26/04/2025
Najisikia furaha sana kuwatumikia hawa watu wakuu, ambao Mungu ameweka hazina zake ndani yao.Ni wito wangu kwa wote (viongozi wa dini, taasisi mbalimbali na serikali) tuwekeze sana katika kuwafundisha na kuwaelekeza kwa usahihi (tukiwalea na kuwasimamia ) watoto na vijana kwa maana ni hazina na msaada kwa kanisa, jamii na Taifa kwa ujumla. Hivyo tunapaswa tuwaelekeze nini wafanye na nini wasifanye kwa mstakabali wa maisha yao.
Mithali 22:6 "Mlee mtoto katika njia impasayo,Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee."
Kumbukumbu la Torati 6:7 "nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo."
Ni hakika, kulijenga Kanisa na Taifa bora inawezekana!
by Enos Shengoyi.
Mwandishi,Mnenaji na Mwanzilishi wa SSA.
Kwa kujifanza zaidi tembelea ukrasa wangu wa Instagram ⬇️ https://www.instagram.com/enos.shengoyi?igsh=ZGUzMzM3NWJiOQ==