Usultani wa Kienembonwe wa Ujiji

Usultani wa Kienembonwe wa Ujiji Ukurasa rasmi wa Usultani wa Kimanyema

Ni Utawala wa kijadi, katika ardhi ya Wamanyema ya Ujiji, kupitia kijumba cha Usultani cha silsila ya Wenembonwe chini ya Sultani, Kolo Malilo II Kizoela Mwenembonwe wa Ujiji(Busonga).

DESTURI YA KUWAKARIBISHA MAHUJAJIKwetu mahujaji, wageni wa Mwenyezimungu hupewa heshima kubwa na wakirejea hukaribishwa ...
01/06/2026

DESTURI YA KUWAKARIBISHA MAHUJAJI

Kwetu mahujaji, wageni wa Mwenyezimungu hupewa heshima kubwa na wakirejea hukaribishwa kwa zafa na rika.

Pia watu huwataka kuwaombea Dua na kuuliza khabari za miji miwili mitukufu ya makka na Madina pamoja na namna walivyomaliza hija yao mji wa makka na walivyomzuru mtume Muhammad (swallallahu alayhi wasallam) mji wa Madina.

Ilivyo desturi ya kwetu; hapo ni nyumba ya Zawiya ya Twarika la Kadiria. Upande wa kushotoni kumeandikwa maneno ya kuwakaribisha Mahujaji wanaotarajiwa kutoka Hijjah, hii ni desturi ya kwetu ya miaka dahari na ni majumba mengi yameandikwa maneno ya kuwakaribisha Mahujaji.

Ghulu lilyo!"Wamanyema hawana mtu baki".Maana yake jamii ambayo ina ndoa nyingi za ndani 'endogamy' familia zao. Wamanye...
01/06/2026

Ghulu lilyo!

"Wamanyema hawana mtu baki".
Maana yake jamii ambayo ina ndoa nyingi za ndani 'endogamy' familia zao.
Wamanyema hasa zamani walikhiyari kuoana wao kwa wao na pia walistahiana kwa mengi, kwa nyumbani hata watoto wa mchanganyiko wa vizazi viwili nyuma si wengi labda kwa pwani.
Familia karibu zote zinamuingiliano mkubwa sana.

Kimila hasa zamani ikijulikana k**a mmeoana na kuna undugu basi ni lazima kutolewa 'mbuzi wa kivunja undugu'. Hekima yake si kuvunja undugu bali kuweka msisitizo kwamba ndugu wa familia moja huwa hawaoani na pia kuweka msisitizo kwamba wahusika waliooana ni ndugu yaani ni jambo moja linalofunza hekima ambazo k**a zinakinzana lakini zinafunza maadili mawili kwa wakati mmoja;
1. Kulinda undugu
2. Kukanya mahusiano ya ndugu wa familia moja

UNDUGU NAUPENDA SANA 🙏

Kutoka;SHIRIKA mpaka MGUMIREK**a,Kutoka;DANI mpaka BEERSHEBA
01/06/2026

Kutoka;

SHIRIKA mpaka MGUMIRE

K**a,
Kutoka;

DANI mpaka BEERSHEBA

UNDANI WA KUIBEZA UJIJI Tunaona kuna kampeni inaanzishwa na vikundi fulani fulani kuibeza ujiji.Je, ni kweli unabezwa ud...
31/05/2026

UNDANI WA KUIBEZA UJIJI

Tunaona kuna kampeni inaanzishwa na vikundi fulani fulani kuibeza ujiji.

Je, ni kweli unabezwa uduni wa maendeleo ya Ujiji?

Hivi, Baa inaweza kuwa kielelezo cha maendeleo badala ya viwanda na miundombinu?

- Tena ya kumilikiwa na mgeni ambaye si raia wa Tanzania na hainufaishi Watanzania.

- Na sheria ipi inampa mgeni ambaye si raia uhalali wa kumiliki ardhi?, na itatwaliwa iwe masabo.

