Rehema Orphans Foundation

Rehema Orphans Foundation Rehema Orphans Foundation | Tanga, Tanzania Caring for 300+ Orphans and Vulnerable Children with love, education, shelter & hope.

Join us in transforming lives and building brighter futures. ๐Ÿ“ž 0695 320 454

25/05/2026

During the 2025 Childrenโ€™s Food Festival, children from Rehema Orphans Foundation had the opportunity to showcase their talents in front of the guest of honor, invited guests, and fellow children. It was a joyful moment filled with confidence, happiness, and incredible talent from our children. โค๏ธ

This year, we warmly invite you, your family, and your friends to join us once again for our 2026 Childrenโ€™s Food Festival taking place on Wednesday, May 27, 2026, at Tate Plus Hall near the Muheza Main Bus Stand from 11:00 AM to 4:00 PM. ๐Ÿ™๐Ÿพ

Come celebrate with our children and continue bringing smiles, hope, and love into their lives. โค๏ธ

HopeForChildren

25/05/2026

Katika hafla ya chakula cha watoto ya mwaka 2025, watoto wa Rehema Orphans Foundation walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao mbele ya mgeni rasmi, wageni waalikwa pamoja na watoto wenzao. Ilikuwa ni wakati wa furaha, kujiamini na kuonesha uwezo mkubwa uliopo ndani ya watoto wetu. โค๏ธ

Mwaka huu tunakukaribisha wewe, familia yako na marafiki zako kuungana nasi tena katika hafla yetu ya mwaka 2026 itakayofanyika Jumatano, tarehe 27 Mei 2026 katika ukumbi wa Tate Plus ulio karibu na stendi kuu ya mabasi ya Muheza kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. ๐Ÿ™๐Ÿพ

Karibu tusherehekee pamoja na watoto wetu na kuendelea kuwaletea tabasamu na matumaini. โค๏ธ

HopeForChildren

25/05/2026

Katika hafla ya chakula cha watoto iliyofanyika mwaka jana tarehe 7 Juni 2025, tulipata heshima kubwa ya kuwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Majengo, Mheshimiwa Mukadam Sabuni, ambaye pia alimuwakilisha Mheshimiwa Mbunge wetu wa Muheza, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma (MwanaFA) โ€” ambaye mwaka huu ndiye mgeni wetu rasmi katika sherehe hizi muhimu.

Katika hafla ya mwaka huu, tunatarajia pia kuwa na mgeni maalum, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mheshimiwa Ayubu Yassini Sebabili. ๐Ÿ™๐Ÿพ

Tunaendelea kuwashukuru kwa dhati viongozi wetu wote wa Serikali katika Wilaya ya Muheza kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa taasisi yetu ya Rehema Orphans Foundation pamoja na watoto wetu kwa ujumla.

Mwenyezi Mungu awabariki sana na kuwafanikisha katika majukumu yenu yote ya kuwatumikia wananchi. โค๏ธ

EidCelebration ServingHumanity

23/05/2026

Tukiendelea na maandalizi ya hafla ya chakula kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, tunaendelea kuwakaribisha wadau mbalimbali kuungana nasi kufanikisha sherehe hii muhimu itakayogusa maisha ya zaidi ya watoto 300. โค๏ธ๐Ÿฝ๏ธ

Karibu tushirikiane kuleta tabasamu na matumaini kwa watoto wetu.

๐Ÿ“ž Wasiliana nasi leo kwa maelezo zaidi: 0695 320 454

23/05/2026

Afisa Tarafa wa Muheza, ndugu Ali H. Kijazi, akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya katika hafla ya chakula na watoto iliyoandaliwa na Rehema Orphans Foundation tarehe 7 Juni 2025, alisisitiza umuhimu wa jamii nzima kushiriki katika malezi ya watoto kwa kutoa msaada utakaowezesha watoto kuendelea kupata malezi bora na kuwaepusha kujiingiza katika mambo yasiyofaa.

