Coast Region Press Club

Coast Region Press Club JOURNALIST CLUB

CHADEMA PWANI WAUNGA MKONO MAAZIMIO YA KAMATI KUU ,YATAKA WALIOHUSIKA NA VURUGU ZA OKTOBA 29/2025 WACHUKULIWE HATUANa Gu...
08/05/2026

CHADEMA PWANI WAUNGA MKONO MAAZIMIO YA KAMATI KUU ,YATAKA WALIOHUSIKA NA VURUGU ZA OKTOBA 29/2025 WACHUKULIWE HATUA

Na Gustaphu Haule,Pwani

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Pwani kimeunga mkono maazimio 12 yaliyopitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho na kutaka wale waliohusika na vurugu za Oktoba 29 wachukuliwe hatua za kisheria.

Maazimio hayo yameungwa mkono katika mkutano uliofanyika Mei 07/2026 katika Manispaa ya Kibaha kwa  kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa Jimbo na  Wilaya wa Mkoa wa Pwani.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Pwani Richard Mbalase amesema mbali na kuungana mkono maazimio ya k**ati kuu lakini pia mkutano huo umetumika kuwasilisha taarifa ya uchambuzi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG).

Mbalase amesema Kamati Kuu ya Chadema iliketi katika kikao chake Aprili 28 hadi Aprili 29/2026 ambapo katika kikao hicho walijadili na kupokea taarifa ya hali ya kisiasa nchini kuanzia Novemba 25/2025 hadi Aprili 24/2026.

Amesema Katika kikao hicho Kamati Kuu ya Chadema iliyokuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti John Heche imepitisha maazimio mbalimbali yanayopaswa kuungwa mkono na viongozi wote wa Tanzania Bara na Tanzania visiwani.

Mbalase, baadhi ya maazimio hayo ni kuhamasisha na kuomba umma wa Watanzania kusimama na wapenda haki kushirikiana na mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lissu ili kusudi aweze kuachiliwa bila masharti yoyote.

Amesema azimio lingine ni kutowatambua viongozi waliochaguliwa Oktoba 29/2025 kwakuwa hawakupata ridhaa ya Wananchi, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika vurugu za Oktoba 29/2025,kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa matukio ya vurugu ya Oktoba 29 na kuhakikisha familia zilizopoteza wapendwa wao wanalipwa fidia.

Maazimio mengine kuanzishwa kwa Katiba Mpya, kuanza rasmi kwa oparesheni ya mikutano ya hadhara ya kisiasa nchi nzima itakayojulikana kwa jina la Oparesheni Katiba Mpya,Free Tundu Lissu na kuwaongoza Wananchi kudai hatua za haraka za kupunguza bei ya mafuta.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bumija Senkondo akiwasilisha taarifa ya uchambuzi wa ripoti ya CAG ametaka waliotajwa katika ripoti hiyo kuchukuliwa hatua mara moja.

MWENGE WA UHURU KUNG'ARISHA  MIRADI  8 YA SH.BILIONI 41.1  MANISPAA YA KIBAHA .Na Gustaphu Haule,PwaniMbio za Mwenge wa ...
21/04/2026

MWENGE WA UHURU KUNG'ARISHA MIRADI 8 YA SH.BILIONI 41.1 MANISPAA YA KIBAHA .

Na Gustaphu Haule,Pwani

Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeingia katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha leo Aprili 21/2026 ambapo jumla ya miradi nane yenye thamani ya Sh.bilioni 41.1 itapitiwa kwa kuzinduliwa na kuwekwa mawe ya Msingi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa  amesema hayo wakati akiwa anapokea  Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Regina Bieda.

Mapokezi ya Mwenge huo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Visiga iliyopo Kata ya Visiga Manispaa ya Kibaha na kushuhudiwa na watumishi pamoja na Wananchi mbalimbali.

Baadhi ya miradi hiyo itawekewa jiwe la Msingi katika kiwanda cha Doweicare Technology Ltd kinachozalisha pampers ,taulo za like na wips,kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Kongowe - Forest,kukagua jiko la nishati Safi na salama la kupikia.

Miradi mingine kiwanda cha J-Chalya Plumbing Services kwa ajili ya kukagua shughuli za kikundi za uuzaji na utengenezaji wa mabomba ya maji pamoja na kuzindua vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Picha ya Ndege.

Pia ,Mbio za Mwenge wa Uhuru utazindua huduma za afya katika Zahanati ya Kilimahewa,kuzindua kisima kirefu cha maji safi shule Msingi Tangini pamoja na kukagua mradi wa Kibaha Shopping Mall.

