11/03/2026
WEL ORGANIZATION YATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, taasisi isiyo ya kiserikali ya WEL Organization (Women for Education and Leadership) imetembelea kituo cha watoto yatima kwa lengo la kuwafariji, kuwapa msaada na kuwahamasisha watoto wa k**e kujitambua na kuthamini uwezo wao tangu wakiwa wadogo.
Ziara hiyo imelenga kuonesha upendo na mshikamano kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, huku viongozi na wanachama wa taasisi hiyo wakitoa ujumbe wa matumaini, motisha na kuwatia moyo watoto hao kuendelea kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao za baadaye.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, muwakilishi Ndg. wa WEL Organization amesema kuwa taasisi hiyo inaamini kuwa kumjengea mtoto wa k**e kujiamini na kujitambua mapema ni msingi muhimu wa kumuwezesha kuwa kiongozi bora katika jamii siku zijazo. Ameongeza kuwa watoto hao wanahitaji upendo, uangalizi na fursa sawa za elimu ili waweze kufikia malengo yao.
Mbali na ziara hiyo, WEL Organization pia imejipanga kuendesha kampeni ya kutoa elimu kwa mabinti katika shule mbalimbali za Mkoa wa Iringa kuhusu umuhimu wa hedhi salama. Kupitia kampeni hiyo, taasisi itatoa elimu kuhusu afya ya uzazi, usafi wakati wa hedhi na namna ya kujitunza ili kuepuka changamoto zinazoweza kuathiri afya na masomo ya wasichana.
Aidha, katika hatua ya kuimarisha afya na ustawi wa mabinti shuleni, taasisi hiyo pia imepanga kugawa taulo za k**e salama na safi kwa wanafunzi wa k**e ili kuwasaidia kuhudhuria masomo yao bila vikwazo wakati wa hedhi.
WEL Organization imeeleza kuwa jitihada hizi ni sehemu ya dhamira yake ya kuwawezesha wanawake na wasichana kupitia elimu, uongozi na afya bora, huku ikitoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana katika kusaidia mabinti na watoto wa k**e kufikia ndoto zao na kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya jamii.