30/03/2026
Magenius wa .club.11 katika wasaa murua na mwandishi wa kitabu cha Hisa, Akiba na Uwekezaji, Mwl. Emilian Busara... na kwa kweli ilikuwa ni moto sana.
Kupitia mazungumzo ya kina, tulibahatika kudondokewa na mbinu za kipekee na zenye maarifa ya uwekezaji ambazo zinaweza kubadilisha kabisa mtazamo na matokeo ya kifedha kwa yeyote aliye tayari kuchukua hatua.
Hizi hapa baadhi ya nukuu nakudokolea...
“Wekeza zaidi ya unavyoweka akiba.”
“K**a umepata kuku anayetaga mayai ya dhahabu usimchinje, kula mayai yake halafu endelea kumfuga.”
“Usiwe mviziaji kuwa mwekezaji. (Stick on the fundamentals rather than sentimentals).”
“Wekeza Tanzania, hapa kuna utajiri mwingi na fursa zaidi.”
“Asilimia kubwa ya matokeo ya uwekezaji wako yatatokana na sehemu chache ulizowekeza, angalia wapi panatoa faida zaidi na ukazane huko.”
“Fanya kazi na biashara kwa bidii ujenge msingi mzuri wa mwendelezo wa mtaji wa uwekezaji wako.”
“Weka malengo ya uwekezaji wako na uwe mvumilivu na mwenye dira iliyonyooka hadi utakapoyafikia.”
Kinachogusa zaidi ni jinsi mwalimu alivyoonesha furaha na kuvutiwa na kiwango cha nidhamu, uelewa, na ari ya members... akitambua kuwa kundi hili linaenda kuwa mfano wa matokeo halisi ya elimu ya kifedha. Ameendelea kuthibitisha kwa vitendo namna anavyogusa maisha ya wengi kupitia maarifa anayoshirikisha.
Na ndio… tulikula vizuri 😄 lakini zaidi ya yote, tulijifunza kwa kina.
K**a ishara ya dhamira yetu, tumekubaliana kukutana naye tena baada ya miaka mitano... si kwa mazungumzo tu, bali kuonesha matokeo halisi ya safari zetu za uwekezaji.
Huu sio mwisho… ni mwanzo wa hadithi za mafanikio.