 

Mwisho.

17/04/2026

MKURUGENZI WA MANISPAA YA KIBAHA DKT. ROGERS SHEMWELEKWA AWAFUTA AIBUA SHANGWE KWA WALIMU MALIPO YA FEDHA ZA LIKIZO.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa awafuta machozi walimu wa Shule za Msingi na Sekondari juu ya fedha za likizo ,na madeni mengine mbalimbali.

Amesema walimu waliokuwa wameenda likizo Desemba 2025 wote walilipwa fedha zao na wale ambao wataenda likizo Juni 2026 wataanza kupokea fedha hizo kwenye akaunti zao kuanzia Leo Aprili 17/2026 na anataka kuhakikisha walimu wote wanapata fedha zao mapema kabla ya kwenda likizo.

Dkt.Shemwelekwa ameweka bayana suala hilo katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari waliofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa ya Mwaka 2025 hafla ambayo ilifanyika Aprili 16/2026 katika ukumbi wa Kibaha Shopping Mall.

Mwisho.

Mwisho

02/04/2026

CCM PWANI YAMPA HEKO RAIS SAMIA

Na Gustaphu Haule,Pwani

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimeendelea kutambua mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya Mkoa na Taifa kiujumla .

Aidha, kutokana na mchango huo, CCM Mkoa wa Pwani kimeona ni vyema kikaendelea kumpongeza Rais Samia kwa namna ambavyo ameung'arisha Mkoa wa Pwani kwa kuleta maendeleo yanayoonekana kwa macho.

Katibu wa Siasa , Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Pwani David Mramba,amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 02/2026 katika ofisi za Chama hicho.

Mramba ,amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026 Mkoa wa Pwani ulitengewa kiasi cha Sh.bilioni 473 fedha ambazo zilitumika kuleta maendeleo ndani ya Mkoa wa Pwani.

Amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali kupitia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza fedha za maendeleo na kupanga kutumia kiasi cha Sh.bilioni 497.1 na hiyo inaonyesha dhahiri kuwa Mkoa wa Pwani upo moyoni mwa Rais Samia.

Amesema sekta ya maji ilikuwa ni changamoto kubwa lakini Rais Samia ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miradi mikubwa ya maji ambapo kwasasa Vijiji vingi vinapata maji Safi na salama lakini Wanawake na watoto wamepunguziwa adha ya kubeba maji kwenye ndoo katika umbali mrefu.

Kuhusu elimu Mramba amesema kuwa Dkt.Samia ametoa fedha nyingi ambazo zimetumika kujenga madarasa mapya yaliyokamilika,maabara zimejengwa na vyoo vya Shule vimeboreshwa na kupelekea watoto kusoma katika mazingira mazuri zaidi kuliko zamani.

Mramba ameongeza kuwa katika sekta ya afya huduma zimeimarika kwa Zahanati kujengwa ,vituo vya afya kuboreshwa na huduma za mama na mtoto zimeimarika na kufanya wananchi kupata huduma karibu na makazi yao na kwamba hiyo inaonyesha Dkt .Samia anajenga Taifa lenye watu wenye afya bora.

Mramba amesema kuwa katika sekta ya miundombinu wameona namna barabara zilivyojengwa na nyingine kuboreshwa na leo wanakila sababu ya kujivunia kuona mazao yanasafirishwa na yanafika sokoni kirahisi,biashara kuongezeka na kwamba hayo ni matunda ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Mwisho.

MANISPAA YA KIBAHA YANUNUA MAGARI MAPYA SABA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI WAKE.Na Gustaphu Haule ,KibahaHALMAS...
31/03/2026

MANISPAA YA KIBAHA YANUNUA MAGARI MAPYA SABA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI WAKE.

Na Gustaphu Haule ,Kibaha

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha imenunua magari saba mapya yenye thamani ya Sh.bilioni 1 na milioni 356 kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Ununuzi wa magari hayo ulipitishwa na Baraza la Madiwani kupitia bajeti hiyo, ambapo magari hayo yanatarajiwa kutumika katika idara mbalimbali za Halmashauri kwa ajili ya kuwahudumia wananchi pamoja na kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa mapato.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, amesema ununuzi wa magari hayo ni utekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati.

Amesema kuwa magari hayo yamenunuliwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri jambo linaloonesha mafanikio katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa fedha za umma.

