SHIVYAWATA

SHIVYAWATA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from SHIVYAWATA, Nonprofit Organization, Dar es Salaam.

SHIVYAWATA is a non-governmental federation that brings together twelve national organizations advocating for the rights and inclusion of people with disabilities.

Michezo jumuishi si burudani tu—ni msingi wa kujifunza, kushirikiana, na kukuza uwezo wa kila mtoto 🧩🤝Kupitia Elimu ya A...
23/04/2026

Michezo jumuishi si burudani tu—ni msingi wa kujifunza, kushirikiana, na kukuza uwezo wa kila mtoto 🧩🤝

Kupitia Elimu ya Awali ya Watoto (ECE), watoto hujenga stadi za kijamii, ubunifu, na kujiamini. Lakini tukihamia kwenye IPECE (Inclusive Play-based Early Childhood Education), tunahakikisha kila mtoto—wakiwemo wenye ulemavu—anashiriki kikamilifu bila kubaguliwa 🌍

Huu ndio wakati wa kuchukua hatua:
TUTOKE ECE, TWENDE IPECE ili kufikia SDG 4.2—elimu bora na jumuishi kwa watoto wote 🎯

.2

Leo SHIVYAWATA tunashiriki katika GAWE 2026 kuanzia tarehe 20 hadi 24 Aprili 2026 🎉Tunaungana kuendeleza kauli mbiu: Mic...
20/04/2026

Leo SHIVYAWATA tunashiriki katika GAWE 2026 kuanzia tarehe 20 hadi 24 Aprili 2026 🎉
Tunaungana kuendeleza kauli mbiu: Michezo jumuishi kwa kila mtoto — kutoka ECE ya kawaida kwenda IPECE kwa SDG 4.2.
Tunaamini kila mtoto ana haki ya kushiriki, kujifunza, na kufurahia michezo bila kizuizi 🤝
.2

SHIVYAWATA tunatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na Serikali kufuatia kifo cha aliyekuwa Waz...
27/03/2026

SHIVYAWATA tunatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na Serikali kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. William Lukuvi.

Tunatambua na kuthamini mchango wake mkubwa katika kutetea, kuimarisha na kusimamia masuala ya watu wenye ulemavu nchini. Uongozi wake utaendelea kukumbukwa na kuenziwa daima.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

SHIVYAWATA inawatakia Heri ya Mwaka Mpya 2026. Tuuanze mwaka huu kwa mshikamano, usawa na kupigania haki na fursa sawa k...
01/01/2026

SHIVYAWATA inawatakia Heri ya Mwaka Mpya 2026. Tuuanze mwaka huu kwa mshikamano, usawa na kupigania haki na fursa sawa kwa watu wote wenye ulemavu.

Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2026! 🎄✨Tuendelee kusherehekea upendo, amani na mshikamano huku tukijenga jamii jumuishi ...
24/12/2025

Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2026! 🎄✨
Tuendelee kusherehekea upendo, amani na mshikamano huku tukijenga jamii jumuishi inayothamini utu wa wote, hususan watu wenye ulemavu.

Leo 9 Disemba tunasherekea miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania tukikumbuka thamani ya umoja, usawa na ujumuishi. Uhuru ni wa k...
09/12/2025

Leo 9 Disemba tunasherekea miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania tukikumbuka thamani ya umoja, usawa na ujumuishi. Uhuru ni wa kila Mtanzania, na tunatambua mchango muhimu wa watu wenye ulemavu katika kujenga taifa lenye maendeleo na haki kwa wote.

Disemba 4-5, 2025 mkoani Morogoro kumefanyika Mapitio ya Mkakati wa Utetezi wa Haki kwa Watu Wenye Ulemavu (2026-2030), ...
06/12/2025

Disemba 4-5, 2025 mkoani Morogoro kumefanyika Mapitio ya Mkakati wa Utetezi wa Haki kwa Watu Wenye Ulemavu (2026-2030), washiriki toka Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu (OWM - KVAU), OWM - TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, Asasi za Kiraia.

Mapitio haya ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya "Wezesha Mtoto 2025-2027" unaofadhiliwa na Lillian Fond kupitia wadau wa SHIVYAWATA, Beyond Inclusion Tanzania (BIT).

Leo, tarehe 3 Desemba 2025, tumesherehekea Siku ya Kitaifa ya Watu Wenye Ulemavu hapa Morogoro, Tanzania. Tukio hili lim...
03/12/2025

Leo, tarehe 3 Desemba 2025, tumesherehekea Siku ya Kitaifa ya Watu Wenye Ulemavu hapa Morogoro, Tanzania. Tukio hili limehudhuriwa na Watu Wenye Ulemavu, wadau mbalimbali pamoja na Mgeni Rasmi, Mhe. Adam Kighoma Malima – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Kuendeleza Jamii Jumuishi kwa Watu Wenye Ulemavu kwa Mustakabali na Ustawi wa Jamii.”

Muonekano wa baadhi ya matukio yenye ushindi, elimu na ushirikiano kwenye Kongamano la Watu Wenye Ulemavu, Morogoro – 2 ...
02/12/2025

Muonekano wa baadhi ya matukio yenye ushindi, elimu na ushirikiano kwenye Kongamano la Watu Wenye Ulemavu, Morogoro – 2 Desemba 2025.
Safari ya kujenga jamii jumuishi inaendelea!

Katika kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu mwaka 2025 leo 2 Disemba, 2025 tutakuwa na kongamano la watu wenye ulemavu...
02/12/2025

Katika kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu mwaka 2025 leo 2 Disemba, 2025 tutakuwa na kongamano la watu wenye ulemavu litakalofanyika mkoani Morogoro katika Chuo Cha Waislamu Morogoro (MUM).

Huu ni wakati wa kujifunza, kushirikiana na kuchochea mabadiliko chanya kwa mustakabali jumuishi.
Hebu tuwe sauti ya mabadiliko! ✨

Jiunge nasi kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu (IDPD)  - 2025.Tukio la mwaka huu litafanyika Kitaifa Mk...
25/11/2025

Jiunge nasi kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu (IDPD) - 2025.
Tukio la mwaka huu litafanyika Kitaifa Mkoani Morogoro, Disemba 2–3, 2025, likiwa na dhamira ya kukuza uongozi wa Watu Wenye Ulemavu kwa ajili ya jamii jumuishi na endelevu.

Karibu ushuhudie, ujifunze na uchangie kwenye safari ya kujenga Tanzania isiyomuacha mtu nyuma.

SHIVYAWATA invites qualified audit firms to conduct the 2025 annual audit for programs funded by KBTA, BRAC Maendeleo, B...
24/11/2025

SHIVYAWATA invites qualified audit firms to conduct the 2025 annual audit for programs funded by KBTA, BRAC Maendeleo, BIT, Government Ruzuku, FFO and MyRight.
The audit will assess proper use of funds, compliance, internal controls and provide recommendations for improvement.

Qualified IFAC-recognized auditors with experience in multi-donor projects are encouraged to apply by 25 Nov 2025 via [email protected]
or submit physically at SHIVYAWATA offices (Samora/Luthuli St., Dar es Salaam).

For more information please visit our website at www.shivyawata.or.tz

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SHIVYAWATA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to SHIVYAWATA:

Share