Uchawi unaweza kuzuia maendeleo?
- Hivi Ujiji kuna uchawi wa namna gani ambao Duniani hakuna wa kudhibiti maendeleo?
- Kigoma mahali gani hapajawahi kusifikana kwa hiyo fani?, kwanini hawasemi?
- Hivi Ujiji ina uchawi kushinda Naijeria kusini?, Mfalme tajiri wa kwanza Afrika ni wa Morocco wa pili ni Olugbo wa Ugbo kutoka Naijeria kusini na kuna matajiri wengi mno na wasomi wengi na wako hukohuko uchawini.
- Huyo anayedai Ujiji kuna uchawi ye uchawi anaujua au yeye ndo mchawi?
- Ameshawahi labda hata kushiriki makongamano ya wachawi akapata uzoefu n ithibati maana kusadiki kwa toma ni kuona.
* Majungu, majungu, majungu na kukosa shule.

Ujiji ni wapi?

- Kwa sisi wenyeji, Ujiji ni sawa na Kigoma mjini na kwa zamani ni sawa na mkoa wote wa Kigoma, ukiwa ni wilaya ya Jimbo la magharibi.
Kubeza maendeleo ya Ujiji ni kutukana serikali na hasa halmashauri ya manispaa ya mji ambayo ndiyo inabeba dhamana kubwa juu ya 'ordinances' za mapato na matumizi mbalimbali ya mji k**a ujenzi wa miundombinu na ukusanyaji wa mapato sambamba na utekelezwaji wa sera za kimaendeleo kwa miongozo na bajeti ya serikali kupitia wizara husika. Serikali ambayo inafanya juhudi kila kukicha kuhakikisha maendeleo na miundombinu vinaimarika.
- Kubeza kinachofanyika na kutotaka kukubali mabadiliko ni silika ya harakati za mageuzi ya kisiasa na siyo za kijamii wala kitamaduni.

Je, Usultani unahusikaje kuzuia maendeleo ya kiuchumi?
- Zaidi Usultani umezidi kuitambulisha ujiji na kurudisha ari ya watu kupapenda nyumbani hii inasaidia kuibua fikra mpya za fursa za kiuchumi na mshik**ano wa kijamii ambao ni muhimu katika kuleta maendeleo.

- Pia Usultani haujawahi hata siku moja kupinga harakati zozote halali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
- Wenye uchungu wa ujiji ni magirini tu k**a ni kweli wajikite makwao,

lumbu nguni zhakuta mwinobe zhisizihang'ilwa ngata.

Je, k**a si hivyo kinachobezwa na kutukanwa hapo ni nini?

- Ni chuki tu, wivu, ujinga na kasumba.
Mtu anatoka kale kakijiji ka kituo cha reli cha karibu na Luiche, uchumi wa hako kakijiji ni miwa ya shilingi 500, yeye mwenyewe kwao ana miongo hajafika lakini anapatukana ujiji, eti kwa kigezo ni mji wa zamani unatakiwa kuendelea kabla ya kwao. Hivi hicho kipaumbele ni cha dhati au kisingizio kwao pasisemwe?

Je, kuna nini nyuma ya pazia?
Kuna harakati za kisiasa na kitamaduni....
maendeleo yametumika k**a kichaka. Huwezi kuchagiza maendeleo ya kusiko kwenu tena hujawahi hata kupafika kwa kutoa kashfa na madhaifu ya makazi ya watu ambayo bado wenyewe wamo ndani kwa maneno ya kusikia, kuona picha na kuhisi.
Hivi hata wewe ungejisikiaje?

Wengine wanadiriki kusema watu wa Ujiji wahamishwe....hivi kweli hapo si ni kujificha kwenye shamba la karanga?
Kigoma si ndo ya kwetu sote?
K**a kuhamisha watu ndo kunaleta maendeleo kuna mapori ya hekari ngapi ya bure huko makwao kwanini wasitoe mawazo yakawa miji mizuri wanayotaka kuiona?

Hizi ni harakati za hao wanaharakati mchombezo kutishia uwepo wa jamii yetu na wamekosa njia...chuki iliyoje!!!!

Kibalo ni lijitu kubwa k**a likizimgara ukishindana nalo litakumeza!!

Watu ambao harakati za kijamii za mkoa zikianzishwa wanajimega na kuanzisha vikundi vyao vya kiuasi vyenye sura ya Vicoba na Saccos mchombezo, hawawezi kufika mbali wala kupata mafanikio kwasababu wamekosa baraka kwa usaliti.

Elimu ya mjinga siku zote ni majungu..

