Hilmy Disability Organisation

Hilmy Disability Organisation Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Hilmy Disability Organisation, Charitable organisation, Vuga, Stone Town.

Hilmy Disability Organisation is a community-driven, non-profit initiative committed to advancing dignity, inclusion, and practical support for people living with disabilities across Zanzibar and Tanzania.

TANGAZO LA TAASISITaasisi ya Hilmy Disabled organisation inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa siku ya Jumamosi, tareh...
02/04/2026

TANGAZO LA TAASISI

Taasisi ya Hilmy Disabled organisation inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa siku ya Jumamosi, tarehe 03/04/2026, In shaa Allah, itaendelea na ziara maalum ya ugawaji wa viti vya magurudumu (wheelchairs) kwa watu wote waliojisajili, pamoja na utoaji wa vifaa vingine muhimu kwa ajili ya watu wenye ulemavu kwa kisiwa cha Unguja.

Lengo la zoezi hili ni kuimarisha ustawi, kujenga ushirikishwaji, na kuboresha maisha ya watu wenye uhitaji maalum katika jamii.

Walengwa wote wanahimizwa kuwa tayari kwa wakati uliopangwa ili kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi. Aidha, tunaomba ushirikiano kutoka kwa familia na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha zoezi linafanyika kwa utaratibu mzuri.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi ya taasisi.

Imetolewa na:
Uongozi wa Taasisi

Mabadiliko hayaanzi na wengi, yanaanza na wewe. Toa leo chochote ulichonacho – iwe sehemu ya kufanikisha wheelchair moja...
02/04/2026

Mabadiliko hayaanzi na wengi, yanaanza na wewe. Toa leo chochote ulichonacho – iwe sehemu ya kufanikisha wheelchair moja.

YAS: 0659 555 942
PBZ: 0993 572 001
UK: Monzo – 79588690 | 04-00-04
Ref: Wheelchair Campaign

Au changia kwa mujibu wa uwezo wako.

Leo ni siku ya kufanya tofauti.Usisubiri mpaka uwe na kiasi kikubwa. Anza na kile ulichonacho leo. Kidogo chako kinaweza...
01/04/2026

Leo ni siku ya kufanya tofauti.

Usisubiri mpaka uwe na kiasi kikubwa. Anza na kile ulichonacho leo. Kidogo chako kinaweza kuwa mwanzo wa kiti mwendo kitakachobadilisha maisha ya mtu.

Wakati wewe unatoa, wengine wataongeza. Kwa pamoja, leo tunaweza kufanikisha kiti kimoja au zaidi.

Changia leo:
YAS: 0659 555 942
PBZ: 0993 572 001

UK: Monzo – 79588690 | 04-00-04

Ref: Wheelchair Campaign

Au changia kwa mujibu wa uwezo wako.

Toa leo. Shirikisha wengine. Fanya iwezekane.

NI MAALUM YA MIEZI 3: TOA KITI MWENDO – BADILI MAISHA(Aprili – Julai)Assalaam Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,Hilmy D...
31/03/2026

NI MAALUM YA MIEZI 3: TOA KITI MWENDO – BADILI MAISHA
(Aprili – Julai)

Assalaam Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Hilmy Disability Organisation inazindua kampeni ya miezi 3 yenye lengo la kufanikisha upatikanaji wa viti mwendo 150 kwa watu wenye ulemavu wanaosubiri msaada.

Kupitia mchango wako, unatoa kiti mwendo ambacho si kifaa tu bali ni fursa ya uhuru, heshima na maisha bora.

Kwa nini uchangie?
• Unarejesha uhuru wa kusogea na kujitegemea
• Unamwezesha mtoto kucheza, kujifunza na kukua kwa kujiamini
• Unarahisisha upatikanaji wa huduma za afya
• Unajenga jamii jumuishi yenye huruma na haki

Gharama za Udhamini:
• Mtu mzima: £100 (Tsh 380,000)
• Mtoto: £80 (Tsh 304,000)

Lengo la Kampeni:
• Viti mwendo 150 ndani ya miezi 3
• Ugawaji kwa wahitaji waliothibitishwa kupitia database

Taarifa za Malipo:
• YAS (Mix By Yas): 0659 555 942
• PBZ Bank (Hilmy Disability Organisation): 0993 572 001

Kwa waliopo UK:
• Bank: Monzo
• A/c No: 79588690
• Sort Code: 04-00-04
• Jina: M. Ahmad

Reference: Wheelchair Campaign

Uwajibikaji:
• Uwazi wa michango yote
• Ripoti za mara kwa mara kwa wadau
• Vielelezo vya ugawaji

“Mwenye kumsaidia mwenzake, Allah humsaidia duniani na Akhera.”

Hilmy Disability Organisation
Inclusion with Integrity, Support with Purpose

Usisubiri – toa kiti mwendo leo, badili maisha ya mtu milele.

