Jumuiya Ya Hifadhi Ya Wanyamapori Uyumbu

Jumuiya Ya Hifadhi Ya Wanyamapori Uyumbu Uhifadhi Kwaajili ya Maendeleo ya Jamii

“Huwezi kuwa mwana wa nchi k**a huna uchungu na nchi yako.”
07/04/2026

“Huwezi kuwa mwana wa nchi k**a huna uchungu na nchi yako.”

Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori Uyumbu inawatakia Wakristo Wote  Furaha, upendo na amani katika kusheherekea sikukuu ya ...
05/04/2026

Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori Uyumbu inawatakia Wakristo Wote Furaha, upendo na amani katika kusheherekea sikukuu ya pasaka.

Heri ya Sikukuu ya Pasaka!  Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Uyumbu, tunawatakia Pasaka njema iliyojaa upendo, amani na...
05/04/2026

Heri ya Sikukuu ya Pasaka!

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Uyumbu, tunawatakia Pasaka njema iliyojaa upendo, amani na matumaini mapya.

🌳

Viongozi wa WMA, pamoja na Afisa wanyamapori wa Wilaya walipata mafunzo,   tarehe 6 Machi 2026 katika Ofisi ya Hakimu wa...
25/03/2026

Viongozi wa WMA, pamoja na Afisa wanyamapori wa Wilaya walipata mafunzo, tarehe 6 Machi 2026 katika Ofisi ya Hakimu wa Wilaya na Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (OC-CID) kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa kesi zinazohusiana na rasilimali za wanyamapori katika hifadhi ya , hususan masuala ya udhibiti wa uvunaji holela wa rasililimali za maliasili.

Kupitia vikao hivyo, uelewa kuhusu taratibu za kisheria, uchunguzi na uendeshaji wa kesi za rasilimali za maliasili ulielekezwa kwa kina kutoka kwa wataalam hao. Pia, changamoto katika ukusanyaji wa ushahidi na uratibu wa taasisi zilijadiliwa kwa kina.

Hatua muhimu iliyofikiwa ni kuwekwa kwa mkakati wa pamoja wa kuboresha usimamizi wa kesi hizi, kwa kuimarisha ushirikiano, mawasiliano, na ufanisi wa vyombo husika.

.tanzania

Mnamo tarehe 6 Machi, viongozi  wa  walipata fursa ya kutembelea ofisi ya Maliasili ya Wilaya ya Urambo District. Katika...
25/03/2026

Mnamo tarehe 6 Machi, viongozi wa walipata fursa ya kutembelea ofisi ya Maliasili ya Wilaya ya Urambo District. Katika ziara hiyo, walifanya kikao na Afisa Maliasili wa Wilaya pamoja na Afisa Wanyamapori wa Wilaya.

Katika kikao hicho, walijadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa jumuiya, ikiwemo
-kutoa mirejesho katika shughuli za usimamizi wa rasilimali za wanyamapori,
-Ulinzi na shughuli za doria
-Mikakati ya kuboresha utendaji wa shughuli za doria na jumuiya kwa ujumla.

Kikao hicho kilikuwa ni muhimu ambacho kililenga kuimarisha ushirikiano kati ya jumuiya na mamlaka za wilaya katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za maliasili kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Uongozi wa Hifadhi ya Jamii Ya Wanyamapori Uyumbu, inawatakia Waislamu wote Nchini kher, furaha na fanaka katika kushehe...
21/03/2026

Uongozi wa Hifadhi ya Jamii Ya Wanyamapori Uyumbu, inawatakia Waislamu wote Nchini kher, furaha na fanaka katika kusheherekea siku ya Eid.

🌙🕌❤️

Viongozi wa Uyumbu WMA watembelea Ofisi Ya Mkuu wa Kanda Ya Magharibi (Tawa)Tarehe 05/03/2026, viongozi wa Uyumbu WMA wa...
06/03/2026

Viongozi wa Uyumbu WMA watembelea Ofisi Ya Mkuu wa Kanda Ya Magharibi (Tawa)

Tarehe 05/03/2026, viongozi wa Uyumbu WMA walitembelea ofisi ya Mkuu wa Kanda ya Magharibi (Tawa) kwa lengo la kufanya mazungumzo na Viongozi wa kanda kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Jumuiya.