Wameachwa na jopo la Kibalo kwa kupuuzwa ila watarudishwa mezani ikiwa wataparama maana tuko nao k**a vivuli vyao.
Muhimu kujikita kwenye hoja na mijadala yenye tija , kibalo kina mbinu zaidi ya 100 kuzima majaribio yasiyo na tija.
Wawe makini, wawe makini, wawe makini.

IDUMU MAKKA NDOGO🤲
IDUMU UJIJI NA BUSAIDI YAKE🤲
UDUMU UUNGWANA WA JAMII YETU 🤲
UDUMU USULTANI WA KIMANYEMA WA KIENEMBONWE WA UJIJI 🤲
ADUMU KOLO MALILO II SULTANI NA KILUNGA WETU🤲

Mwailizhe!Karibu Ujiji, mji uliobarikiwa kwa neema nyingi.
31/05/2026

Mwailizhe!

Karibu Ujiji, mji uliobarikiwa kwa neema nyingi.

Hawamlindi Mwami wao,Wanalinda ukazi wa kichuguu chao k**a ishara ya uwepo wao, umoja na mshik**ano wao.
31/05/2026

Hawamlindi Mwami wao,
Wanalinda ukazi wa kichuguu chao k**a ishara ya uwepo wao, umoja na mshik**ano wao.

SULTANI KUWAOMBEA BARAKA WENEKIBALO NA WAKWAKIBALOKwenye Sherehe za kusimika Riwaya, Sultani hukutana na Wenekibalo pamo...
31/05/2026

SULTANI KUWAOMBEA BARAKA WENEKIBALO NA WAKWAKIBALO
Kwenye Sherehe za kusimika Riwaya, Sultani hukutana na Wenekibalo pamoja na kuwaombea Baraka, muda wa kuwaombea Baraka huwa ndiyo kilele cha Sherehe yenyewe na kufuatiwa na dhifa ya mafungu.

Dhifa itatolewa kwa ukubwa wa nyumba za Wamanyema.

Yaani nyumba zitatoa dhifa zake k**a sehemu ya uwepo wake

Dhifa ya Wagoma
Dhifa ya Wabwari
Dhifa ya Wakusu
Dhifa ya Wabangubangu n.k

Kuna Dhifa zinazotelewa na makundi;
Dhifa ya Wakwakolo - Watu wa nyumba ya Kisultani
Dhifa ya Wakwanakolo - Dhifa ya Familia ya Mama Malkia
N.k.

HAFLA NA MATUKIO KATIKA USULTANI WA KIMANYEMA  Kuna Sherehe ya MlambuKuna Matamasha mengine ya kitamaduni Lakini Sherehe...
31/05/2026

HAFLA NA MATUKIO KATIKA USULTANI WA KIMANYEMA

Kuna Sherehe ya Mlambu
Kuna Matamasha mengine ya kitamaduni
Lakini Sherehe kuu muhimu za Usultani wetu ziko 4
- Sherehe ya kutawazwa Sultani
- Sherehe ya kusimika Riwaya
- Dhifa za Idi mbili
- Ijaza ya Wali Ahad (Mrithi wa Usultani)
Mbili za kati hurudiwa katika hizo 4.

Sherehe ya kusimika Riwaya ndiyo pekee inaweza kurudiwa kwa mwaka kadri ya itakavyotakiwa au kuwezekana.....
Na ndiyo ishara endelevu ya urithi wa malezi ya kiroho ya Usultani wetu.

KUSIMIKA RIWAYA pia siyo kuichomeka mahali bali pale Sultani k**a Swahibul Maqam wa Zawiya-Ngolo anapoik**ata kwenye daira, kusoma talakini yake na Kisha kuketi nayo akiwa ameishika kabla haijawekwa kwenye makamu.

Sherehe ya kusimika Riwaya inatarajiwa kufanyika Busaidi, Ujiji muda wowote itakapotajwa baada ya maandalizi kukamilika.

ITABAKI KUWA NI HAFLA YA KIPEKEE KWASABABU MSINGI WAKE SIYO BURUDANI BALI KURITHISHA FIKRA NA ITIKADI YA MAANA YA UMUHIMU WA MAMLAKA YA KIROHO YA USULTANI WA BABU ZETU.