28/03/2026

Alhamdulillah, kila msaada unaowafikia wenye mahitaji ni hatua ya kurejesha matumaini. Asanteni kwa kuwa sehemu ya mabadiliko haya.

INTERIM REPORT: ZIARA YA PEMBA – UGAWAJI WA WHEELCHAIRSTarehe ya Ziara: 23 Machi 2026Imeandaliwa na: Hilmy Charity Organ...
28/03/2026

INTERIM REPORT: ZIARA YA PEMBA – UGAWAJI WA WHEELCHAIRS
Tarehe ya Ziara: 23 Machi 2026
Imeandaliwa na: Hilmy Charity Organisation

1. Utangulizi

Ripoti hii ya muda inaeleza maendeleo ya awali ya ziara ya ugawaji wa wheelchairs kwa watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba. Zoezi lililenga kuwafikia walengwa waliokuwa wamejisajili na kuthibitishwa kupitia database ya taasisi, kwa kuzingatia vigezo vya mahitaji halisi (needs-based approach).

Kwa mujibu wa nyaraka za usajili , walengwa walitoka maeneo mbalimbali ikiwemo Wete, Konde, Mkoani na vijiji vya pembezoni, wakiwa na aina tofauti za ulemavu.

2. Malengo ya Ziara
• Kugawa wheelchairs kwa walengwa waliothibitishwa
• Kufanya uhakiki wa hali halisi ya maisha ya walengwa
• Kubaini mahitaji ya ziada (mf. pampers, magodoro, magongo)
• Kuimarisha uhusiano na jamii na viongozi wa maeneo

3. Muhtasari wa Utekelezaji

Ugawaji ulianza katika eneo la Uweleni Basra na kuendelea kwa awamu katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini Pemba. Zoezi lilifanyika kwa kuzingatia upatikanaji wa walengwa na hali ya miundombinu.

Taarifa zinaonesha kuwa:
• Walengwa wengi wana ulemavu wa miguu au mwili mzima
• Baadhi walihitaji msaada wa ziada k**a pampers na magodoro
• Umri wa walengwa unatofautiana kuanzia watoto hadi wazee

Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha kuwa baadhi ya walengwa bado hawajafikiwa (“Bado”), hivyo zoezi halijakamilika kikamilifu .

4. Mafanikio ya Awali
• Idadi kubwa ya walengwa waliothibitishwa wamepatiwa wheelchairs
• Uhakiki wa mahitaji umefanyika kwa njia ya ziara za ana kwa ana
• Ushirikiano mzuri kutoka kwa jamii na viongozi wa maeneo
• Watoto waliokuwa nje ya mfumo wa elimu sasa wana nafasi ya kurejea skuli

5. Changamoto Zilizobainika

Miundombinu: Barabara mbovu na maeneo ya vijijini kuchelewesha usambazaji
Upatikanaji wa Walengwa: Baadhi hawakupatikana kwa wakati
Mahitaji Makubwa: Uhitaji wa vifaa vya ziada k**a magodoro na pampers
Usahihi wa Data: Baadhi ya taarifa zilihitaji uhakiki zaidi

6. Hali ya Mahitaji (Unmet Needs)

Kwa mujibu wa database ya taasisi, zaidi ya watu 380 wenye ulemavu wa aina mbalimbali bado hawajafikiwa. Hii inaonesha pengo kubwa kati ya mahitaji yaliyopo na uwezo wa sasa wa usambazaji.

Hali hii ina athari zifuatazo:
• Kuchelewa kwa huduma kwa walengwa walio katika mazingira hatarishi
• Kuongezeka kwa matarajio na presha kutoka kwa jamii
• Hatari ya kushuka kwa imani ya wadau iwapo hatua hazitachukuliwa kwa wakati.

7. Mapendekezo ya Kiutendaji

a) Kuongeza Timu za Usambazaji (Parallel Deployment)
Kuanzisha timu mbili au zaidi zinazofanya kazi kwa wakati mmoja ili kuongeza kasi ya kufikia walengwa wengi kwa muda mfupi.
• Faida: kuongeza ufanisi na kupunguza backlog
• Tahadhari: inahitaji uratibu madhubuti na usimamizi wa rasilimali

b) Mfumo wa Vituo vya Ugawaji (Distribution Hubs)
Kuanzisha vituo vya kimkakati ambapo walengwa watafika au kufikishwa kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa.
• Faida: kupunguza gharama na muda wa usafiri
• Tahadhari: kulinda hadhi ya walengwa na kuhakikisha upatikanaji kwa wenye ulemavu mkubwa

c) Ushirikiano na Viongozi wa Maeneo
Kushirikisha shehia na wadau wa kijamii katika kuratibu walengwa na ratiba za ugawaji ili kuongeza uwazi na ufanisi

d) Uboreshaji wa Data na Ufuatiliaji
Kuhakiki database na kuweka mfumo wa kufuatilia waliopokea na ambao bado hawajafikiwa

