombe, Uyole-Mbeya.

Pamoja na hayo Tulia Trust inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kweke mnamo mwaka 2026.

NUKTA TUMEIBEBA | HAKUNA MWISHO

Historia yenye alama…

🙏


YearJourney

Miaka10YaTuliaTrust

Leo saa5:00 asubuhi Agosti 21.2026 tuna jambo letu , tutakupa taarifa zote kwenye mitandao yetu ya kijamii📍Gr City hotel...
21/08/2026

Leo saa5:00 asubuhi Agosti 21.2026 tuna jambo letu , tutakupa taarifa zote kwenye mitandao yetu ya kijamii

📍Gr City hotel-sower
NUKTA TUMEIBEBA | HAKUNA MWISHO

Historia yenye alama…

🙏


YearJourney

Miaka10YaTuliaTrust

WAMEAMUA KUIBEBA NUKTA | WANAHITAJI MCHEZO UENDELEENukta tumeibeba na tutaendelea kuibeba, tulikuwa nayo enzi na enzi na...
20/08/2026

WAMEAMUA KUIBEBA NUKTA | WANAHITAJI MCHEZO UENDELEE

Nukta tumeibeba na tutaendelea kuibeba, tulikuwa nayo enzi na enzi na tunaendelea kuwa nayo kwa vizazi na vizazi

NUKTA TUMEIBEBA | HAKUNA MWISHO

Tarehe 24 mpaka 26 mwaka huu 2026 Jambo ni moja tu.

Historia yenye alama…

🙏


YearJourney

Miaka10YaTuliaTrust

20/08/2026

SWALI LA MWL. NYERERE.

Hilo ni swali la hayati Mwalimu Julius Kambalage Nyerere, unajua kwanini aliuliza hilo swali?

NUKTA TUMEIBEBA | HAKUNA MWISHO

Tarehe 24 mpaka 26 mwaka huu 2026 Jambo ni moja tu.

Historia yenye alama…

🙏


YearJourney

Miaka10YaTuliaTrust

Address

Uyole
Uyole

Opening Hours

Monday 07:30 - 17:00
Tuesday 07:30 - 17:00
Wednesday 07:30 - 17:00
Thursday 07:30 - 17:00
Friday 07:30 - 17:00
Saturday 07:30 - 13:00

Telephone

+255767860515

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tulia Trust posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share