20/06/2026
Katika kipindi cha maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoanza rasmi mwezi Aprili na kuhitimishwa tarehe 16 Juni 2026, Iringa Recovery Community (IRC) ilipata nafasi kubwa ya kushiriki kikamilifu kupitia Mwanasaikolojia John John, ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa K**ati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo ndani ya Manispaa ya Iringa.
Kupitia nafasi hiyo, Mr. John John Psychologist JOHN JOHN ameongoza shughuli mbalimbali za utoaji elimu katika maeneo tofauti ya Manispaa ya Iringa, akigusia mada muhimu zenye lengo la kumlinda na kumjenga mtoto wa Afrika. Mada hizo zimehusisha ukatili dhidi ya watoto, afya ya akili, kujitambua, pamoja na masuala mengine muhimu yanayolenga kupinga ukatili wa aina yoyote dhidi ya mtoto.
Maadhimisho haya yamefanikiwa kufanyika kwa ushirikiano mkubwa kati ya Serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo, na taasisi zinazofanya kazi za kijamii ndani ya Manispaa ya Iringa. Kwa niaba ya wadau wote, Mr. John John alipata nafasi ya kutoa hotuba yenye ujumbe mzito na wa kugusa maeneo muhimu katika harakati za kutetea haki, usalama, na ustawi wa mtoto wa Kiafrika.
K**a taasisi, IRC itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kupinga ukatili dhidi ya watoto na jinsia, kusimamia haki za binadamu, na kutoa elimu pamoja na msaada wa kisaikolojia na afya ya akili kwa jamii. Tunaamini kuwa kupitia ushirikiano na Serikali pamoja na wadau wengine, tunaweza kuendelea kuikomboa jamii yetu kiakili, kijamii na kiuchumi.
Endelea kutufuatilia kupitia kurasa zetu kwa taarifa zaidi kuhusu kazi tunazoendelea kufanya katika kuijenga jamii salama, yenye afya na matumaini kwa watoto, vijana na familia kwa ujumla πβ¨
NB: Mtuwie radhi kwa uhafifu wa video hii, ila kwa umuhimu wake imetulazimu kuitumia.