"Wanaotubeza kwa;Kuathiriana kitamaduni - ni tabia binaadamu kuathiriwa na anaochangamana nao, wawe wabantu, wazungu, wa...
31/05/2026

"Wanaotubeza kwa;

Kuathiriana kitamaduni - ni tabia binaadamu kuathiriwa na anaochangamana nao, wawe wabantu, wazungu, wahindi au Waarabu. kuathiriana hakuna mipaka k**a kwa huyu ndo sawa kwa huyu si sawa, HAPA TUNAWAONA WATU WEUSI WAKIPIGA MBIU YA KUJIKOMBO KWA SLOGANS ZA KIBAGUZI ZILEZILE WANAZOZIKATAA DHIDI YAO.

Dini na utamaduni - Kuna baadhi ya jamii dini na utamaduni wake haviwezi kutenganishika ni sehemu ya turathi zake na kiini cha jamii yao, ya kwetu ni miongoni mwa hizo jamii. Kuna harakati za Wakushi sijui dini ya watu weusi kubeza uongozi wa jadi wa jamii yetu na ulezi wake wa kiroho wa kiislamu.
Miskiti ya Manyema ni kielelezo kikubwa cha historia na turathi za jamii yetu ambayo ilienea tangu zamani kila mkoa na ikawa ni sehemu ya mikusanyiko ya kijamii kwetu baada ya ibada.

Kamwe hatuwezi kukubali kupoteza kilichotuinua kwa kutaka kuwaridhisha watu wa tamaduni nyingine hilo ni kinyume na misingi ya kuvumiliana kiimani "religious tolerance" maana tunaienzi historia yetu na utambulisho wetu bila kuzuia jamii nyingine kuenzi ya kwake.

Sisi hatuoni haya wala wasiwasi kuhifadhi kilicho chetu, pia zipo jamii nyingi mno Afrika za mfano wetu isipokuwa kutofahamu mambo au ndo tuseme ujinga, wakati mwingine hutengeneza kanuni yake, mazuri waliyotuachia mababa zetu hatuwezi kuyaacha kwa ushauri wa jirani ambaye wala hakuwa sehemu ya hatma yetu.

Turathi zetu na Utambulisho wetu tutavilinda kwa wivu mkubwa mno.

Tunajivunia kuwa miongoni mwa jamii chache na za kipekee sana katika mbari ya kibantu, tena sisi ni wabantu kuliko hao wanaojiona ni wabantu zaidi yetu."

TAMKO LA SULTANI JUU YA MMOMONYOKO WA MAADILI HASA MAMBO YA AKHERI ZAMANI "Tunafuatilia kwa makini mambo yote ya maadili...
31/05/2026

TAMKO LA SULTANI JUU YA MMOMONYOKO WA MAADILI HASA MAMBO YA AKHERI ZAMANI

"Tunafuatilia kwa makini mambo yote ya maadili hasa kwa vijana wetu huku tukizingatia utaratibu na misingi ya sheria, mambo mengi hufanyika falagha na hayawezi kukisiwa maana sivyo mambo ya sheria yalivyo. Pia kazi yetu ni walimu wa maadili na kukemea wala hatuna mamlaka ya kumhukumu mtu jinai. Pia kuhusu uwepo wa wapishi na wauzaji wa pombe za kienyeji ambazo hukatazwa pia kisheria na matumizi ya mihadarati tutaangalia namna ya kushirikiana na jeshi la polisi katika kulifanikisha hilo. Katika duru za Usultani huwa kuna idadi ya Wagabo wanaotakiwa kuratibu mambo hayo ambayo yenyewe mawanda yake ni mapana zaidi, siyo jambo la kukurupuka na la mara moja. Asili ya sheria za kimaadili hasa za kijamii siyo kukomesha binaadamu asikosee kabisa bali kuzuia makosa kupata kibali na kuwa sehemu ya maisha ya kawaida, maana mambo mengi hufanyika falagha na pia kuna haki ya falagha ya mtu na huko hatuwezi kufika.

Kwa wanaopasema Ujiji, tunajua kwa vile si kwao na pia desturi zetu nzuri si zao na kila chetu si chao, ni wazi wivu, roho ya fihi na chuki binafsi.
ZIDUMU DESTURI ZA WAMANYEMA."
Kolo Othman Malilo II wa Wamanyema.

Address

Busaidi, Ujiji
Kigoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Usultani wa Kienembonwe wa Ujiji posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share