10/09/2024
Mnamo tarehe 6 Septemba 2024 Jukwaa la wanawake Mtwara kupitia Mradi wa Sauti zetu kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania Trust , tumeendesha mdahalo wa siku 1 kwenye kata ya Vigaeni Mtwara , kwa kuwakutanisha Wanawake 83 kutoa elimu na kujadili kuhusu mapambano dhidi ya aina zote za Ukatili , rushwa ya ngono, na umuhimu wa Wanawake kushiriki fursa za Uongozi ikiwepo michakato ya chaguzi zijazo.. Miongoni mwa watoa mada ni Afisa Ustawi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Godlove Miho na Bi. Fidea Ruanda Mkurugenzi wa Shirika la KIMWAM Mtwara.
TGNP WLAC