31/07/2026
Kwa Shamila, na kwa kila Askari Wanyamapori kote nchini Tanzania: asanteni sana🙏.
Mnalinda zaidi ya wanyamapori pekee. Mnalinda riziki za wanajamii, mandhari asilia, na urithi wa vizazi vijavyo. Uhifadhi endelevu hauwezi kusimamiwa kutokea mbali. Shamila anafanya doria kwenye ardhi ambayo familia yake imeishi kwa vizazi vingi, anawajua majirani zake, na wao pia wanamjua.
Taarifa zinamfikia kabla tatizo halijawa kubwa, kwa sababu jamii inamuamini na kumpa ushirikiano. Hiyo ndiyo nguvu ya mfumo wa WMA (Hifadhi za Jamii): si tu kulinda wanyamapori, bali pia kuhakikisha jamii inanufaika na matumizi endelevu ya maliasili zao.
Bonyeza link hii kuitazama filamu yake au itazame kupitia kituo cha runinga cha Tanzania Safari Channel.
https://youtu.be/ZR2HwOx3MPw?si=RGZ_KYrkavRGGVQr
Uhifadhi ni wajibu wa kila mmoja wetu. Kuwa mhifadhi.