Katika kikao hicho, masuala mbalimbali yalijadiliwa yakiwemo,

i.Utambulisho wa viongozi wapya wa WMA kwa uongozi wa Kanda.

ii.Uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za WMA pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usimamizi na ulinzi wa rasilimali za hifadhi.

iii.Kujadili namna ya kuimarisha kikosi cha Askari wa WMA (VGS), kupitia mafunzo pamoja na kuboresha mikakati ya kudhibiti ujangili na uvamizi ndani ya maeneo ya hifadhi.

iv.Njia mbadala kwa WMA kuwekeza katika kufanya biashara, kupitia rasilimali zake.

Ambapo Mkuu wa Kanda, Afande. Winbright Munuo alisisitiza kwa kushauri umuhimu wa WMA kuendelea kubuni nakutengeneza miongozo ya vyanzo mbadala vya mapato vinavyotokana na rasilimali zilizopo ndani ya WMA. Na alitaja shughuli k**a ufugaji wa nyuki na uvuvi endelevu kuwa miongoni mwa fursa zinazoweza kusaidia kuongeza mapato ya jumuiya na kuimarisha juhudi za uhifadhi na maendeleo kwa jamii.

Aidha, Kamanda Munuo, alisisitiza kuwa ofisi ya Kanda itaendelea kutoa ushirikiano na msaada wakutosha wa kitaalamu kwenye WMA kwaajili ya kuakikisha inafanya ulinzi wa rasilimali wenye tija ambao utaleta maendeleo kwenye jumuiya na jamii kwa ujumla.



Ziara ya Kikazi ya Viongozi wa Uyumbu WMA – Ofisi ya Maliasili Mkoa wa TaboraKatika Kuimarisha ushirikiano na kuhakikish...
06/03/2026

Ziara ya Kikazi ya Viongozi wa Uyumbu WMA – Ofisi ya Maliasili Mkoa wa Tabora

Katika Kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha ushirikishwaji wa wadau muhimu katika usimamizi na maendeleo ya shughuli za uhifadhi ndani ya Uyumbu WMA, Tarehe 05/03/2026, Viongozi wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori Uyumbu WMA (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu) walitembelea Ofisi ya Maliasili ya Mkoa wa Tabora na kufanya mazungumzo na Afisa Wanyamapori wa Mkoa (RGO), wa Mkoa wa Tabora pamoja na Afisa Nyuki wa Mkoa wa Tabora.

Mambo muhimu yaliyojadiliwa ni,

-Utambulisho rasmi wa viongozi wapya wa Jumuiya.
-Kutoa taarifa juu ya Utekelezaji wa shughuli mbalimbali jumuiya, ikiwemo ulinzi na usimamizi wa eneo la WMA.
-Maendeleo ya uwekezaji na fursa za kiuchumi ndani ya Jumuiya.
-Fursa za kuendeleza ufugaji nyuki na Biashara ya Asali kwa WMA.

Katika mazungumzo hayo, Regional Game Officer (RGO) wa Mkoa wa Tabora alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha usimamizi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori, akibainisha kuwa Uyumbu WMA ni tunu muhimu kwaajili ya maendeleo ya vijiji wanachama, na Mkoa wa Tabora.

Aidha, aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano na msaada wa kitaalamu kwa Jumuiya ili kuhakikisha rasilimali hizo zinahifadhiwa kwa uendelevu kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.


Uwasilishaji wa Mapato na Matumizi ya WMA– KIJIJI CHA NSONGOLOKupitia utekelezaji wa Mradi wa SEGA, tarehe 28/02/2026, K...
02/03/2026

Uwasilishaji wa Mapato na Matumizi ya WMA– KIJIJI CHA NSONGOLO

Kupitia utekelezaji wa Mradi wa SEGA, tarehe 28/02/2026, Katibu wa WMA pamoja na viongozi wawakilishi wa Kijiji cha Nsogolo waliwasilisha rasmi taarifa ya mapato na matumizi ya Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori Uyumbu (Uyumbu WMA) kwa wananchi. Taarifa hiyo ilihusu mwaka wa fedha 2024/2025 na mwaka wa fedha 2025/2026 hadi robo ya tatu.

