LeMachu

LeMachu Kuinua jamii za Kitanzania kupitia afya, elimu na msaada. Jiunge nasi kuleta mabadiliko ya kudumu.

‎Taarifa Rasmi kwa Wanachama wa LeMaChU Wilaya ya Ubungo – Tarehe 18 Julai‎Habari ndugu Wana LeMaChU,‎Napenda kwa heshim...
23/07/2025

‎Taarifa Rasmi kwa Wanachama wa LeMaChU Wilaya ya Ubungo – Tarehe 18 Julai

‎Habari ndugu Wana LeMaChU,
‎Napenda kwa heshima niliyopewa na viongozi wetu kuwaarifu kuwa leo, tarehe 18 Julai, viongozi wetu wamezindua kampeni ya “Amani Yetu na Dkt. Samia”, kampeni inayolenga kuimarisha mshik**ano, utulivu, na uzalendo kwa taifa letu.
‎
‎🌿 Maana ya Amani
‎
‎Amani ni hali ya utulivu, upendo, na maridhiano kati ya watu na jamii kwa ujumla. Ni hali ambayo haina migogoro, vurugu, au hofu. Ni msingi wa maisha bora, maendeleo endelevu, na mafanikio ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
‎
‎🔑 Umuhimu wa Amani
‎
‎Maendeleo: Hakuna maendeleo ya kiuchumi, kielimu, au kijamii bila kuwepo kwa amani.
‎
‎Uhuru wa Mawazo: Amani hutupatia uhuru wa kueleza, kufikiri, na kushiriki katika mambo ya kijamii na kisiasa bila hofu.
‎
‎Maisha Bora: Amani hutoa mazingira bora ya kulea familia, kufanya kazi, na kujenga taifa lenye mshik**ano.
‎
‎Uzalendo: Amani huimarisha moyo wa kizalendo, mshik**ano wa kitaifa, na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kijamii.
‎
‎🕊️ Pongezi na Wito
‎
‎Niwapongeze viongozi wote na wanachama waliohudhuria uzinduzi huu muhimu, na pia kuwashukuru wale ambao kwa changamoto mbalimbali hawakuweza kuhudhuria lakini wana moyo wa kizalendo.
‎
‎Kwa heshima na dhamana ya LeMaChU, nichukue fursa hii kuwaasa wanachama wote tuwe mabalozi wa amani katika jamii zetu. Tuitangaze na kuiishi amani kwa vitendo. Kumbuka:
‎
‎> "Ukikosa amani, hata akili yako haitafikiri vizuri; lakini ukiwa na amani, kila jambo hufanyika kwa usahihi, hekima, na uzalendo."
‎
‎Amani ni msingi wa kila mafanikio – bila amani, hakuna chochote kinachoweza kusonga mbele.
‎
‎Imetolewa na: Balozi
‎Jacob Mndeme
‎Afisa habari na Mahusiano LeMaChU – Wilaya ya Ubungo
‎Tarehe: 18 Julai 2025

‎

MSIMU WA NNE WA JERUSALEM MARATHON WAFANAMhe. Dkt Dorothy Gwajima ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawa...
22/07/2025

MSIMU WA NNE WA JERUSALEM MARATHON WAFANA

Mhe. Dkt Dorothy Gwajima ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amewaongoza maelfu ya wakimbiaji katika msimu wa nne wa Jerusalem Children Home Marathon maeneo ya Kigamboni Kibada Jijini Dar es Salaam.

Kumbuka lengo la mbio hizi ni kusaidia kituo cha kulelea watoto cha Jerusalem na kuwapa tabasamu watoto hao.

‎VIONGOZI WA LeMaChU WASISITIZA AMANI KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI‎‎Imetolewa na Balozi Jacob Mndeme,‎Afisa Habari na Mahu...
21/07/2025

‎VIONGOZI WA LeMaChU WASISITIZA AMANI KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI
‎
‎Imetolewa na Balozi Jacob Mndeme,
‎Afisa Habari na Mahusiano – LeMaChU Wilaya ya Ubungo
‎
‎Katika kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi, viongozi wa Taasisi ya LeMaChU – Leta Mabadiliko Chanya Uraiani wanasisitiza kwa nguvu umuhimu wa kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi.
‎
‎Amani ni msingi wa maendeleo, ni msingi wa haki, na ni nguzo muhimu ya maisha ya kila siku. Bila amani, hata haki ya kuchagua viongozi kwa uhuru na kwa demokrasia inakuwa hatarini. Tunapopiga kura, tunafanya hivyo kwa lengo la kuleta maendeleo na mabadiliko chanya katika jamii zetu – mabadiliko haya hayawezi kufikiwa k**a hatutadumisha hali ya utulivu na mshik**ano.
‎
‎Tunaikumbusha jamii kwamba:
‎
‎Uchaguzi ni tukio la muda mfupi, lakini taifa ni letu milele.
‎
‎Tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa sababu ya chuki wala migawanyiko.
‎
‎Kauli zetu, vitendo vyetu na msimamo wetu unapaswa kujenga, si kubomoa.
‎
‎LeMaChU inaendelea kuelimisha jamii kuhusu njia bora za kushiriki uchaguzi kwa amani:
‎
‎Kushiriki mijadala kwa hoja, si jazba.
‎
‎Kukataa kuchochewa kwa maneno ya uchochezi, ukabila au udini.
‎
‎Kulinda na kuheshimu maamuzi ya wengi kwa njia za kistaarabu.
‎
‎Tunawaalika vijana, wanawake, wazee na viongozi wa dini na kimila kushirikiana na taasisi yetu katika kampeni za kuhimiza amani kwenye mitaa, kata, na wilaya zetu zote.
‎
‎Kauli mbiu yetu ni:
‎Amani ni chaguo, tusikubali kuchochewa – Tanzania ni yetu sote!
‎
‎Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki uchaguzi wa amani.
‎
‎

Address

UBUNGO
Dar Es Salaam
22796

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LeMachu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share