UNICEF TANZANIA

UNICEF TANZANIA This is the Official Page of UNICEF Tanzania. UNICEF has been working in Tanzania since 1954 advocating for the rights of children. www.unicef.org/tanzania

UNICEF has been on the ground in Tanzania since 1954 as part of its emergency operations, though the office was set up in 1975. Since then, UNICEF’s assistance to Tanzania has taken many forms guided by the changing situation of women and children in Tanzania, national and organization priorities. UNICEF plays a unique role in Tanzania as an advocate for children’s rights, identifying gaps in thei

r realization, providing technical advice and assistance to the government in addressing the gaps, and bringing evidence to the table.

Kuelekea hatua inayofuata ya First Foods Africa: Mwongozo wa kimkakati na hatua za kipaumbele.Wiki hii, Wizara ya Viwand...
13/08/2026

Kuelekea hatua inayofuata ya First Foods Africa: Mwongozo wa kimkakati na hatua za kipaumbele.

Wiki hii, Wizara ya Viwanda Biashara , kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Tanzania na UNICEF, iliitisha Kamati ya Ushauri ya Kiufundi ya First Foods Africa (FFA), iliyowakutanisha taasisi za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wasomi, washirika wa maendeleo na wataalamu wa kiufundi.

Mkutano huo ulilenga kuimarisha hatua za pamoja za kuboresha lishe ya watoto wadogo, ikiwemo kuongeza upatikanaji wa vyakula vya kwanza vyenye lishe, salama na vya bei nafuu; kuimarisha sera wezeshi; na kuchochea mahitaji ya lishe bora.
Kupitia First Foods Africa, wadau wanaendelea kushirikiana kuhakikisha kila mtoto mdogo anapata vyakula vya kwanza vyenye lishe anavyohitaji ili kukua na kuendelea vizuri.

Matarajio ya maisha bora huanza na fursa sawa.Katika  , kupitia mpango wa Every Adolescent Girl Learns (EAGL), Canada’s ...
12/08/2026

Matarajio ya maisha bora huanza na fursa sawa.

Katika , kupitia mpango wa Every Adolescent Girl Learns (EAGL), Canada’s International Development – Global Affairs Canada na UNICEF TANZANIA wanawezesha vijana balehe kwa kuwapatia ujuzi na fursa wanazohitaji ili kufanikiwa shuleni, kazini na maishani.

Ni rahisi k**a 1, 2, 3... 4. ✨Kuanzia usajili hadi kuingiza taarifa kwa usalama kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Usajili...
11/08/2026

Ni rahisi k**a 1, 2, 3... 4. ✨

Kuanzia usajili hadi kuingiza taarifa kwa usalama kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Usajili na Utambuzi wa Watu (e-RITA), inachukua hatua nne tu rahisi kuhakikisha kila mtoto anapata utambulisho wake wa kwanza wa kisheria.

Tazama jinsi usajili unavyofanyika.

“Kila mtoto anayehesabiwa ni mtoto ambaye haki zake zinaweza kulindwa.” — Elke Wisch, Mwakilishi wa UNICEF TanzaniaLeo m...
10/08/2026

“Kila mtoto anayehesabiwa ni mtoto ambaye haki zake zinaweza kulindwa.” — Elke Wisch, Mwakilishi wa UNICEF Tanzania

Leo mjini Dodoma, Tanzania imeungana na nchi nyingine za Afrika kuadhimisha Siku ya Usajili wa Kiraia na Takwimu Muhimu Afrika . Zaidi ya watoto milioni 12 tayari wamepata utambulisho wao wa kwanza wa kisheria kupitia usajili wa vizazi, chini ya uongozi wa Serikali ya Tanzania, kwa ushirikiano na UNICEF na kwa msaada wa Canada’s International Development – Global Affairs Canada na Yas Tanzania.

Aidha, European Union in Tanzania inaendelea kushirikiana na UNICEF katika kuimarisha miundombinu ya kidijitali ya umma, kwa ajili ya mfumo wa usajili wa vizazi na utambulisho wa kidijitali uliojumuishi na unaounganisha huduma mbalimbali.

10/08/2026

Kwa pamoja, tunaweza kufanya “Kila Mtu Kutambulika Afrika” kuwa kweli.

Cheti cha kuzaliwa ni zaidi ya hati; ni utambulisho wa kwanza wa kisheria wa mtoto na ni njia ya kupata huduma za afya, elimu, ulinzi na huduma nyingine muhimu.

