Tuli-Hamwe

Tuli-Hamwe Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tuli-Hamwe, Community Service, Mzumbe.

Ni Kikundi cha Kijamii cha wana-Kigoma na watu wenye asili ya Mkoa wa Kigoma(Kwa kuzaliwa, kuoa ama kuolewa na mtu mwenye asili ya Mkoa wa Kigoma) wanaoishi Kata ya Mzumbe, Mlali na Maeneo Jirani

25/12/2025
TULIHAMWE DAY 2025Baadhi ya picha za Matukio ya siku ya TULIHAMWE iliyofanyika 13/12/2025, Mzumbe Morogoro...Kama hujaji...
13/12/2025

TULIHAMWE DAY 2025

Baadhi ya picha za Matukio ya siku ya TULIHAMWE iliyofanyika 13/12/2025, Mzumbe Morogoro...Kama hujajiunga na umoja huu, fanya himu uwasiliane na uongozi wa TULIHAMWE upewe utaratibu wa kuwa mwana umoja.

TULIHAMWE DAY 2025 Wageni Maalum ambao ni watoto wetu wakiendelea kuwasili eneo la tukio hapa ukumbi mdogo wa Kuzilwa......
13/12/2025

TULIHAMWE DAY 2025

Wageni Maalum ambao ni watoto wetu wakiendelea kuwasili eneo la tukio hapa ukumbi mdogo wa Kuzilwa....Hili ni tukio mhimu sana kwa wana TULIHAMWE kwandi ndio tukio pekee la furaha linalokutanisha WANA-TULIHAMWE wote na familia zao!!

21/11/2025

Watoto wetu wengi, tunapoenda kwenye sherehe k**a harusi, sendoff, kitchen party n.k., mara nyingi hubaki nyumbani.

Moja ya malengo ya kuanzisha SIKU YA TULIHAMWE ni kuwapa nafasi watoto wetu nao kufurahi pamoja na watoto wenzao kupitia chakula, michezo na burudani mbalimbali Kwani furaha yao ndiyo furaha yetu.

20/11/2025

Watani Wetu Wangoni Kutoka Mkoa wa Ruvuma Wakitoa Zawadi Yao Wakati wa Siku ya TULIHAMWE.

Katika utamaduni wetu wa asili, tuliorithishwa na wazee wetu, Wangoni, Wakurya na Wahaya ni baadhi ya makabila ambayo ni watani wa Waha. Tumefundishwa kwamba furaha ya mtani wako ni furaha yako, na shida yake ni shida yako. Huu ni msemo ambao umejengeka katika jamii yetu na unasisitiza mshik**ano wa kijamii.

Licha ya kwamba sisi(Waha), tunashirikiana na jamii nzima ya Watanzania, tunahakikisha kwamba tunadumisha pia utamaduni wetu kwa vitendo, hasa kwa kudumisha uhusiano na watani zetu.

Mojawapo ya njia za kuonyesha mshik**ano na kusherehekea pamoja ni kwa kupitia kitu kinachoitwa NGUTO

NGUTO ni mwaliko maalum unaotolewa na mtani wako kukualika kushiriki tukio la furaha au la huzuni. Mwaliko huu huletwa kwa njia ya barua, na mara nyingi huambatana na kiasi cha fedha kisichopungua Tsh. 1,000/=. Ni ishara ya uhusiano wa karibu na kuonyesha mshik**ano na dhihirisho la msaada kwa mtani wako, iwe ni katika nyakati za furaha au majonzi.

20/11/2025

WAMAMA WA TULIHAMWE

Kujiunga na Umoja huu wasiliana na uongozi kupewa utaratibu na sifa za kuwa Mwana Umoja,umoja huu hatubagui jinsia, dini...Ni mhimu sana kujiunga na kuwa sehemu ya vikundi vya kijamii kwani tunasaidiana kwenye shida na Raha.



Mawasiliano: +255656384609

20/11/2025

WAMAMA WA TULIHAMWE WAKICHEZA NGOMA YA KITAMADUNI YA MKOA WA KIGOMA KWENYE SIKU YA TULIHAMWE 2024.

Tukio hili huwaleta pamoja Wana Umoja wa TULIHAMWE pamoja na familia zao na hufanyika kila Mwaka wiki ya Kwanza ya Disemba.

Mwaliko Kwa  WANA TULIHAMWE wa kushiriki tukio hili mhimu linalokutanisha familia zetu
15/11/2025

Mwaliko Kwa WANA TULIHAMWE wa kushiriki tukio hili mhimu linalokutanisha familia zetu

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA YA SIKU YA TULIHAMWE 2024 ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA UKUMBI WA KUZILWA HAPA MZUMBE ...
15/11/2025

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA YA SIKU YA TULIHAMWE 2024 ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA UKUMBI WA KUZILWA HAPA MZUMBE MOROGORO

SIKU YA TULIHAMWETangu mwaka 2022 tulianzisha utamaduni wa kuwa na Siku ya TULIHAMWE, sisi wanatulihamwe tulikubaliana k...
15/11/2025

SIKU YA TULIHAMWE

Tangu mwaka 2022 tulianzisha utamaduni wa kuwa na Siku ya TULIHAMWE, sisi wanatulihamwe tulikubaliana kwamba kila wiki ya kwanza ya mwezi Desemba kila mwaka tutakuwa na siku maalum ya kukutanisha familia zetu.
Ni siku ya pekee ambayo sisi pamoja na watoto wetu tunakusanyika kwa pamoja kumshukuru Mungu kwa kutulinda na kutuvusha miezi 12 ya mwaka.

Katika siku hii tunakula na kunywa vyakula vyetu vya asili, tunashiriki michezo na burudani mbalimbali ikiwemo kutoka kwa watoto wetu. Zaidi ya hayo, huwa tunatoa nasaha kwa watoto wetu, kuwasikiliza mawazo yao, mitazamo yao, pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku.

Maandalizi ya sherehe ya mwaka huu 2025 yanaendelea.
Kwa maelekezo ya ushiriki na utaratibu wa tukio hili, tafadhali wasiliana na viongozi wetu kupitia namba hizi: 0656 384 809 au 0713 551 987

Address

Mzumbe

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tuli-Hamwe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share