Mustapha HEB Foundation

Mustapha HEB Foundation Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mustapha HEB Foundation, Non-Governmental Organization (NGO), Dar es salaam, Dar es Salaam.

12/11/2025

Ball hall managers , how can you make your Banda umiza so special and unique for the people to enjoy football?.
Dondosha comment yako
Mustapha HEB Foundation
THE POWER OF THE COMMUNITY

07/10/2025

Health matters, your health our riority
WELLCOME for Services
Contact us
0766232427

06/09/2025

Mustapha HEB Foundation ✍️✍️✍️✍️✍️✍️
Committed for empowering them and supporting them

05/09/2025

Among of the main goal of Mustapha HEB Foundation is to save and donate for the poor , especially in rural areas across all regions in Tanzania. Through collaborations with with other institution and the government in enhancing and raising the quality of life for the poor and those in needs as special groups.
Through our commitments and readiness to save , alin collaboration with other stakeholders and other NGO'S, we are inspired to bring hope to the community .
In collaboration with with
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Fedha
Wizara ya Maliasili na Utalii - Tanzania
We are all excited to reach and meet the community through diferent ways and see how we can afford and meets our planned goals
You are all welcome , for any commitment
Communicate with us
Manager: 0766232427

05/09/2025

Am so grateful for how people inspired with the project with their commitment . This is the main collaborator in Mental health and parenting styles. The head of department at university . And the Mental Health specialist at Muhimbili National Hospital , Dr. Sofia Sanga
In collaboration with Mustapha HEB Foundation . We are aimed to meet the communities in raising awareness educating and empowering the communities in Mental health , parenting styles and the effect of drugs abuse in relation to mental health.
WELLCOME for our continuous updates
Meetings
Seminars
Books and articles are all ready prepared
Sponsorship from
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Are all on progress to meet our targeted goals.
Communicate us
Manager : 0766232427

05/09/2025

Am so grateful for how people inspired with the project with their commitment . This is the main collaborator in Mental health and parenting styles. The head of department at Muhimbili University of Health and Allied Sciences . And the Mental Health specialist at Muhimbili National Hospital , Dr. Sofia Sanga
In collaboration with Mustapha HEB Foundation . We are aimed to meet the communities in raising awareness educating and empowering the communities in Mental health , parenting styles and the effect of drugs abuse in relation to mental health.
WELLCOME for our continuous updates
Meetings
Seminars
Books and articles are all ready prepared
Sponsorship from
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Are all on progress to meet our targeted goals.
Communicate us
Manager : 0766232427

FAIDA KUU ZA TAASISI HIIMUSTAPHA HEB FOUNDATION , itakuwa na faida kuu zifuatazo katika taifa letu pamoja na inchi zingi...
05/09/2025

FAIDA KUU ZA TAASISI HII
MUSTAPHA HEB FOUNDATION , itakuwa na faida kuu zifuatazo katika taifa letu pamoja na inchi zingine za afrika mashariki na kati kwa ujumla. Kwa kushirikiana na serikali katika kufanikisha malengo ya taasisi hii itakuwa na faida kubwa sana katika maendeleo ya inchi yetu k**a ilivyoainishwa hapa chini

1. Kulinda afya ya jamii na kupanua uelewa wa kila mtu katika jamii juu ya namna bora ya kujikinga na magonjwa.

2. Itapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto kwa 5% kila mwaka kupitia elimu juu ya afya ya uzazi.

3. Kupunguza vifo visivyo vya lazima kutokana na magonjwa.

4. Kujenga jamii zenye afya kote inchini kwa kupanua uelewa kwa wahusika hasa katika magonjwa ya kuambukiza,

5. Kuongeza ufaulu wa wanafunzi mashuleni kwa ongezeko la 5% kia mwaka hasa katika shule za kata.

6. Kuongeza mwamko wa elimu katika jamii hasa maeneo ya vijijini

7. Kupunguza tatizo la ajira inchini kwa vijana kwa 0.5% kila mwaka

8. Kupunguza vijana wa mitaani wasiokuwa na mambo ya kufanya, na hivo kupunguza vijana wezi, vibaka, majambazi pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya kwa kuwawezesha vijana hawa kujihusisha katika shughuli za uzalishaji.

MALENGO YA TAASISIMUSTAPHA HEB FOUNDATION  imejikita katika kufanikisha malengo yafuatayo1. Kuelimisha jamii juu ya afya...
05/09/2025

MALENGO YA TAASISI
MUSTAPHA HEB FOUNDATION imejikita katika kufanikisha malengo yafuatayo
1. Kuelimisha jamii juu ya afya na namna bora ya kujikinga na magonjwa mbalimbali

2. Kuelimisha jamii juu ya madhara ya madawa ya kulevya na kuwainua vijana kwa kuepuka makundi ya mitaani ili waweze kujihusisha katika shuguli za uzalishaji

3. Kuelimisha jamii juu ya malezi bora katika jamii pamoja na afya ya akili ya jamii

4. Kutoa misaada ya kiafya ikiwemo vyandarua, sabuni, dawa za kuua wadudu na usafi wa vyoo, vitakasa mikono pamoja na mahitaji mengine hasa katika familia masikini zilizopo vijijini na makundi mengine yenye uhitaji.