Kwa pamoja tunaweza kujenga jamii yenye upendo, matumaini na mustakabali bora kwa watoto wetu. ๐Ÿคโค๏ธ

21/05/2026

๐ŸŒ™โค๏ธ EID AL ADHA NA WATOTO WETU โค๏ธ๐ŸŒ™

Katika siku hii muhimu ya upendo, mshikamano na kujali jamii, Rehema Orphans Foundation inayo furaha kubwa kuungana pamoja na viongozi wetu wenye moyo wa huruma na upendo kwa watoto pamoja na jamii ya Muheza. ๐ŸŽŠ

๐ŸŽ–๏ธ MGENI RASMI
Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA)
Mbunge wa Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

๐ŸŽ–๏ธ MGENI MAALUM
Mhe. Ayubu Yassini Sebabili
Mkuu wa Wilaya ya Muheza.

Viongozi hawa wameendelea kuwa sehemu muhimu ya watu wanaoiunga mkono Rehema Orphans Foundation katika kuwapa watoto wetu matumaini, furaha na maisha bora. โค๏ธ

Karibuni tushirikiane kueneza upendo kwa watoto wetu. ๐Ÿค

Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi kwa namba: 0695 320 454

Children Hope Love Community MwanaFA

21/05/2026

Katika sherehe ya sikukuu ya mwaka jana tarehe 7 Juni 2025, tulibarikiwa kuwa na kwaya ya watoto kutoka Kanisa la Anglican chini ya uongozi wa Father Paul Luhinga โ€” mshauri na mlezi wetu wa karibu. ๐ŸŽถโค๏ธ

Ilikuwa ni wakati wa furaha, upendo na umoja uliogusa mioyo ya wengi. Mwaka huu, kupitia sapoti yako, tunatarajia kuona mambo makubwa na mazuri zaidi.๐Ÿ™

Karibu uwe sehemu ya maadhimisho yetu ya mwaka huu kwa kushiriki nasi kuwapa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu tabasamu la kweli. ๐ŸŒ

Sherehe ya hafla ya chakula ya watoto itafanyika siku ya Jumatano, tarehe 27 Mei 2026 katika ukumbi wa Tate Plus ulio karibu na stendi kuu ya mabasi ya Muheza, Tanga.

Wote mnakaribishwa .

๐Ÿ“ž Mawasiliano: 0695 320 454

Community Love TogetherWeCan

21/05/2026

Katika sherehe ya sikukuu ya mwaka jana tarehe 7 Juni 2025, tulibarikiwa kuwa na waimba kaswida kutoka Msikiti wa Shauri Moyo chini ya uongozi wa Sheikh Mkuu Ramadhani Akida โ€” baba yetu na mshauri wetu wa karibu. ๐ŸŒ™โœจ

Mwaka huu tunajiandaa kwa tukio kubwa zaidi, lenye furaha, upendo na mshikamano kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu. โค๏ธ

Karibu uwe sehemu ya historia hii nzuri kwa kushiriki nasi katika maadhimisho ya mwaka huu, In Shaa Allah. ๐Ÿ™

Charity Community TogetherWeCan

07/05/2026

๐Ÿ”ฅ๐Ÿš’ Huu ni mwezi wa Usalama wa Moto na Maandalizi ya Dharura ๐Ÿš’๐Ÿ”ฅ

Katika Rehema Orphans Foundation tunaendelea kuwajengea watoto elimu ya:
โœ… Kujikinga na moto
โœ… Usalama wa nyumbani na shuleni
โœ… Hatua za kuchukua wakati wa dharura

Tunajenga jamii salama kupitia watoto salama. โค๏ธ

โ€œMtoto Salama, Jamii Salamaโ€

28/04/2026

Kwa furaha kubwa tunawajulisha kuwa ujenzi wa ๐‘๐ž๐ก๐ž๐ฆ๐š ๐Š๐ข๐๐ฌ ๐ƒ๐ข๐ ๐ข๐ญ๐š๐ฅ ๐‡๐ฎ๐› ( ๐Š๐ข๐ญ๐ฎ๐จ ๐œ๐ก๐š ๐Œ๐š๐Ÿ๐ฎ๐ง๐ณ๐จ ๐ฒ๐š ๐Š๐จ๐ฆ๐ฉ๐ฒ๐ฎ๐ญ๐š ๐ง๐š ๐”๐ฃ๐ฎ๐ณ๐ข ๐ฐ๐š ๐Š๐ข๐๐ข๐ฃ๐ข๐ญ๐š๐ฅ๐ข ๐ค๐ฐ๐š ๐ฐ๐š๐ญ๐จ๐ญ๐จ) cha shirika la Rehema Orphans Foundation katika wilaya ya ๐Œ๐ฎ๐ก๐ž๐ณ๐š ๐ฆ๐ค๐จ๐š๐ง๐ข ๐“๐š๐ง๐ ๐š unaendelea.

