AHUKI organization

AHUKI organization Taasisi inayotoa huduma za kijamii kwa makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji. Tunalenga kuboresha maisha kupitia afya, elimu na ustawi wa jamii.

KIKAO CHA UMOJA WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WILAYA YA MAGU. 30/04/2026.Kikao cha mashirika yasiyo ya kiserikali wi...
05/05/2026

KIKAO CHA UMOJA WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WILAYA YA MAGU. 30/04/2026.
Kikao cha mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya Magu mkoani Mwanza, kilifanyika katika Halmashauri ya wilaya kwa lengo la kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za robo mwaka, pamoja na kufanya maandalizi ya jukwaa la mkutano mkuu ujao unaotarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 100.

Kikao hicho kilihudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali wakiwemo Afisa ustawi wa jamii, Afisa mazingira, Afisa elimu msingi, Afisa biashara na Afisa mipango, ambao walitoa mchango wao katika kujadili maendeleo na changamoto za utekelezaji wa shughuli za mashirika.

Uongozi wa kikao ulisimamiwa na mwenyekiti wa mtandao wa mashirika wilaya ya Magu akishurikiana na Katibu pamoja na msajili msaidizi wa mashirika.
Miongoni mwa mashirika yaliyohudhuria ni AHUKI pamoja na mashirika mingine ya maendeleo.

Kwa ujumla, kikao kilikuwa na mafanikio makubwa kwa kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika na serikali, pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kufanikisha mkutano mkuu ujao.

01/03/2026

Nyakato- Mwanza. 26/02/2026.
Baadhi ya wadau wa taasisi zisizo za kiserikali wakishiriki maoni yao juu ya changamoto zinazokabili taasisi zisizo za kiserikali katika usimamizi na uendeshaji wa taarifa hizo.
Mojawapo ya changamoto hizo ikiwemo ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya uendeshaji wa taasisi hizi.
Haya yamezungumzwa katika kikao kilichofanyika kati ya mh. Magreth Baraka , mbunge wa viti maalumu upande wa taasisi zisizo za kiserikali na wadau au wawakilishi wa taasisi hizo mjini Mwanza.

Nyakato, Mwanza | 26/02/2026Mh. Magreth Baraka, Mbunge wa Viti Maalumu upande wa NGO’s, akiwa katika picha ya pamoja na ...
28/02/2026

Nyakato, Mwanza | 26/02/2026

Mh. Magreth Baraka, Mbunge wa Viti Maalumu upande wa NGO’s, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa taasisi zisizo za kiserikali mara baada ya kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu, na kujadili changamoto zinazozikabili taasisi hizo.

Picha hii inaakisi mshikamano na dhamira ya pamoja ya kuendelea kushirikiana kwa ajili ya maendeleo endelevu ya jamii.

🤝 Pamoja tunaweza — kwa ustawi wa jamii yetu

28/02/2026

Tap to view!

Nyakato, Mwanza | 26/02/2026Baadhi ya wadau na wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali wakichangia hoja na kuwasilis...
28/02/2026

Nyakato, Mwanza | 26/02/2026

Baadhi ya wadau na wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali wakichangia hoja na kuwasilisha maoni yao wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu upande wa NGO’s, Mh. Magreth Baraka.

Kikao hiki kilitoa fursa muhimu kwa wadau kueleza uzoefu wao, kubainisha changamoto wanazokutana nazo katika uendeshaji wa taasisi, na kupendekeza maboresho kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii.

🤝 Ushirikiano wa wadau ni nguzo muhimu ya maendeleo endelevu.

NYAKATO-MWANZA.   26/02/2026.Mbunge wa viti maalumu upande wa taasisi zisizo za kiserikali mh. Magreth Baraka akiongoza ...
28/02/2026

NYAKATO-MWANZA. 26/02/2026.

Mbunge wa viti maalumu upande wa taasisi zisizo za kiserikali mh. Magreth Baraka akiongoza kikao kazi na wadau wa taasisi zisizo za kiserikali kilicholenga kufahamiana, kusikiliza changamoto na kuimarisha ushirikiano katika usimamizi na uendeshaji wa taasisi hizo.
Miongoni mwa washiriki wa kikao hicho ni Asasi ya huduma za kijamii( AHUKI) iliyowakilishwa na mkurugenzi wake mh.Hanzi Z. Masindi.

🤝 Tupo pamoja katika kujenga ushirikiano imara kwa maendeleo endelevu ya jamii.
# Ushirikiano # NGO's # Maendeleo ya jamii # Mwanza.

Shughuli mbalimbali na mikutano iliyofanywa na Shirika la AHUKI katika utoaji wa mahitaji mbalimbali Kwa watoto wenye uh...
24/12/2025

Shughuli mbalimbali na mikutano iliyofanywa na Shirika la AHUKI katika utoaji wa mahitaji mbalimbali Kwa watoto wenye uhitaji, katika kata ya Nyigogo, halmashauri ya wilaya ya Magu, mwaka 2024.

24/12/2025
Watoto wenye uhitaji katika hafla ya kupokea vifaa na mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Shirika la AHUKI katika kata y...
24/12/2025

Watoto wenye uhitaji katika hafla ya kupokea vifaa na mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Shirika la AHUKI katika kata ya Nyigogo, halmashauri ya wilaya ya Magu, mwaka 2024.

Address

Magu
Mwanza
103

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AHUKI organization posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share