Uwasilishaji huu ulilenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora, kwa kutoa wananchi taarifa sahihi kuhusu mapato na matumizi ya Jumuiya kwa wananchi ambao ni wadau muhimu wa jumuiya.

katika kikao hicho kilichohudhuriwa na diwani wa kata ya Uyumbu Mhe. Mkandala Gabriel Mkandala, alipongeza uongozi wa WMA kwakuakikisha kuwa wananchi ambao ndio wadau wakwanza kabisa kupata taarifa za muenendo wa mapato na matumizi ya jumuiya, na kusisitiza kuwa viongozi waakikishe wanasimamia zile rasilimali kwaajili ya maslai mapana ya jamii ili inufaike na maendeleo kutoka kwenye hazina ya uhifadhi waliotoa.

Vilevile Wananchi walishukuru kwa kushirikishwa na kueleza kuwa awali hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu haki yao ya kupokea taarifa hizi.

Zoezi hili limeimarisha uelewa wa wananchi, ushirikishwaji wa jamii, na kuunda imani thabiti kati ya WMA, uongozi wa kijiji na wananchi.


UtawalaBora Ushirikishwaji MaendeleoVijiji

KIKAO CHA WADAU WA WMAMnamo tarehe 26 Februari 2026, WMA iliandaa kikao na wadau wake muhimu, wakiwemo Wenyeviti na Wate...
02/03/2026

KIKAO CHA WADAU WA WMA

Mnamo tarehe 26 Februari 2026, WMA iliandaa kikao na wadau wake muhimu, wakiwemo Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji wanachama, Maafisa Watendaji wa Kata za Ugalla na Uyumbu, Afisa Tarafa wa Ussoke, Afisa Wanyamapori wa Wilaya na Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Urambo.

Kikao kililenga kutathmini changamoto za WMA na kubaini mikakati ya kuimarisha ushirikiano na wadau, kuhakikisha uwajibikaji, uwazi, na uendelevu wa uhifadhi. Ndugu Nelson Majura, Afisa Tarafa wa Ussoke, aliwasisitiza viongozi wa WMA kushirikiana kwa karibu na serikali za vijiji ili kuhakikisha maendeleo ya jamii na manufaa yanayohusiana na rasilimali za WMA yanawanufaisha vijiji wanachama.

Aidha, viongozi wa serikali za vijiji walisisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano baina ya WMA na vijiji ili kuimarisha misingi ya utawala bora na uwajibikaji.


Uwajibikaji Uwazi

Jana, tarehe 16 Februari 2026, WMA ilipokea simu mbili za kisasa kutoka Wasima Organization kwa ajili ya kuimarisha ukus...
17/02/2026

Jana, tarehe 16 Februari 2026, WMA ilipokea simu mbili za kisasa kutoka Wasima Organization kwa ajili ya kuimarisha ukusanyaji wa taarifa za doria katika Pori la Uyumbu.

Simu hizo zitatumika katika mfumo wa SMART (Spatial Monitoring and Reporting Tool), hatua inayokwenda kuongeza usahihi wa taarifa za doria, uwajibikaji na ufanisi katika ulinzi wa rasilimali za WMA.

Aidha, askari (VGS) walipata mafunzo ya vitendo juu ya matumizi ya mfumo huo, ambayo yamesaidia katika kuimarisha uwezo wao wa kitaalamu katika ukusanyaji wa taarifa za doria. Kadhalika WMA inatoa shukrani za dhati kwa WASIMA kwajitiahada zao za dhati za kuboresha shughuli za utendajikazi wa doria.



Address

Urambo
P.O.BOX150URAMBO-TABORA

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jumuiya Ya Hifadhi Ya Wanyamapori Uyumbu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share