24/08/2026
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ashiriki Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Utengenezaji wa Mifuko Rafiki kwa Mazingira
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukene, Ndugu Abubakary Ally, ameshiriki katika hafla ya kufunga mafunzo ya utengenezaji wa mifuko rafiki kwa yaliyotolewa na Christian Education and Development Organization (CEDO) kwa ufadhili wa Colleges and Institutes Canada ( ) kupitia mradi wa (Uwezeshaji Kupitia Ujuzi).
Mafunzo hayo yamehusisha jumla ya washiriki 10, ambao wamepatiwa mafunzo kwa muda wa siku 8 na kupata ujuzi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo utengenezaji wa mifuko rafiki kwa mazingira, uandaaji wa mpango wa biashara, utunzaji na uhifadhi wa mazingira, pamoja na usawa wa kijinsia.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ndugu Abubakary Ally aliwapongeza washiriki kwa kukamilisha mafunzo na kuwasisitiza kutumia ipasavyo maarifa na ujuzi walioupata ili kujenga fursa za kiuchumi kwao binafsi, familia zao na jamii kwa ujumla.
Aidha, aliwahimiza washiriki kuunda vikundi vya uzalishaji na ujasiriamali ili kuwa na fursa nzuri ya kupata mikopo na programu mbalimbali za uwezeshaji zinazotolewa na Halmashauri, pamoja na taasisi nyingine za kifedha na maendeleo.
Alisisitiza kuwa ujuzi walioupata ni mtaji muhimu wa kujiajiri na kuongeza kipato, huku uzalishaji wa mifuko rafiki kwa ukiwa na mchango katika kulinda mazingira, kupunguza matumizi ya mifuko isiyooza na kukuza uchumi wa kijani.
Kwa upande wake, imeeleza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana na wanawake kupata ujuzi wa vitendo, kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kiuchumi zinazolinda mazingira na kukuza maendeleo endelevu.
CEDO inaendelea kuhimiza matumizi ya ujuzi, ubunifu na ujasiriamali k**a nyenzo muhimu katika kuwawezesha wananchi kujenga maisha yenye kipato endelevu.