05/06/2026
Unyanyasaji wa kijinsia hauwezi kumalizwa na mtu mmoja au taasisi moja pekee. Mabadiliko ya kweli yanatokea pale wazazi, walimu, viongozi wa dini, viongozi wa jamii, vijana na serikali wanapounganisha sauti na nguvu zao kwa lengo moja.
Kupitia majadiliano ya jamii, tunajenga uelewa, kuimarisha ushirikiano na kuchukua hatua za pamoja katika kuzuia na kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Tukisimama pamoja, tunaweza kujenga jamii salama, yenye usawa na heshima kwa kila mtu.