“Tunazingatia maono ya Mheshimiwa Rais kwa kuhakikisha tunakusanya mapato kwa ufanisi na kuyatumia kuboresha huduma kwa wananchi, lengo likiwa ni kupeleka tabasamu kwa wakazi wa Manispaa ya Kibaha,” amesema Dkt. Shemwelekwa.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, ameipongeza menejimenti ya Halmashauri hiyo kwa mafanikio ya ukusanyaji wa mapato, akieleza kuwa manispaa hiyo imeshika nafasi ya pili kati ya halmashauri 184 nchini.

Amesema mafanikio hayo yanaakisi utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye anatamani kuona wananchi wanahudumiwa kwa haraka na changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

“Tunapaswa kuhakikisha magari haya yanatumika k**a ilivyokusudiwa hasa katika ukusanyaji wa mapato na kuboresha huduma kwa wananchi ili kuongeza bajeti ya maendeleo,” amesema Dkt. Mawazo.

Naye Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu, Mrisho Mlela amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali watumishi wa umma, akibainisha kuwa ununuzi wa magari hayo utasaidia kuongeza ufanisi wa kazi.

MWENYEKITI CCM KIBAHA MJINI AWATOLEA UVIVU WATUMISHI WA MANISPAA .Na Gustaphu Haule,PwaniMWENYEKITI wa Chama Cha Mapindu...
29/03/2026

MWENYEKITI CCM KIBAHA MJINI AWATOLEA UVIVU WATUMISHI WA MANISPAA .

Na Gustaphu Haule,Pwani

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka ametoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa hiyo ili hiweze kukamilika kwa wakati.

Nyamka ametoa maelekezo hayo katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Kibaha Mjini uliofanyika Machi 27 /2026 kwa ajili ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025.

Amesema Halmashauri Kuu ya CCM imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Kibaha kwani bila Rais kutoa fedha Kibaha kusingekuwa na miradi ya maendeleo.

Nyamka amesema Halmashauri Kuu ya CCM Kibaha Mjini imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo kwakuwa ilifanya ziara ya kuitembelea na imeona namna ambavyo miradi ilivyotekelezwa vizuri japokuwa ipo baadhi ya miradi ambayo bado haijakamilika.

Amesema miradi ambayo bado haijakamilika ni lazima watumishi wa Manispaa ya Kibaha chini ya Mkurugenzi wake Dkt. Rogers Shemwelekwa wahakikishe miradi hiyo inakamilika kwa muda uliopangwa na ikiwezekana mkandarasi asimamiwe kufanyakazi usiku na mchana k**a ambavyo Wachina wanafanya.

"Sisi Halmashauri Kuu ya CCM Kibaha Mjini tumeridhishwa na utekelezaji wa ilani katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025 iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha lakini tunatoa maelekezo kuwa miradi ambayo bado kukamilika isimamiwe kikamilifu ili hiweze kukamilika kwa muda uliopangwa,"amesema Nyamka.

Pia Nyamka amesema Halmashauri Kuu imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na kuiwezesha Manispaa hiyo kushika nafasi ya pili Kitaifa.

Amesema wakati mkurugenzi huyo anaingia Kibaha alikuta mapato yanayokusanywa ni Sh.bilioni 7 lakini hadi sasa amefikisha ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya Sh.bilioni 17 huku akiwa na malengo ya ukusanyaji wa mapato hayo hadi kufikia Sh.bilioni 30.

*BoT YASHIRIKISHA WADAU MPANGO WA KUANZISHA KAMPUNI YA UDHAMINI WA MIKOPO*Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikiongozwa na Nai...
12/03/2026

*BoT YASHIRIKISHA WADAU MPANGO WA KUANZISHA KAMPUNI YA UDHAMINI WA MIKOPO*

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikiongozwa na Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, imefanya kikao na wadau mbalimbali kujadiliana kuhusu mpango wa kuanzishwa kwa kampuni ya utoaji na usimamizi wa dhamana za mikopo itakayojulikana k**a Tanzania Credit Guarantee PLC.

Kikao hicho kilichofanyika leo, tarehe 12 Machi 2026, katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam, kimewakutanisha wadau kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kampuni za Bima, Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji wa Mitaji, Mifuko ya Pensheni pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mpango wa kuanzishwa kwa kampuni hiyo unalenga kuendana na ukubwa na kasi ya utekelezaji unaohitajika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inalenga kuimarisha uchumi wa Tanzania na kuongeza mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya taifa.

Vilevile, kampuni hiyo itasaidia kutenganisha majukumu ya Benki Kuu ya udhibiti na utoaji wa dhamana za mikopo, hivyo kuondoa mgongano wa maslahi na kuboresha ufanisi wa kiutendaji. Pia itahamasisha ubunifu pamoja na kuongeza uwezo wa taasisi husika kujibu kwa haraka mahitaji ya soko.

