Youth with disabilities organization

Youth with disabilities organization Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Youth with disabilities organization, Community Organization, mbezi kati street mbezi beach Goba Road, Dar es Salaam.

Youth with Disabilities Organization (YoWDO) is a registered non-governmental organization that work to promote the welfare of all youth with disabilities in Tanzania and envision the communities where YWDs enjoy their rights.

Happy Easter to you All
05/04/2026

Happy Easter to you All

Happy New Month 01 April 2026
01/04/2026

Happy New Month 01 April 2026

Heri ya Siku ya Wanawake Duniani! 🌸Leo tarehe 08/03/2026 Shirika la Vijana wenye Ulemavu (YoWDO) tunasherehekea nguvu, u...
08/03/2026

Heri ya Siku ya Wanawake Duniani! 🌸
Leo tarehe 08/03/2026 Shirika la Vijana wenye Ulemavu (YoWDO) tunasherehekea nguvu, ujasiri na mchango mkubwa wa wanawake katika jamii zetu. Tunaamini kila mwanamke ana haki ya kuheshimiwa, kusikilizwa na kupewa nafasi sawa bila kujali hali yake.

Tunahasa jamii juu ya ujumuishwaji, usawa na upendo kwa wanawake wote, hasa wanawake na wasichana wenye ulemavu ambao mara nyingi hukutana na changamoto nyingi katika jamii. Ni wajibu wetu k**a jamii kuhakikisha wanapata fursa sawa katika elimu, ajira, uongozi na maendeleo ya kiuchumi.

Tuungane kuondoa vikwazo, kubadili mitazamo na kujenga dunia ambayo kila mwanamke na kila mtu mwenye ulemavu anaweza kufikia ndoto zake. Kumbuka Ujumuishwaji ni haki si hisani.
Tunakutakia Heri ya siku ya Wanawake Duniani.





Hello FebruaryHappy New month
01/02/2026

Hello February
Happy New month

DALASA LA LUGHA YA STAHA - 01UNAWAJUA WATU WASIOONA? Watu wasioona ni watu waliopoteza uwezo wa kuona kwa macho. Kundi h...
17/01/2026

DALASA LA LUGHA YA STAHA - 01

UNAWAJUA WATU WASIOONA?
Watu wasioona ni watu waliopoteza uwezo wa kuona kwa macho. Kundi hili linajumuisha:

1: Watu wasioona kabisa, na

2: Watu wenye uoni hafifu (wanaoweza kuona kwa kiwango kidogo).

Unapokutana au kuwasiliana kwa mara ya kwanza na mtu asiyeona, ni muhimu kutumia lugha ya staha na kuzingatia mawasiliano yenye heshima na uelewa.

Tafadhali endelea kufuatilia darasa hili kupitia mitandao yetu ya kijamii.

IJUE LUGHA YA STAHA NA UMUHIMU WAKE KWENYE JAMII JUMUISHILugha ni nyenzo muhimu katika jamii, si chombo cha mawasiliano ...
08/01/2026

IJUE LUGHA YA STAHA NA UMUHIMU WAKE KWENYE JAMII JUMUISHI

Lugha ni nyenzo muhimu katika jamii, si chombo cha mawasiliano tu bali pia ni kiungo kikuu kinacho chochea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Lugha humtambulisha mtu, kundi au jamii fulani na hivyo lugha ni sehemu muhimu ya utamaduni na utu wa binadamu.

Hata hivyo, watu wenye ulemavu tumekuwa tukikumbana na changamoto za kuitwa au kutambuliwa kwa misingi ya ulemavu tulionao badala ya majina yetu halisi, nafasi zetu katika jamii na utu wetu k**a binadamu.

Ukweli ni kuwa lugha isiyo ya staha kwetu Watu wenye Ulemavu inasababisha madhara makubwa ya kisaikolojia na kijamii ikiwemo kupungua kwa kujiamini, kushuka kwa uthamani binafsi, kutengwa na jamii na wakati mwingine kushindwa kufikia malengo na ndoto zetu.

Kwa kulitambua hili, Shirika la Vijana Wenye Ulemavu (YoWDO) tunaamini kuwa matumizi ya lugha yenye staha ni msingi wa kujenga jamii yenye usawa, heshima na jumuishi. Kutokana na imani hii, YoWDO tumeandaa mafunzo maalum ya Lugha ya Staha kwa Watu wote tukiwa na lengo la kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya maneno, mitazamo chanya na heshima katika mawasiliano ya kila siku.

Mafunzo haya yatatolewa bila malipo kupitia mitandao ya kijamii ya YoWDO yakilenga kujengea jamii uelewa mpana kuhusu lugha yenye utu na nafasi ya watu wenye ulemavu katika maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kwa pamoja, tutumie lugha inayojenga, inayoheshimu utu wa kila mtu na kuimarisha mshik**ano katika jamii yetu.

Karibu darasani.
Mtumie na mwenzako ujumbe huu.

