12/06/2026
UKAGUZI WA ASUBUHI WA KAMBI YA MASHINDANO – GOBA SEKONDARI
Asubuhi ya leo, Watahini wa Kambi ya Mashindano walifanya ukaguzi maalum kwa kutembelea vikosi mbalimbali vilivyoweka kambi katika Shule ya Sekondari Goba. Ukaguzi huo ulilenga kutathmini utekelezaji wa stadi za Skauti, usafi wa kambi, ubora wa miundo ya kambini, nidhamu, mpangilio wa vifaa pamoja na uwezo wa Skauti kuishi kwa kuzingatia misingi ya Scouting.
Katika zoezi hilo, kila kikosi kilipata nafasi ya kuwasilisha kazi na ubunifu wake mbele ya Watahini huku kikionyesha umahiri katika matumizi ya kamba, ujenzi wa miundo ya kambini, uhifadhi wa mazingira na uendeshaji wa shughuli za kila siku kambini.
Ukaguzi wa asubuhi ni sehemu muhimu ya mashindano kwani huwapa Skauti fursa ya kupimwa maarifa yao kwa vitendo na kujifunza maeneo yanayohitaji kuboreshwa. Aidha, hujenga moyo wa uwajibikaji, umoja, uongozi na ushindani wenye afya kati ya vikosi vinavyoshiriki.
Hongereni kwa vikosi vyote vinavyoendelea kuonyesha ari, nidhamu na kujituma katika shughuli za kambi. Endeleeni kuzingatia Ahadi na Sheria za Skauti huku mkionesha mfano bora wa vijana wenye maadili na uzalendo.
📍 Goba Sekondari
📅 12 Juni 2026