Women and Youth Care Organization

Women and Youth Care Organization Empowering women and youth through education, economic opportunities, gender equality advocacy, support for GBV survivors, and environmental conservation

19/05/2026

Tusikubali watoto kuingizwa kwenye biashara ya ngono, kutumikishwa au kunyanyaswa kwa kisingizio chochote. Kila mtoto ana haki ya kuishi salama, kupata elimu, upendo na malezi bora yanayomlinda dhidi ya ukatili wa aina yoyote. Jamii inapokaa kimya, watoto wengi huendelea kuumizwa na kupoteza ndoto zao. Tuungane kupaza sauti, kutoa taarifa na kusimama imara dhidi ya unyonyaji, ukatili wa kijinsia na matumizi mabaya ya watoto, kwa sababu watoto ni taifa la kesho na wanastahili kulindwa leo.”

— Dr Florah Msuya
CEO, WAYCO Organisation

‎Meet with our friends from England Emma and Charlotte development partners of WAYCO.Great discussion on social economy ...
18/05/2026

‎Meet with our friends from England Emma and Charlotte development partners of WAYCO.
Great discussion on social economy and community development.

15/05/2026

‎Tusisubiri kuwa na uwezo mkubwa ndipo tushiriki kuwainua wengine. Kila mtoto anayepata elimu leo hujengwa kuwa kijana mwenye maadili, maono na mchango chanya kwa jamii ya kesho.” ❤️

“Uwekezaji kwa watoto na vijana si hisani pekee, bali ni ujenzi wa rasilimali watu na mustakabali wa taifa. Uharakati wa kweli ni kusimamia haki yao ya kupata elimu, malezi bora na fursa sawa za kuendelea kielimu.”

“Na hakuna zawadi kubwa k**a kuona tabasamu la mtoto anayehisi kuthaminiwa, kusikilizwa na kupewa matumaini ya maisha bora. Tabasamu lao ni ishara kuwa bado tuna nafasi ya kuibadilisha dunia kupitia upendo, elimu na mshik**ano.”

Katika ziara ya kijamii iliyofanywa na WAYCO Organization katika visiwa vya Wilaya ya Nansio, Ukerewe mkoani Mwanza, Mkurugenzi wa WAYCO, Dr. Florah Msuya, alitembelea maeneo ya visiwani humo na kukutana na mtoto aitwaye Joseph, mwenye umri wa miaka 9, anayesoma darasa la pili.

Joseph anaishi na babu na bibi yake katika mazingira ya visiwani yenye changamoto za kijamii na kiuchumi. Babu yake ni mlemavu, hali inayofanya familia hiyo kuwa katika hali ngumu zaidi ya maisha, ikiwa na changamoto za kupata mahitaji ya msingi k**a elimu, chakula na huduma za afya.

Pamoja na mazingira hayo, Joseph anaendelea kuonyesha bidii na matumaini makubwa katika masomo yake, jambo lililogusa sana moyo wa timu ya WAYCO Organization.

Ziara hiyo ililenga kuona hali halisi ya maisha ya watoto wanaoishi visiwani, na kuhamasisha jamii na wadau mbalimbali kushirikiana kuwasaidia watoto k**a Joseph ili wasikose haki yao ya elimu na malezi bora.

Kisa cha Joseph kinatukumbusha kuwa hata katika maeneo ya visiwani, kuna watoto wenye ndoto kubwa wanaohitaji mikono ya upendo kuwainua.






Happy Mother’s Day to all the incredible mothers around the world. 💐Today we celebrate your unconditional love, strength...
10/05/2026

Happy Mother’s Day to all the incredible mothers around the world. 💐
Today we celebrate your unconditional love, strength, sacrifices, and endless care.
Thank you for being the heart of our families and the light in our communities.

Your kindness, patience, and courage inspire us every day.
May this special day bring you joy, peace, love, and all the happiness you truly deserve. ❤️

Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kutoka WAYCO Organization. Tunawashukuru kwa bidii na kujituma kwenu. Tuendelee kuwa...
01/05/2026

Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kutoka WAYCO Organization. Tunawashukuru kwa bidii na kujituma kwenu. Tuendelee kuwawezesha wanawake na vijana kwa kesho iliyo bora zaidi.

✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽 ゚viralシfypシ゚viralシalシ
01/04/2026

✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽
゚viralシfypシ゚viralシalシ

30/03/2026

Kitaa kwa Kitaa — Kuzungumza na Vijana Kuhusu Kujitambua na Thamani Yao

Tunaenda kitaa kwa kitaa kuhamasisha vijana kujitambua, kugundua uwezo wao, na kuelewa thamani waliyonayo katika jamii.

Lengo letu ni kuwasaidia vijana:
• Kujitambua na kujiamini
• Kutambua vipaji na uwezo wao
• Kufanya maamuzi sahihi ya maisha
• Kujenga maadili na malengo yenye mwelekeo
• Kuamini kuwa wanaweza kubadilisha maisha yao na jamii inayowazunguka

Kijana anayejitambua thamani yake hubadilisha maisha yake — na hatimaye hubadilisha dunia inayomzunguka.

— Florah Msuya
CEO, WAYCO Organisation
Empowering Women and Youth for a Brighter Tomorrow

Anajua kusema hapana pale ambako anaona panaelekea kuharibu kesho yake.Huchagua maendeleo kuliko starehe za muda mfupi.H...
30/03/2026

Anajua kusema hapana pale ambako anaona panaelekea kuharibu kesho yake.
Huchagua maendeleo kuliko starehe za muda mfupi.
Huamini kuwa mafanikio huanza na nidhamu binafsi.
Hujenga maisha yake hatua kwa hatua bila kukata tamaa.

Florah Msuya
CEO, WAYCO Organisation

✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽
29/03/2026

✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽

21/03/2026
Kwa niaba ya Wayco Women and Youth Care Organization  tunatoa salam za pongezi na heshima kwa wanawake wote  Duniani  si...
08/03/2026

Kwa niaba ya Wayco
Women and Youth Care Organization tunatoa salam za pongezi na heshima kwa wanawake wote Duniani siku hii muhimu ni ya kutambua nguvu ,ujasiri na mchango mkubwa wa wanawake katika familia,jamii na maendeleo ya jamii inayomzunguka.

Kupitia juhudi zetu katika kuwawezesha Wanawake na vijana tunaendelea kujenga kizazi chenye matumaini ,uwezo na ndoto kubwa kwa ajili ya kesho iliyo bora .
Happy international women's day.

Address

Kibamba
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Women and Youth Care Organization posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share