Kwa sasa, Benki Kuu ya Tanzania inasimamia mifuko miwili ya udhamini wa mikopo ambayo ni Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Mauzo ya Nje (Export Credit Guarantee Scheme – ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SME Credit Guarantee Scheme – SME-CGS).

Serikali ilianzisha mifuko hiyo kwa lengo la kudhamini benki na taasisi za fedha ili kuimarisha utoaji wa mikopo kwa wakopaji wenye miradi yenye tija lakini wanaokabiliwa na upungufu wa dhamana. Lengo kuu ni kuwezesha mazingira rafiki ya kukuza na kuendeleza miradi ya maendeleo, kuongeza ajira, kuimarisha upatikanaji wa fedha za kigeni kupitia mauzo ya nje na kuchangia ukuaji wa pato la Taifa.

07/03/2026

DIWANI WA KATA YA TANGINI ANTHONY MILAO AIBUKIA KIJIWE CHA WAZEE WA TAWI LA GUNEWE KUTEKELEZA AADI YAKE.

Na Gustaphu Haule,Pwani

DIWANI wa Kata ya Tangini Anthony Milao leo Machi 07,2026 amekutana na wazee wa kijiwe cha kahawa kilichopo tawi la Gunewe Mtaa wa Tangini kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo.

Pamoja na kuzungumzia masuala ya maendeleo lakini pia Milao alifika katika kijiwe hicho kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake kwa wazee hao aliyotoa kipindi cha kampeni ya uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025.

Milao aliwaahidi wazee hao kuwasaidia kuimarisha banda lao la Kahawa ili hata mvua inaponyesha wawe katika mazingira mazuri ambapo amewakabidhi wazee hao kiasi cha Sh.200,000 kwa ajili ya ujenzi wa banda hilo.

Katibu wa wazee wa Kijiwe hicho Mzee Mbongo amemshukuru diwani huyo kwa kutekeleza aadi yake huku akisema fedha aliyoitoa itafanyakazi iliyokusudiwa na mara baada ya kukamilisha banda hilo watamualika kwenda kutembelea.

Mbongo,amesema wazee wamefurahia kumpata diwani ambaye mchapakazi na mwenye kujali wazee na hatua ambayo ameianza wao watakuwa tayari kumpa ushirikiano katika shughuli zote za kimaendeleo ili Kata ya Tangini iweze kusongambele zaidi.

Hatahivyo,Mbongo amesema kuwa Kijiwe hicho kinajumla ya wazee 25 huku wakiwa wanasimamiwa na uongozi wa Umoja wa wazee Kata ya Tangini ukiwa chini ya mwenyekiti wake Hassan Lugano.

Mwisho.

07/03/2026

DIWANI KATA YA TANGINI AKUTANA NA WAZEE WA KIJIWE CHA KAHAWA TAWI LA GUNEWE KUTEKELEZA AADI YAKE.

Na Gustaphu Haule,Pwani

DIWANI wa Kata ya Tangini Anthony Milao leo Machi 07,2026 amekutana na wazee wa kijiwe cha kahawa kilichopo tawi la Gunewe Mtaa wa Tangini kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo.

Pamoja na kuzungumzia masuala ya maendeleo lakini pia Milao alifika katika kijiwe hicho kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake kwa wazee hao aliyotoa kipindi cha kampeni ya uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025.

Milao aliwaahidi wazee hao kuwasaidia kuimarisha banda lao la Kahawa ili hata inaponyesha mvua wawe katika mazingira mazuri ambapo amewakabidhi wazee hao kiasi cha Sh.200,00 kwa ajili ya ujenzi wa banda hilo.

Katibu wa wazee wa Kijiwe hicho Mzee Mbongo amesema anamshukuru diwani huyo kwa kutekeleza aadi yake huku akisema fedha aliyoitoa itafanyakazi iliyokusudiwa na mara baada ya kukamilisha banda hilo watamualika kwenda kutembelea.

Mbongo,amesema wazee wamefurahia kumpata diwani ambaye mchapakazi na mwenye kujali wazee na hatua ambayo ameianza wao watakuwa tayari kumpa ushirikiano katika shughuli zote za maendeleo ili Kata ya Tangini iweze kusongambele.

Hatahivyo,Mbongo amesema kuwa Kijiwe hicho kinajumla ya wazee 25 huku wakiwa wanasimamiwa na uongozi wa Umoja wa wazee Kata ya Tangini ukiwa chini ya mwenyekiti wake Hassan Lugano.

Mwisho.

