Amani Girls Organization

Amani Girls Organization We are NGO working to enrich the lives of women and Girls in Tanzania

15/05/2026

Amani Girls Organization imefungua rasmi ofisi mpya kwa lengo la kuendelea kuimarisha elimu, afya na uhifadhii wa jamii kupitia huduma na programu mbalimbali za maendeleo.

Amani Girls Organization na Stromme Foundation Tumewekeza kwenye ujuzi, kwa sababu kumpa kijana ujuzi ni kumpa fursa ya ...
08/05/2026

Amani Girls Organization na Stromme Foundation Tumewekeza kwenye ujuzi, kwa sababu kumpa kijana ujuzi ni kumpa fursa ya kujikwamua kiuchumi na kujenga maisha yenye matumaini.

05/05/2026

LISHE BORA SHULENI.

Kupitia ushirikiano wa Amani Girls Organization na Stromme Foundation, tunaendelea kuhamasisha lishe bora mashuleni ili kujenga afya, kuongeza umakini darasani, na kuhakikisha wanafunzi wanafikia ndoto zao.

01/05/2026

Happy Worker's Day from Amani Girls Organization

24/04/2026

Amani Girls Organization Leo tumefurahi kumpokea ofisini kwetu - mwanamke kijana anayefanya vizuri kwenye tasnia ya mapishi na biashara.

Kupitia mazungumzo yetu, tumejadili namna ambavyo tunaweza kushirikiana katika programu zetu za Young Mothers, ambapo atatumia platform yake kuangazia safari ya mama vijana - changamoto wanazokutana nazo, nguvu walizonazo, na namna bora ya kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Hii ni hatua muhimu ya kuunganisha nguvu za ushawishi na kazi ya kijamii ili kuleta mabadiliko chanya kwa wasichana na wanawake vijana.

Tunaamini kupitia sauti k**a yake, hadithi nyingi zitafikiwa na kugusa maisha ya wengi zaidi.

Karibu sana kwenye safari hii ya mabadiliko.

Amani Girls Organization  inaendelea kutekeleza juhudi za kuwafikia na kuwasaidia wasichana pamoja na vijana wa kiume wa...
14/04/2026

Amani Girls Organization inaendelea kutekeleza juhudi za kuwafikia na kuwasaidia wasichana pamoja na vijana wa kiume waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali.

Kupitia hatua hizi, shirika tunaweka mkazo katika kurejesha fursa za elimu kwa kundi hili, huku likisisitiza umuhimu wa kuhakikisha haki ya msingi ya elimu inapatikana kwa usawa bila ubaguzi.

09/04/2026

Amani Girls Organization kwa kushirikiana na Stromme Foundation wameleta mabadiliko chanya kwa wakulima katika wilaya za Iramba, Manyoni na Ikungi kupitia mafunzo ya kilimo hifadhi chenye mwelekeo wa kibiashara.
Kupitia mafunzo hayo, wakulima wamewezeshwa kutumia mbinu bora za kisasa k**a matumizi ya mbegu bora, utunzaji wa udongo na teknolojia rafiki za kilimo, jambo lililosaidia kuongeza uzalishaji na kuboresha mavuno.
Matokeo yake, wakulima wengi sasa wanavuna kati ya magunia 25 hadi 30 ya mahindi kwa hekari, tofauti na awali ambapo walikuwa wakivuna chini ya magunia 10 kwa hekari, hali inayowawezesha kuwa na uhakika wa chakula na ziada ya kuuza.

Amani Girls Organization Inawatakia nyote Heri ya Sikukuu ya Pasaka!
05/04/2026

Amani Girls Organization Inawatakia nyote Heri ya Sikukuu ya Pasaka!

03/04/2026
"Tulisikiliza igizo la redio k**a familia, na nikatambua kuwa nina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa binti yangu ny...
01/04/2026

"Tulisikiliza igizo la redio k**a familia, na nikatambua kuwa nina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa binti yangu nyumbani, shuleni na hata sokoni. Pia ni muhimu kumtimizia mahitaji yake ya msingi ili aepuke tamaa na vishawishi."

- Mzazi akitoa ushuhuda wake

Leo tupo Kishapu, Shinyanga, tukishiriki matokeo ya utafiti uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 kwa kushirikiana na chini ya mradi wa , unaolenga kuzuia na kupambana na ngono ya kubadilishana zawadi kati ya wasichana wa rika balehe na wanaume watu wazima.

Tunashukuru ushirikiano wa wadau wote waliofanikisha hatua hii muhimu katika kulinda na kuwezesha wasichana.

Kishapu, Shinyanga, Tanzania Amani Girls Organization

Address

Bwiru, Kumalija Street
Mwanza

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255282560538

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Amani Girls Organization posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Amani Girls Organization:

Share