27/07/2026
Tunayo furaha kubwa kumkaribisha rasmi Bi. Ida Andrew Jaribu katika nafasi ya Katibu na Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Tanzania Paralympic Committee (TPC).
Tunaamini kuwa uzoefu, weledi, maono na kujitolea kwake vitachangia kwa kiwango kikubwa kuimarisha maendeleo ya michezo ya watu wenye ulemavu nchini Tanzania na kuwafungulia wanamichezo wetu fursa zaidi za kung'ara kitaifa na kimataifa.
Kwa pamoja, tuendelee kujenga jamii yenye ushirikishwaji, usawa wa fursa na mafanikio kupitia michezo.
Karibu sana kwenye familia ya TPC, Bi. Ida Andrew Jaribu! ๐๐๐๐ค