Shirika la Vijana Wenye Ulemavu (YoWDO) tunapoadhimisha mwaka mpya 2026, tunatoa shukrani za dhati kwa wadau, mashirika ...
01/01/2026

Shirika la Vijana Wenye Ulemavu (YoWDO) tunapoadhimisha mwaka mpya 2026, tunatoa shukrani za dhati kwa wadau, mashirika na jamii kwa ujumla kwa ushirikiano na mchango mkubwa mlioutoa katika mwaka 2025 uliosaidia katika kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya ujumuishwaji.

Tunapoanza mwaka huu mpya wa 2026, YoWDO tunaendelea kutoa wito kwa jamii juu ya ujumuishwaji, kujenga mazingira fikivu, kuendeleza usawa wa fursa kwa vijana na watu wenye ulemavu na kujenga jamii jumuishi kwa wote.

Heri ya Mwaka Mpya 2026
Kwa pamoja tujenge jamii isiyomuacha mtu nyuma.

YoWDO tunakutakia heri ya Krismas.Tunaposheherekea Krismas tudumishe upendo, umoja na kuendeleza ujumuishwaji wa watu we...
25/12/2025

YoWDO tunakutakia heri ya Krismas.
Tunaposheherekea Krismas tudumishe upendo, umoja na kuendeleza ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye masuala yote ya kijamii.

YoWDO kwa kushirikiana na Sightsavers - Tanzania tumefanikiwa kutoa mafunzo ya uajirikaji kwa vijana wenye ulemavu ikiwa...
20/12/2025

YoWDO kwa kushirikiana na Sightsavers - Tanzania tumefanikiwa kutoa mafunzo ya uajirikaji kwa vijana wenye ulemavu ikiwa ni hatua nyingine ya mafanikio kupitia Mradi wa RISE/E. Mafunzo haya yamelenga kuwaandaa vijana wenye ulemavu walio hitimu VETA, vyuo vya kati pamoja na vyuo vikuu katika mchakato mzima wa kutafuta ajira, ikiwemo uandishi wa barua za maombi ya kazi, uandaaji wa wasifu binafsi (CV), maandalizi ya usahili (Interview) pamoja na misingi na taratibu za mazingira ya kazi. Aidha, vijana wamewezeshwa kupata maarifa muhimu yanayohitajika katika safari yao ya utafutaji wa ajira.

Sambamba na hilo, YoWDO tumefanikiwa kuwaunganisha vijana hawa kwenye mfumo wa kidijitali wa ajira wa shirika, ujulikanao k**a *YoWDO Connect Portal* unaowarahisishia waajiri na wadau kuwafikia kwa urahisi.

Tunatoa wito kwa wadau, asasi, mashirika, pamoja na watu binafsi wenye nafasi za ajira, mafunzo kwa vitendo (internship), fursa mbalimbali au shughuli za uzalishaji, kuwatumia vijana hawa wenye sifa na uwezo. Unaweza kupata taarifa zao kupitia tovuti: www.yowdo.career.or.tz
Tunatoa shukrani za dhati kwa wadau wetu wote wanaoendelea kutuunga mkono na kushirikiana nasi katika kuhakikisha jamii ya watu wenye ulemavu inajikwamua kiuchumi na kupata fursa zenye usawa.

Mr. Godwini Kabalika Mkurugenzi Sightsavers - Tanzania akipita kwenye banda la maonyesho lililo sheheni wajasiriamali we...
03/12/2025

Mr. Godwini Kabalika Mkurugenzi Sightsavers - Tanzania akipita kwenye banda la maonyesho lililo sheheni wajasiriamali wenye ulemavu wanaojishughulisha na kutengeneza na kuuza bidhaa za usafi, ngozi, chakula pamoja na mapambo. YoWDO tunatoa shukurani za dhati kwa serikali, viongozi, wadau, asasi na watu wote mlioshiriki maadhimisho ya siku ya Watu wenye ulemavu ikiwa k**a sehemu ya kuhakikisha tunajenga jamii yenye usawa na inayompa kipaumbele mtu mwenye Ulemavu.

Mgeni rasmi Mh. Adam Kighoma Malima - Mkuu wa Mkoa Morogoro akipita kwenye banda la wajasiriamali waliopata mafunzo ya u...
03/12/2025

Mgeni rasmi Mh. Adam Kighoma Malima - Mkuu wa Mkoa Morogoro akipita kwenye banda la wajasiriamali waliopata mafunzo ya uajirikaji na kujiajiri kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na YoWDO kwa kushirikiana na Sightsavers - Tanzania pamoja na wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha mtu mwenye ulemavu anajikwamua kiuchumi pamoja na kufanyakazi yenye staha kulingana na ujuzi au elimu aliyo nayo. Maadhimisho ya siku ya Watu wenye Ulemavu yamefanyika Mkoani Morogoro December 03, 2025 ikiwa k**a sehemu ya kuonyesha jamii umuhimu wa kujumuisha Watu wenye Ulemavu kwenye masuala ya kiuchumi na kijamii.

Address

Mbezi Kati Street Mbezi Beach Goba Road
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Youth with disabilities organization posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Youth with disabilities organization:

Share