Cocoda Tanzania

Cocoda Tanzania Community Concern of Orphans and Development Association (COCODA) formally registered as a non-governmental organization in Njombe, Tanzania in 2000.

COCODA is providing education to local communities so as to increase awareness about HIV/AIDS.

05/08/2026

Insp. Alexander Makwasa Polisi Kata wa Mjimwema akieleza jinsi mafunzo ya Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu yatakavyosaidia kupunguza kesi na migogoro katika jamii.

Mafunzo haya yamefanyika Kata ya Mjimwema kupitia mradi wa ESP CICan Tanzania unaotekelezwa na Cocoda Tanzania na Colleges and Institutes Canada / Collèges et instituts Canada kwa ufadhili wa Global Affairs Canada Global Affairs Canada.

Mafunzo ya siku tatu ya Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu kwa katika Kata ya Mjimwema Halmashauri ya Mji Njombe, yam...
31/07/2026

Mafunzo ya siku tatu ya Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu kwa katika Kata ya Mjimwema Halmashauri ya Mji Njombe, yamefikia tamati yakilenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki, wajibu, na ushiriki sawa wa wanawake na wanaume katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mafunzo yalilenga katika mada za usawa wa kijinsia, tofauti kati ya jinsi (s*x) na jinsia (gender), pamoja na mgawanyo wa majukumu ndani ya familia na jamii. Mafunzo hayo yamelenga kubadili mitazamo potofu na kuhamasisha ushirikiano unaozingatia usawa ili kuchochea maendeleo jumuishi katika Kata hiyo ya Mjimwema.

Mafunzo haya yamefanyika kupitia Mradi wa Uwezeshaji kupitia Ujuzi (ESP) unaotekelezwa na Colleges and Institutes Canada (CICan) kwa kushirikiana na shirika la COCODA, chini ya ufadhili wa Global Affairs Canada.

.

The management of COCODA Tanzania would like to express its sincere gratitude to the leadership of the ESP Tanzania Proj...
26/07/2026

The management of COCODA Tanzania would like to express its sincere gratitude to the leadership of the ESP Tanzania Project CICan Tanzania implemented through the partnership of Colleges and Institutes Canada (CICan), the Government of Tanzania through the Ministry of Education, Science and Technology Moest Moest Folk Development Colleges (FDCs), and Community-Based Organizations (CBOs), with financial support from the Government of Canada.

We sincerely appreciate the opportunity to participate in the practical study tour facilitated by Fanshawe College Fanshawe College Centennial College, and CICan Tanzania.

This hands-on learning experience has significantly enhanced the knowledge, skills, and capacity of our participants through direct exposure to best practices and practical experience.

We also highly value the strong collaboration and the generous support of modern equipment provided to our organization. These resources will strengthen the implementation of our project activities and enhance our institutional capacity to achieve sustainable development outcomes.

The knowledge, experience, and resources gained through this partnership will enable COCODA Tanzania to further strengthen its training and empowerment programs for girls and women facing social and economic vulnerabilities, equipping them with the skills and opportunities they need to become self-reliant and achieve their aspirations.

We are deeply grateful for your continued partnership, trust, and commitment to creating lasting positive change in our communities.

.

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika COCODA Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kupitia I...
23/06/2026

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika COCODA Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii na TECDEN Tanzania ECD Network imefika Kijiji cha Nyombo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kuendesha vituo vya kulelea watoto mchana k**a nyenzo muhimu ya kuimarisha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.

Kupitia uhamasishaji huu wananchi walipata elimu kuhusu malezi chanya, lishe bora, ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria. Elimu hii inalenga kujenga jamii inayoweka mtoto mbele na kuhakikisha kila mtoto anapata mwanzo bora wa maisha.

Vituo vya kulelea watoto mchana vina mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya mtoto, huku vikitoa fursa kwa wazazi na walezi kushiriki shughuli za uzalishaji mali kwa utulivu wakijua watoto wao wako katika mazingira salama na yenye kujali ustawi wao.

Cocoda Tanzania inaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Serikali, washirika wa maendeleo na jamii kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya kukua, kujifunza na kufikia uwezo wao kamili.

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika COCODA Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kupitia I...
18/06/2026

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika COCODA Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii na TECDEN tunaendelea kufanya uhamasishaji wa uanzishwaji wa Vituo vya kulelea watoto mchana wenye lengo la kuchochea Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM)

Uhamasishaji huo umefanyika katika Kijiji cha Utalingolo Halmashauri ya Mji Njombe ambapo wananchi walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa vituko hivyo maadili, malezi chanya na makuzi, lishe bora, kinga dhidi ya ukatili wa kijinsia na upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria, Mada hizi zilitolewa na wataalamu kutoka mkoani, Halmashauri na COCODA Tanzania.

07/06/2026

Kila mtoto ana haki ya kuishi katika mazingira salama, yenye ulinzi, upendo na heshima.

Usalama na ulinzi unahusisha:
Kumkinga dhidi ya ukatili na unyanyasaji
Kuzuia ajali nyumbani na shuleni
Kumpatia mazingira salama ya kucheza
Kumlinda dhidi ya kazi na matumizi mabaya ya watoto
Kumsajili na kupata cheti cha kuzaliwa

Mtoto anayelindwa leo anakuwa raia mwema na mwenye mchango chanya kwa jamii kesho.

07/06/2026

Lishe bora husaidia ukuaji wa mwili, ubongo na kinga ya mtoto dhidi ya magonjwa.

Mtoto anahitaji:
Kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 ya kwanza
Vyakula vya makundi mbalimbali baada ya miezi 6
Maji safi na salama
Milo ya kutosha kulingana na umri wake

06/06/2026

Afya bora ni msingi wa ukuaji na maendeleo ya mtoto. Mtoto mwenye afya njema ana uwezo mkubwa wa kujifunza, kucheza na kukua vizuri.

Mambo muhimu katika afya bora ni:
Chanjo zote kwa wakati
Uchunguzi wa afya mara kwa mara
Matibabu ya haraka anapougua
Usafi wa mwili na mazingira
Huduma bora kwa mama wakati wa ujauzito

Kupitia Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) inayo simamiwa na TECDEN kwa kushirikiana na COCODA Tanzania na Serikali inaendelea kuhamasisha wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapata huduma bora za afya tangu kipindi cha ujauzito hadi wanapokua.

COCODA Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii tumefanya uhamas...
06/06/2026

COCODA Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii tumefanya uhamasishaji wa uanzishwaji wa Vituo vya Awali vya Malezi ya Watoto Wakati wa Mchana chini ya Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) inayo simamiwa na TECDEN

Uhamasishaji huo ulifanyika katika Kijiji cha Kitandililo, Halmashauri ya Mji wa Makambako, ambapo wananchi walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa malezi na makuzi bora ya watoto, lishe bora, kinga dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma za msaada wa kisheria.

Lengo la uhamasishaji huu ni kuongeza uelewa wa jamii na kuimarisha ushiriki wa wazazi, walezi na wadau wengine katika kuhakikisha watoto wanapata mazingira salama na bora ya ukuaji na maendeleo yao.

06/06/2026

Address

Chaungingi Street
Njombe
P.O.BOX712

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 14:00

Telephone

+255624890450

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Cocoda Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Cocoda Tanzania:

Shortcuts

Share