Kwa zaidi ya miaka 30, UNICEF imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kuimarisha usajili wa vizazi, ikiwemo kupitia ushirikiano na Yas Tanzania na kwa msaada wa Canada’s International Development – Global Affairs Canada. Kwa pamoja, tunarahisisha usajili wa watoto kwa akina mama k**a Zaituni na familia kote Tanzania kupitia huduma zilizopanuliwa, ubunifu wa kidijitali na uhamasishaji wa jamii.

Katika , tunaangazia umuhimu wa usajili wa kuzaliwa na tofauti unaoleta katika maisha ya watoto.

Unyonyeshaji hustawi pale akina mama wanapopata msaada wanaouhitaji.Katika uzinduzi wa Kitaifa wa   uliofanyika Tanga, S...
07/08/2026

Unyonyeshaji hustawi pale akina mama wanapopata msaada wanaouhitaji.

Katika uzinduzi wa Kitaifa wa uliofanyika Tanga, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau walisisitiza dhamira yao ya kuhakikisha kila mama anapata msaada anaohitaji ili aweze kunyonyesha kwa mafanikio.

Tukio hilo liliimarisha ujumbe muhimu kwamba kuunga mkono unyonyeshaji ni kuwekeza katika mifumo imara ya afya, ushauri bora wa unyonyeshaji, na mazingira yanayowawezesha akina mama kunyonyesha kwa kujiamini.

Kwa pamoja, tunaweza kuhakikisha kila mama anapata msaada na kila mtoto anaanza maisha akiwa na afya bora zaidi.

Kutokomeza utapiamlo mkali kwa watoto kunaanza na ushirikiano imara.UNICEF, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Tanzania,...
07/08/2026

Kutokomeza utapiamlo mkali kwa watoto kunaanza na ushirikiano imara.

UNICEF, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Tanzania, TFNC Tanzania, na Ofisi ya Rais - Tamisemi, iliwaleta pamoja wadau mjini Morogoro kujadili namna ya kuimarisha utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Kuzuia Utapiamlo Mkali na Uvimbe Utokanao na Utapiamlo.

Viongozi wa serikali, wataalamu wa lishe, taasisi za elimu, washirika wa maendeleo na wadau wa utekelezaji walibadilishana uzoefu na kujadili hatua za kuzuia utapiamlo mkali kwa watoto, kuboresha huduma za lishe na kuimarisha mifumo inayowafikia watoto na familia.

Kwa pamoja, tunaimarisha mifumo ya lishe ili kuhakikisha kila mtoto ana nafasi ya kuishi, kukua na kustawi.

Unyonyeshaji huwa rahisi zaidi pale akina mama wanapopata msaada wanaouhitaji.Baba ana mchango muhimu katika safari ya u...
05/08/2026

Unyonyeshaji huwa rahisi zaidi pale akina mama wanapopata msaada wanaouhitaji.

Baba ana mchango muhimu katika safari ya unyonyeshaji kwa kuwahamasisha, kuwasaidia na kushiriki bega kwa bega na mama, hivyo kuwapa watoto mwanzo bora zaidi wa maisha.

Familia imara huchangia watoto kupata mwanzo imara wa maisha.

Maziwa ya mama ni zaidi ya chakula; ni kinga ya kwanza ya mtoto.Kuanzia kuimarisha kinga ya mwili wa mtoto hadi kumpatia...
04/08/2026

Maziwa ya mama ni zaidi ya chakula; ni kinga ya kwanza ya mtoto.

Kuanzia kuimarisha kinga ya mwili wa mtoto hadi kumpatia virutubisho vyote anavyohitaji ili akue na kustawi, unyonyeshaji humpa kila mtoto mwanzo wenye afya bora maishani.

Katika Wiki ya Unyonyeshaji Duniani, tushirikiane kuhakikisha kila mama anapata msaada anaohitaji ili kumpa mtoto wake mwanzo wenye afya bora maishani.

Kila mtoto anastahili mwanzo bora wa maisha.Safari hiyo huanza ndani ya saa ya kwanza baada ya kuzaliwa. Kumnyonyesha mt...
03/08/2026

Kila mtoto anastahili mwanzo bora wa maisha.

Safari hiyo huanza ndani ya saa ya kwanza baada ya kuzaliwa. Kumnyonyesha mtoto ndani ya saa ya kwanza baada ya kuzaliwa, kumnyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza, na kuendelea kumnyonyesha sambamba na kumpatia vyakula vya nyongeza hadi afikishe miaka miwili au zaidi, humuwekea msingi imara wa afya, ukuaji na maendeleo.

Katika , tushirikiane kuhakikisha kila mama anapata msaada anaohitaji ili kumpa mtoto wake mwanzo bora wa maisha.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UNICEF TANZANIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to UNICEF TANZANIA:

Shortcuts

Share