๐Ÿ’ก ๐Š๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐๐ฎ๐ง๐ข๐š ๐ฒ๐š ๐ฅ๐ž๐จ, ๐ฎ๐ฃ๐ฎ๐ณ๐ข ๐ฐ๐š ๐ค๐ข๐๐ข๐ฃ๐ข๐ญ๐š๐ฅ๐ข ๐ฌ๐ข๐จ ๐œ๐ก๐š๐ ๐ฎ๐จ, ๐ง๐ข ๐ก๐ข๐ญ๐š๐ฃ๐ข ๐ฅ๐š ๐ฆ๐ฌ๐ข๐ง๐ ๐ข.

Mtoto asiye na ujuzi wa teknolojia anakosa fursa nyingi za ๐ž๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ, ๐š๐ฃ๐ข๐ซ๐š ๐ง๐š ๐ฎ๐›๐ฎ๐ง๐ข๐Ÿ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐ค๐ž๐ฌ๐ก๐จ.

Kupitia kituo hiki, tunajenga daraja la kuwaunganisha watoto wetu na dunia ya kisasa:

๐Ÿ’ป ๐Š๐ฎ๐ฃ๐ข๐Ÿ๐ฎ๐ง๐ณ๐š ๐Š๐จ๐ฆ๐ฉ๐ฒ๐ฎ๐ญ๐š
๐Ÿ‘จ๐Ÿ’ป ๐‚๐จ๐๐ข๐ง๐ 
๐ŸŽจ ๐”๐›๐ฎ๐ง๐ข๐Ÿ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐Š๐ข๐๐ข๐ฃ๐ข๐ญ๐š๐ฅ๐ข
๐ŸŒ ๐Œ๐š๐ญ๐ฎ๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐’๐š๐ฅ๐š๐ฆ๐š ๐ฒ๐š ๐Œ๐ญ๐š๐ง๐๐š๐จ
๐Ÿค– ๐“๐ž๐ค๐ง๐จ๐ฅ๐จ๐ฃ๐ข๐š ๐ฒ๐š ๐Š๐ข๐ฌ๐š๐ฌ๐š (๐€๐ซ๐ญ๐ข๐Ÿ๐ข๐œ๐ข๐š๐ฅ ๐ˆ๐ง๐ญ๐ž๐ฅ๐ฅ๐ข๐ ๐ž๐ง๐œ๐ž - ๐€๐ˆ)

๐Ÿ‘‰ Kwa wengi wao, hii itakuwa mara yao ya kwanza kabisa kushika kompyuta. ๐‡๐ฎ๐ฎ ๐ง๐ข ๐ฎ๐ฐ๐ž๐ค๐ž๐ณ๐š๐ฃ๐ข ๐ฆ๐ฎ๐ก๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ค๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐๐ฎ๐ง๐ข๐š ๐ฒ๐š ๐ฌ๐š๐ฌ๐š ๐ฎ๐ญ๐š๐ค๐š๐จ๐›๐š๐๐ข๐ฅ๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ฆ๐š๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ฒ๐š๐จ ๐ฆ๐ข๐ฅ๐ž๐ฅ๐ž.

๐Ÿ™ Asante kwa kuendelea kuwa sehemu ya safari hii.

๐Ÿค Tunaendelea kuhitaji msaada wako ili tukamilishe mradi huu muhimu.

๐–๐š๐ฌ๐ข๐ฅ๐ข๐š๐ง๐š ๐ง๐š๐ฌ๐ข ๐ค๐ฐ๐š ๐ญ๐š๐š๐ซ๐ข๐Ÿ๐š ๐ณ๐š๐ข๐๐ข;
๐Ÿ“ž ๐ŸŽ๐Ÿ”๐Ÿ—๐Ÿ“ ๐Ÿ‘๐Ÿ๐ŸŽ ๐Ÿ’๐Ÿ“๐Ÿ’
๐Ÿ“ง ๐ซ๐ž๐ก๐ž๐ฆ๐š๐จ๐ซ๐ฉ๐ก๐š๐ง๐ฌ@๐ ๐ฆ๐š๐ข๐ฅ.๐œ๐จ๐ฆ

Address

Shauri Moyo, Masaki Msufini, Muheza
Tanga

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 13:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rehema Orphans Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share