5. Kutoa elimu na semina mbalimbali juu ya afya ya uzazi katika jamii, umuhimu wa njia za kisasa za uzazi wa mpango, mama wajawazito na watoto ikiambatana na uuzaji wa nakala za vitabu maalumu vilivyoandaliwa na taasisi .

6. Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wao, kuongeza mwamuko wa elimu katika jamii, kutoa elimu kwa wazazi juu ya namna bora ya kuwawezesha vijana ili waweze kutimiza ndoto zao kupitia elimu, elimu hii itaambatana na uuzaji na usambazaji wa vitabu maalumu vilivyoandaliwa na taasisi

7. Kuwaelimisha wanafunzi mashuleni kupitia semina mbalimbali juu ya namna bora za usomaji,mbinu za usomaji,mbinu za ujibuji mitihani, mbinu za ujibuji wa maswali katika kila somo, na mbinu za kufaulu kila somo sekondari kwa kuwapa miongozo mbalimbali iliyoainishwa katika vitabu maalumu vilivyoandaliwa na taasisi na kisha kuwauzia nakala hizo.

8. Kuwawezesha baadhi ya wanafunzi wanaotokea katika familia masikini na mazingira magumu kwa kuwapatia baadhi ya mahitaji k**a vile sare za shule, daftari, vitabu pamoja na kuwalipia baadhi ya michango ya shule ikiwemo ada ili waweze kutimiza malengo yao kupitia elimu

9. Kugawa taa za kusomea kwa wanafunzi walioko vijijini katika shule za kata ambako hata umeme haupo majumbani,, wanafunzi wanaoishi katika familia masikini, kuwapatia baiskeli baadhi ya wanafunzi wanaotembea umbali mrefu ili kufika shuleni na kurudi nyumbani hasa katika shule za kata zilizopo vijijini na watoto kutoka katika familia masikini katika mikoa yote Tanzania

10. Kuanzisha vituo vya tution vikiwa vimelenga kuwawezesha vijana kujifunza katika kipindi chga mda wa ziada na likizo ili waweze kuwa wabobezi katika masomo yao na kuwafanya wafaulu vizuri

11. Kujenga mabweni au hostel karbu na shule hasa shule za kata ili kuwawezesha wanafunzi kukaa karbu na shule na kuwa bize na kusoma mda wote kwa kuwaepusha kutembea umbali mrefu na changamoto zingine za mazingira ya nyumbani zinazowafanya washindwe kupata mda wa kujisomea. Hosteli hizi wanafunzi watalipia kwa garama nafuu ili kuwawezesha wanafunzi wa aina zote kuwa karbu na mazingira ya shule.

12. Kusambaza vitabu, reviews, past papers na material mbalimbali yatakayowasaidia vijana katika kufaulu mitihani yao na kusonga mbele, taasisi itawaunganisha shule zote Tanzania kwa kusambaza material fanani hasa kutoka katika shule kubwakubwa inchini ambazo zinaongoza kwa kufaulisha wanafunzi, material hayo na mitihani yote wataipata hata wale walopo vijijini katika shule za kata ili waweze kupata miongozo na namna bora ya usomaji ili kuendena na mitihani husika.

13. Kuwafikia wanafunzi mashuleni na kuwapa semina mbalimbali katika kuwawezesha na kuwainua hata wale waliokata tamaa waweze kuinuka. Semia hizi zitendeshwa kidarasa kulingana na uhitaji wa darasa husika.

14. Kuanzisha vituo na shule za awali (chekechea) katika maeneo yote ya vijijini inchi nzima ambako mwamko wa elimu ni kidogo ili kuwajengea watoto msingi wa kupenda shule.

15. Kuanzisha vituo maalumu vya kulea vipaji kwa vijana ikiwemo mpira wa miguu pamoja na mziki au filamu za uigizaji/comedy

16. Kuanzisha miradi mbalimbali ya kibiashara ili kuajiri vijana zaidi ya 200 kila mwaka k**a ilivo ainishwa kwenye muhtasari wa taasisi hapo juu

17. Kuanzisha mafunzo mbalimbali kwa vitendo ili kuwawezesha vijana kujiajiri vikiwemo, ufundi, viwanda vidogovidogo k**a utengenezaji wa sabuni, kilimo cha bustani, ufugaji pamoja na miradi mingine.

18. Kutoa misaada kwa wenye uhitaji k**a vile familia masikini,, wazee, yatima na walemavu
Kutoa elimu kwa vijana wa mitaani ili waweze kujihusisha katika shughuli za uzalishaji na kuepuka wizi, ukabaji na ujambazi,elimu hii itatolew kupitia semina, mikutano , vipeperushi pamoja na vyombo vingine vya habari.