MANISPAA YA KIBAHA YAWAITA WANANCHI KUSHIRIKI BURUDANI NA NYAMA CHOMA KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANAWAKE DUNIANI.N...
05/03/2026

MANISPAA YA KIBAHA YAWAITA WANANCHI KUSHIRIKI BURUDANI NA NYAMA CHOMA KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANAWAKE DUNIANI.

Na Gustaphu Haule.

HALMASHAURI  ya Manispaa ya Kibaha imeandaa tamasha maalum la burudani pamoja nyama choma  pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza Machi 4, 2026, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Kibaha Leah Lwanji amesema kuwa tamasha hilo linafanyika katika viwanja vya Stendi ya zamani MailiMoja Kibaha likiwa na lengo la kuwapatia wananchi fursa ya kupata huduma mbalimbali pamoja na kushiriki katika maadhimisho hayo.

Lwanji ,amesema miongoni mwa huduma za kijamii zinazotolewa ni elimu kuhusu matumizi ya nishati safi, elimu ya fursa za uwezeshaji wanawake kiuchumi, huduma za upimaji wa afya pamoja na uchangiaji wa damu, msaada wa kisheria, na kliniki ya ardhi kwa ajili ya kushughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi.

Aidha,Lwanji amesema  maadhimisho hayo pia yameambatana na maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa na wanawake wajasiriamali wa Manispaa ya Kibaha  ambapo wananchi wanapata fursa ya kujionea na kununua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali hao.

Amewaomba Wananchi kutembelea maonyesho hayo kwa lengo la kujionea bidhaa mbalimbali pamoja na kuunga mkono jitihada za wanawake wajasiriamali katika kukuza uchumi wao.

Amesema wananchi wote wanakaribishwa kwa wingi kutembelea viwanja vya Stendi ya zamani MailiMoja Kibaha ili kujipatia bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali wa eneo hilo, kufurahia nyama choma pamoja na kupata huduma muhimu zinazotolewa katika maadhimisho hayo.

Mwisho.

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI HAMOUD JUMAA ( MZEE WA SAMBUSA ) AWAMWAGIA SHUKRANI WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU .Na Gustaphu Ha...
25/02/2026

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI HAMOUD JUMAA ( MZEE WA SAMBUSA ) AWAMWAGIA SHUKRANI WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU .

Na Gustaphu Haule, Pwani

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ( Mzee wa Sambusa) amekutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Kata Sita zilizopo katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Mlandizi na kuwataka waendelee kushik**ana kwa ajili ya kukiendeleza Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Aidha,Jumaa amewaomba wajumbe hao kuhakikisha wanavunja makundi kwakuwa kazi ya uchaguzi imekwisha na sasa kila mmoja awajibike katika nafasi yake kuhakikisha wanafanya shughuli moja ya kuwaletea Wananchi maendeleo.

Jumaa ametoa kauli hiyo leo Februari 25/2026 katika kikao maalum kilichofanyika karibu na stendi ya daladala ya Mji wa Mlandizi akiwa na lengo la kuwashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu kwa kazi kubwa waliyoifanya hususani ya kuhakikisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anashinda katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Amesema mbali na Rais lakini pia kutoa shukrani kwa viongozi hao kwa kumchagua yeye kuwa mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini pamoja na kuwachagua madiwani 19 wanaotokana na CCM.

"Nimekuja kukutana nanyi katika kikao hiki cha Halmashauri Kuu kwa ajili ya mambo makubwa mawili,kwanza nikuwashukuru kwasababu ya kunichagua mimi kuwa mbunge wenu pamoja na madiwani wote ambao wanatokana na CCM lakini pili kuwashukuru kwasababu ya kumchagua Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania ",amesema Jumaa.

Jumaa amesema Rais Samia anakwenda kumaliza muda wake lakini anapokwenda kumaliza ana mambo mengi ya kufanya ambayo mengine aliyaanza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na mengine atayanzisha miaka hii mitano.

Amesema kipindi hiki ndio kipindi ambacho Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anahitaji ushirikiano mkubwa na wa kutosha ili kusudi kila alichokipanga aweze kukikamilisha kwa wakati.

Jumaa amewaomba kuendelea kushik**ana na kuwa wa moja kwa ajili ya kukiendeleza chama chao huku akisema anajua viongozi hao walikuwa katika makundi na wamepambana katika uchaguzi mkuu kwa ajili ya kumpata mbunge na madiwani lakini mwisho wa siku makundi yote yanavunjwa na linabaki kundi Moja kwa maslahi ya Chama.

Mwisho

Address

Mailimoja
Kibaha
15

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Coast Region Press Club posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Coast Region Press Club:

Share