22/02/2026
*Akiba ya Dharura ni Akili, si Woga* π°π§
Watu wengi hudhani kuwa kuweka akiba ya dharura ni kuogopa maisha.
*Ukweli ni huu* : akiba ya dharura ni akili ya fedha, si woga. Maisha hayana ratiba maalum; dharura hutokea bila taarifa, kwa mtu wa kipato chochote.
Ugonjwa wa ghafla unaweza kutokea. π
Msiba wa familia unaweza kugharimu fedha nyingi.
Majanga k**a ajali, moto, au uharibifu wa biashara yanaweza kutokea.
Hata kupoteza kazi au kushuka kwa kipato kunaweza kukukuta bila kutarajia.
Dharura hizi zikitokea wakati huna akiba, mara nyingi unalazimika kukopa madeni mabaya, kuvunja uwekezaji wako, au kuuza vitu muhimu kwa hasara. Ndipo safari ya uhuru wa kifedha huanza kurudi nyuma.
Akiba ya dharura inakupa utulivu wa akili, inakulinda usiharibu mipango yako, na inakufanya ubaki imara hata maisha yanapobadilika ghafla
π. Lakini kumbuka β hii ni akili moja tu kati ya akili 6 za fedha unazopaswa kujenga.
Unahitaji pia akili ya kutengeneza kipato, matumizi sahihi, kuepuka madeni mabaya, uwekezaji, na kulinda utajiri wako. Hizi ndizo akili zinazokuweka kwenye njia ya uhuru wa kifedha wa kweli.
π Kitabu cha *AKILI YA FEDHA* kinakufundisha kwa lugha rahisi jinsi ya kujenga akili hizi zote na kuishi maisha yenye utulivu wa kifedha.
π₯ Bei ya ofa: Sh 5,000 tu
π² Lipia M-Pesa: 0752 206 899 (Alfred Mwanyika)
π₯ Softcopy: https://vitabu.somavitabu.co.tz/ #/view/shop-item/85/οΏ½
Usisubiri dharura ikufundishe kwa maumivu.
Jifunze sasa β _anza kujenga uhuru wako wa kifedha leo_ π.