18/09/2024
"Kwa yamini yangu, naahidi ya kuwa, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu, Kutimiza wajibu wangu, kwa mungu na taifa langu, kuwasaidia watu siku zote na kutii kanuni za skauti"
Hiyo ni ahadi wanayofundishwa vijana mara tu wanapoingia katika chama cha skauti na ndio ahadi waliyonayo skauti wote ulimwenguni...
Unaweza kuilinganisha Ahadi hiyo ya skauti na daraja imara linalounganisha mtu, jamii yake na ulimwengu.
K**a daraja linavyojengwa juu ya msingi thabiti, ni sawa na Ahadi ya Skauti ilivyoundwa kwa kutegemea maadili muhimu k**a uaminifu, uzalendo na kusaidia wengine.
Wakati Skauti wanaposoma ahadi yao, wanasema, "Nitashikilia maadili haya na kusaidia Skauti wenzangu na jamii yangu." Ahadi hii inawasaidia kuvuka mito ya matatizo na mabonde ya shaka, ikihakikisha wanaweza kufikia malengo yao huku wakisaidia wengine.
Mazingatio:
katika ahadi ya skauti, tunajifunza mambo kadhaa muhimu. Kwanza, tunajifunza umuhimu wa uaminifu na kujitolea kwa jamii.
Pia, tunajifunza kuheshimu wengine. Aidha, ahadi hii inatufundisha kuwa na nidhamu na kujitahidi kuwa bora katika kila jambo tunalofanya. Kwa ujumla, ahadi ya skauti inatufundisha maadili na tabia nzuri ambazo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku.
Imeandaliwa na:
Asedi Hassani