The Bilal Tz

The Bilal Tz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from The Bilal Tz, Charitable organisation, Libya Street, Plot no. 2239/208 Block 233, Dar es Salaam.

Siku ya Kuzaliwa Mtume (S.A.W.W) Lazima IkumbukweJifunze ukweli na umuhimu wa kuadhimisha mazazi ya Bwana wa Viumbe (S.A...
02/09/2026

Siku ya Kuzaliwa Mtume (S.A.W.W) Lazima Ikumbukwe

Jifunze ukweli na umuhimu wa kuadhimisha mazazi ya Bwana wa Viumbe (S.A.W.W). Kitabu hiki kinatoa majibu na ufafanuzi wa kina kuhusu adhimisho hili muhimu.

Jipatie nakala yako sasa!

Fika kwenye Maktaba yetu iliyopo;
Mnazi Mmoja - Mtaa wa Libya (Karibu na Mwendokasi Kisutu)
Dar es Salaam - Tanzania
Kwa Mawasiliano:
0745 111 150
0678 888 795

Kituo cha Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) Ikwiriri Mjini kilifanikiwa kuandaa na kuendesha Majlisi tukufu ya kua...
01/09/2026

Kituo cha Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) Ikwiriri Mjini kilifanikiwa kuandaa na kuendesha Majlisi tukufu ya kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya kiongozi wa umma, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Majlisi hii iliyowaleta pamoja waumini na wanafunzi kutoka madrasa mbalimbali, ilijikita katika kuangazia fadhila, athari, na ubora wa kuzaliwa kwa Mtume Rehema na Amani zishuke juu yake na Aliy zake.

Kituo cha Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) Kilwa Kivinje kimefanikiwa kuendesha  maadhimisho makubwa ya Maulid ya...
31/08/2026

Kituo cha Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) Kilwa Kivinje kimefanikiwa kuendesha maadhimisho makubwa ya Maulid ya Mtume Mtukufu, Muhammad (s.a.w.w).

Mkusanyiko huu wa kiibada umekua ni fursa nyingine adhimu ya kudhihirisha ushahidi na athari ya mapenzi yetu ya dhati kwa Mtume na Ahlu-Bayt (a.s) kupitia visomo, mawaidha, na kauli thabiti za kiislamu. Shukrani za dhati kwa kila aliyeshiriki na kufanikisha.

31/08/2026

yaa Rasullah

Matawi ya Bilal Muslim Mission ya Ngarenairobi, Matadi na Muangaza, yakiongozwa na Tawi Kuu la Moshi, yamejumuika pamoja...
31/08/2026

Matawi ya Bilal Muslim Mission ya Ngarenairobi, Matadi na Muangaza, yakiongozwa na Tawi Kuu la Moshi, yamejumuika pamoja katika maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) yaliyofanyika katika Kijiji cha Ngarenairobi, kwenye Madrasa ya Kibosho.

Waumini na wananchi walipata fursa ya kusikiliza mawaidha kutoka kwa mzungumzaji mahiri, Samahat Sheikh Miraji Kiago, kutoka makao makuu ya taasisi hiyo mkoani Kilimanjaro. Sheikh Kiago alisisitiza umuhimu wa kufuata nyayo na maadili mema ya Mtume (s.a.w.w) katika kujenga jamii yenye amani na misingi imara ya kidini.

31/08/2026
Mnamo tarehe 30 Agosti 2026, ikisadifiana na tarehe 17 Rabiul Awwal 1448H, waumini na wanafunzi wa Bilal Muslim Mission ...
31/08/2026

Mnamo tarehe 30 Agosti 2026, ikisadifiana na tarehe 17 Rabiul Awwal 1448H, waumini na wanafunzi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) tawi la Kilidu walijumuika kwa pamoja katika kuadhimisha mazazi ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Maadhimisho haya muhimu yalipambwa na mahudhurio ya viongozi mashuhuri wa kidini walioshiriki kutoa miongozo, dua, na hotuba za kiroho, akiwemo Alhaj Sheikh Abillah na Sheikh Yusuf kutoka BMMT Newala, pamoja na Sheikh Abdurazaki kutoka BMMT Chitenda na Sheikh Juma kutoka BMMT Kilidu. Waumini walipata fursa ya kusikiliza mawaidha yenye kujenga, visomo vya Quran Tukufu, pamoja na kaswida safi zilizowasilishwa na wanafunzi wa Kilidu.

Uongozi unatoa shukrani za dhati kwa kila aliyefanikisha majlisi hii kwa hali na mali. Mwenyezi Mungu awalipe sote kwa mapenzi yetu kwa Mtume (s.a.w.w).

Kutoka wilayani Mafia, Mkoa wa Pwani, Bilal Muslim Mission of Tanzania imefanya maadhimisho ya Wilada (Kuzaliwa) kwa Mtu...
31/08/2026

Kutoka wilayani Mafia, Mkoa wa Pwani, Bilal Muslim Mission of Tanzania imefanya maadhimisho ya Wilada (Kuzaliwa) kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu, Muhammad (s.a.w.w).

Nyoyo za waumini zimejaa furaha, upendo na amani tukikumbuka na kuhuisha mafundisho ya amani na huruma aliyokuja nayo Mtume kwa walimwengu wote.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania, Mr. Hafidh Mansor, amehudhuria sherehe za Mazazi ya Mtukuf...
31/08/2026

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania, Mr. Hafidh Mansor, amehudhuria sherehe za Mazazi ya Mtukufu wa Darja Mtume wetu Muhammad s.a.w.w Katika viwanja vya pipo uliopo Mitaa ya Kigogo Dar es Salaam.

Maulidi hayo imeandaliwa na Jumuiya ya Shia Ithnaashariyyah Tanzania TIC, imehudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa kidini na kisiasa wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi, Ajira na Mahusiano) Mhe. Deusi Clement Sangu Akimuwakilisha Mgeni Rasmi Mhe. DKT. Mwigulu Lameck Nchemba.

https://youtu.be/7_MRmPYt1zQ  Like, Comment and Share
29/08/2026

https://youtu.be/7_MRmPYt1zQ

Like, Comment and Share

Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

Address

Libya Street, Plot No. 2239/208 Block 233
Dar Es Salaam
11104

Opening Hours

Monday 08:30 - 17:30
Tuesday 08:30 - 17:30
Wednesday 08:30 - 17:30
Thursday 08:30 - 17:30
Friday 08:30 - 17:30
Saturday 08:30 - 13:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Bilal Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share