MUSTAPHA HEB FOUNDATION                             Ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na mmiliki wake MUSTAPH...
05/09/2025

MUSTAPHA HEB FOUNDATION
Ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na mmiliki wake MUSTAPHA MISUNGWI JIMONDOGWE mnamo mwaka 2025 ikiwa na dhumuni la kuwainua vijana kupitia idara ya afya, elimu na ujasiliamali(biashara)

Taasisi hii inalenga zaidi katika kuwainua vijana hasa wale wanaotokea katika mazingira magumu na familia za kimasikini, aidha taasisi hii imedhamilia katika kurudisha matumaini hasa kwa vijana waliokata tamaa pamoja na kuongeza mwamko wa elimu katika jamii

Taasisi hii imeainisha wazi kwa kujikita katika misingi ya Elimu, Afya Pmoja na Ujasiliamali au biashara ambayo ndiyo misingi mikuu na mzizi mkuu wa maisha ya mwanadamu katika kuelekea kujikwamua kimaisha.

Taasisi hii inatambua uwepo wa changamoto nyingi kwa vijana walio wengi mitaani katika soko la ajira. MUSTAPHA HEB FOUNDATION imejikita pia katika utoaji wa ajira ndogondogo katika biashara ili kupunguza tatizo la ajira inchini paoja na inchi zingine za afrika mashariki na kati

Taasisi hii imebeba matumaini pia kwa watu wenye uhitaji kupitia makundi mbalimbali wakiwemo yatima, wasiojiweza, wazee, walemavu, familia masikini pamoja na wajane

Taasisi hii imelenga pia katika kuelimisha jamii juu ya afya ya jamii kupitia mikutano, semina mbalimbali,pamoja na usambazaji wa nakala za vitabu mbalimbalivinavyotoa elimu juu ya afya katika kulinda afya ya jamii ikiwemo elimu juu ya uelewa wa magonjwa na visababishi vyake, njia bora za kujikinga na magonjwa, madhara ya madawa ya kulevya, malezi bora katika jamii, afya ya uzazi,ulaji ufaao afya, pamoja na kubadili mitindo ya maisha ili kulinda afya zao kimwili, kiakili/kisaikolojia pamoja na kiroho

Aidha taasisi hii imelenga kuwawezesha vijana hasa wanaotoka katika mazingira magumu kwa kuwasomesha na kuwapatia mahitaji yao ili kuwasaidia kutimiza malengo yao kupitia elimu.

Kwa kushirikiana na serikali kupitia sekta ya Elimu, taasisi hii imelenga kuandaa vitabu maalumu katika kuwawezesha wanafunzi mashuleni kujitambua, kujua mbinu sahihi za usomaji, mbinu za ujibuji mitihani,, namna sahihi na jinsi ya kufaulu masomo yote ya sekondari, mbinu za kuwa mwanafunzi bora shuleni. Na miongozo yote ya usomaji na namna ya ujibuji wa maswali katika somo husika.

Aidha katika kulitekeleza hili, taasisi hii itatoa semina kwa wanafunzi katika mashule kwa kuwaelimisha na kuwafundisha juu ya umuhimu wa elimu na kisha kuwapatia vitabu vya miongozo yote, hasa katika shule za kata na shule zote zilizopo vijijini ambako mwamuko wa elimu bado ni kidogo.

Taasisi hii pia imelenga katika kuandaa miradi mbalimbali ya kibiashara itakayowezesha kupunguza tatizo la ajira inchini kwa kuajiri vijana zaidi ya 200 kila mwaka kupitia biashara na miradi mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji,bustani, ufundi pamoja na mengineyo

Taasisi hii imelenga kufungua na kuanzisha miradi mbalimbali ya kibiashara katika kuajiri vijana ikiwemo maduka, stationary, studio/library, kumbi za mpira na mikutano, maduka ya madawa, vituo vya kuchoma chipsi, kumbi za starehe k**a vile baa, hoteli, migahahawa na cafeteria, vituo vya kutengeneza juice za matunda na juice ya muwa, nyama choma, maduka ya vinywaji, maduka ya nafaka na bidhaa za sokoni, maduka ya aina zote, ufundi seremala, ufundi cherehani, saloon za k**e, maduka ya vitabu na maktaba ya kisasa pamoja na computer lab, mitambo ya bustani za mbogamboga na matunda pamoja na mazao mengine, ufugaji wa ng”ombe wa kisasa wa maziwa, kuku wa mayai pamoja na viwanda vingine vidogovidogo vya kuteneneza sabuni na kufuga samaki.

WELLCOME Mustapha HEB Foundation
SUPPORT YAKO NDIYO MAFANIKIO YA TAASISI HII
Mawasiliano
Manager: 0766232427

03/08/2025

Karbuni Sana wadau wa ELIMU Tanzania katika mwendelezo wa masomo haya ili kuwawezeaha vijana wetu walioko mashuleni kufaulu vizuri mitihani Yao na kutimiza ndoto zao.
Kwa maelekezo zaidi nitafute kwa simu number 0766232427. Educational inspirational and awareness for BIG RESULTS NOW✍️

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mustapha HEB Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share