8. Masuala ya Utawala Bora na Uadilifu
• Ugawaji umefanyika kwa uwazi na kwa kuzingatia mahitaji halisi
• Mfumo wa uthibitishaji umetumika kupunguza upendeleo
• Ufuatiliaji wa kumbukumbu unaimarisha uwajibikaji kwa wadau na wafadhili

9. Hatua Zinazofuata
• Kukamilisha ugawaji kwa walengwa waliobaki
• Kufanya tathmini ya kina ya mahitaji ya ziada (phase 2 support)
• Kuandaa ripoti kamili yenye takwimu sahihi
• Kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji wa muda mrefu kwa walengwa

10. Hitimisho

Ziara ya Pemba imeleta mafanikio ya awali yenye kuonekana, lakini pia imebainisha ukubwa wa mahitaji uliopo. Ili kufikia walengwa wote kwa ufanisi, kuna umuhimu wa kuimarisha mkakati wa usambazaji kupitia timu nyingi na vituo vya ugawaji, huku tukidumisha misingi ya uwazi, uadilifu, na huduma yenye heshima kwa walengwa.

26/03/2026

TAARIFA MUHIMU KUHUSU MCHANGO WA BI ASHA – PEMBA

Ndugu zetu wapendwa,

Kufuatia ziara yetu ya hivi karibuni kisiwani Pemba (Kaskazini Wete, Barawa Kisiwani), tulipata fursa ya kukutana na ndugu yetu Bi Asha, ambaye ni mtu mwenye ulemavu, na tukamkabidhi kiti mwendo (wheelchair) ili kumsaidia katika maisha yake ya kila siku.

Tuliguswa sana na hali ngumu ya makazi na mazingira anayoishi. Kwa ridhaa yake mwenyewe, tuliweza kurekodi video inayoonesha hali halisi ili kuwafahamisha wadau na kuhamasisha msaada wa kumboreshea makazi yake.

Hata hivyo, kumekuwa na taarifa zinazozagaa zikidai kuwa juhudi hizi si za kweli, na kwamba taasisi yetu inajihusisha na shughuli zisizo sahihi. Tunapenda kuweka mambo yafuatayo wazi:
1. Uhalali wa Taasisi
Jumuiya yetu imesajiliwa kisheria, na taarifa zake zinapatikana kupitia mamlaka husika za usajili wa jumuiya zisizo za kiserikali Zanzibar.
2. Uwajibikaji na Uwazi
Tupo tayari kutoa taarifa za kifedha (annual accounts na returns) kwa yeyote mwenye nia ya kuthibitisha uhalali na uwajibikaji wa shughuli zetu kupitia taratibu rasmi.
3. Wito wa Uthibitisho wa Taarifa
Tunamkaribisha yeyote mwenye mashaka kufuata njia sahihi za kisheria na kiutawala kuthibitisha taarifa, badala ya kusambaza tuhuma zisizo na ushahidi ambazo zinaweza kuathiri msaada unaohitajika kwa wahitaji k**a Bi Asha.
4. Lengo Letu
Dhamira yetu ni kusaidia jamii yenye uhitaji kwa uadilifu, uwazi na kwa kuzingatia misingi ya utu na huruma.

Tunawaomba wadau wote kuendelea kuwa na moyo wa kusaidia na kuchukua tahadhari dhidi ya taarifa zisizothibitishwa. Kila mchango wenu una athari ya moja kwa moja katika kubadilisha maisha ya watu wenye uhitaji.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote kuwa miongoni mwa wanaosaidia kwa ikhlasi na kutuepusha na fitna na tuhuma zisizo na msingi.

Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.

Hilmy Disability Organisation

Alhamdulillah, kwa fadhila za Allah ziara yetu ya Pemba imekamilika kwa mafanikio makubwa.Tumeweza kugawa wheelchairs 56...
25/03/2026

Alhamdulillah, kwa fadhila za Allah ziara yetu ya Pemba imekamilika kwa mafanikio makubwa.

Tumeweza kugawa wheelchairs 56 — kati ya hizo 46 ni kwa watoto na 10 kwa watu wazima. Mahitaji ni makubwa sana, na changamoto za miundombinu zilikuwepo, lakini kwa uwezo na msaada wa Allah tumefanikisha jukumu hili.

Tunatoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia sadaka, hususan sadaka za kila Ijumaa, pamoja na wale waliosaidia kugharamia na kurahisisha usafirishaji wa vifaa hadi Pemba na safari yetu kwa ujumla.

Mchango wenu umeleta faraja, heshima, na matumaini mapya kwa wahitaji. Allah awalipe kwa wema na azidi kuweka baraka katika mali na juhudi zenu.

Tarehe 23/03/2026, Hilmy Charity Organisation — In shaa Allah, kesho tutawasili Pemba kwa ajili ya kukabidhi vifaa kwa n...
22/03/2026

Tarehe 23/03/2026, Hilmy Charity Organisation — In shaa Allah, kesho tutawasili Pemba kwa ajili ya kukabidhi vifaa kwa ndugu zetu wenye ulemavu.

Sadaka zenu za kila Alhamisi na Ijumaa zinaendelea kuleta tofauti kubwa katika maisha ya jamii yenye mahitaji.

Ahsanteni sana kwa kila aliyechangia na kuunga mkono juhudi hizi za kheri.

Usikubali kubaki nyuma; nawe uwe miongoni mwa wanaoleta mabadiliko katika jamii.

Assalamu alaykumIn shaa Allah, Hilmy Charity Organisation tunatarajia kwenda kisiwa cha Pemba mwishoni mwa mwezi Machi 2...
13/03/2026

Assalamu alaykum

In shaa Allah, Hilmy Charity Organisation tunatarajia kwenda kisiwa cha Pemba mwishoni mwa mwezi Machi 2026 kwa ajili ya kuwafikishia ndugu zetu wenye uhitaji viti mwendo (wheelchairs) vipya 45. Vifaa hivi vingi vimekusudiwa kwa watoto wenye ulemavu, ambao ndio kipaumbele chetu, ili kuwasaidia wazazi na walezi wao kuwafikisha katika maeneo muhimu k**a skulini, hospitalini na nyumba za ibada.

Pia tumepanga kutoa idadi k**a hiyo ya wheelchairs katika kisiwa cha Unguja, kwa malengo hayo hayo ya kuwasaidia watoto na watu wenye uhitaji mkubwa katika jamii.

Hilmy Charity Organisation iliasisiwa mwaka 2013 na tayari ina usajili wa kudumu Zanzibar. Tangu kuanzishwa kwake, kwa msaada wa wahisani na watu wema, tumefanikiwa kutoa zaidi ya:

• Wheelchairs 5000
• Crutches 200
• Magodoro 188
• Zaidi ya boksi 3000 za pampers

Tunawaomba ndugu na marafiki wenye uwezo waunge mkono juhudi hizi za kheri ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wenye uhitaji. Mchango unaweza kutumwa kupitia nambari iliyo kwenye kipeperushi chetu.

Kusaidia mtu mwenye ulemavu ni kurejesha matumaini na heshima ya maisha yake. Karibuni tushirikiane katika kufanya kheri hii.

Hilmy Disability Organisation itaendelea kusimamia rasilimali kwa uadilifu, kuimarisha ujumuishi na kutoa msaada wenye m...
13/03/2026

Hilmy Disability Organisation itaendelea kusimamia rasilimali kwa uadilifu, kuimarisha ujumuishi na kutoa msaada wenye malengo mahsusi kwa jamii.

09/03/2026

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Ndugu zangu Waislamu,

Tunapokaribia kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunakumbushwa wajibu muhimu wa Zakatul Fitr – sadaka ambayo Mtume ﷺ alituamrisha kuitoa ili kuwatakasa waliokufunga na kuwasaidia wale wenye uhitaji siku ya Eid. Lengo lake ni kuhakikisha kuwa hata watu walio katika hali ngumu hawabaki nyuma katika furaha na baraka za siku hii tukufu.

Kupitia HILMY DISABILITY ORGANISATION, tunawaomba muunge mkono juhudi zetu za kuwafikia ndugu zetu wenye ulemavu ambao ni miongoni mwa wanaostahiki kupokea Zakah. Taasisi yetu kwa sasa inahudumia zaidi ya familia 50 za watu wenye ulemavu katika Unguja na Pemba, wengi wao wakiwa katika mazingira magumu ya maisha. Kwa msaada wenu wa Zakatul Fitr, tunaweza kuhakikisha kuwa nao wanapata chakula na mahitaji muhimu ili washerehekee Eid kwa heshima, furaha na matumaini mapya.

Kutoa kwako leo kunaweza kubadilisha furaha ya familia nzima siku ya Eid. Tunawaomba wale waliojaaliwa wachangie kupitia:

Namba ya kuchangia:
0659 555 942
Jina: HILMY DISABILITY ORGANISATION

Allah akubalie funga zenu, dua zenu na sadaka zenu, na azidishe baraka katika mali zenu. Mwenyezi Mungu awajaalie wote wanaotoa na wanaopokea wawe miongoni mwa wenye kupata radhi zake.

Jazakumullahu khayran.

Address

Vuga
Stone Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hilmy Disability Organisation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share