Veriafya

Website

Veriafya Taarifa sahihi za afya bila upotoshaji! Fanya kazi nasi:
πŸ—¨οΈ DM
βœ‰οΈ[email protected]

Fahamu chanzo cha maumivu makali ya hedhi na jinsi ya kuyatibu ukiwa nyumbani
20/09/2026

Fahamu chanzo cha maumivu makali ya hedhi na jinsi ya kuyatibu ukiwa nyumbani

π‚π‘π„πƒπˆπ“: Baadhi ya picha na video zilizotumika kukamilisha kazi hii ...

20/09/2026

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi anasisitiza umuhimu wa kutunza afya na kufanya mambo kwa kiasi kuliko kutunza fedha kwa ajili ya kutibu magonjwa uzeeni.

Anaeleza kuwa tabia mbaya za maisha, k**a vile unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara, zinasababisha madhara makubwa kwa viungo k**a vile moyo kupanuka na mapafu kuharibika.

Hivyo, anatoa wito wa kuchukua hatua za kinga mapema na kuwekeza katika mifumo endelevu ya afya ili kuwa na nguvu kazi yenye afya kwa muda mrefu.

Video: Mwananchi Digital

19/09/2026

Ulaji wa nyama unaoshauriwa kiafya ni ule wa kuichemsha kwanza kuliko kuichoma kwenye joto kali kwani huongeza hatari ya kuugua saratani ya Utumbo mpana.

Haya yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Watoto, Lucas Mkeni kizungumza kupitia kituo cha Wasafi media

19/09/2026

Daktari Bingwa wa Watoto, Lucas Mkeni kizungumza kupitia kituo cha TBC anaeleza kuwa maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto kwa sababu yanamkinga na magonjwa mbalimbali k**a Nimonia, kuhara, pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza k**a shinikizo la damu na kisukari.

Pia ameeleza kuwa maziwa ya mama ni safi, yanapatikana wakati wote bila gharama wala maandalizi, na yanasaidia kuongeza uwezo wa akili (IQ), kufikiri na kumbukumbu kwa mtoto, ndio maana madaktari wanasisitiza unyonyeshaji wa maziwa pekee kwa miezi sita ya kwanza na kuendelea hadi miaka miwili.

18/09/2026

Kurudia mafuta yaleyale kupikia na kukaangia vyakula ni tabia inayoongeza hatari ya kupata saratani ya utumbo mpana.

Haya yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Watoto, Lucas Mkeni kizungumza kupitia kituo cha Wasafi media

17/09/2026

Utumiaji wa Energy drinks na vinywaji vingine vyenye sukari nyingi k**a soda huongeza hatari ya kuugua Saratani ya utumbo mpana.

Haya yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Watoto, Lucas Mkeni kizungumza kupitia kituo cha Wasafi media

Dalili 9 za Ovulation kuonesha ukishiriki tendo la ndoa unaweza kupata mimba
17/09/2026

Dalili 9 za Ovulation kuonesha ukishiriki tendo la ndoa unaweza kupata mimba

π‚π‘π„πƒπˆπ“: Baadhi ya picha na video zilizotumika kukamilisha kazi hii ...

17/09/2026

Akizungumza kupitia Clouds Media, Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Nathanael Mtinangi anaeleza kuwa ili mwanamke apate ujauzito, mwanamume anahitaji kuwa na mbegu zaidi ya milioni 20. Tofauti na wanawake ambao huzaliwa na idadi maalum ya mayai, mfumo wa uzazi wa mwanamume hufanya kazi k**a kiwanda kinachozalisha mbegu mpya.

Kufanya tendo la ndoa kila siku hasa kwa wanandoa wanaopitoa kipindi kigumu cha kupata watoto hupunguza kiwango cha mbegu chini ya milioni 20 kwa sababu mwili unahitaji siku 3 hadi 5 kutengeneza mbegu zenye ubora na idadi ya kutosha.

16/09/2026

Akizungumza kupitia kituo cha Wasafi media, Daktari Bingwa wa Watoto, Lucas Mkeni anabainisha kuwa mojawapo ya mambo yanayoweza kuongeza hatari ya kupatwa na Saratani ya Utumbo ni ulaji wa nyama za kusindika, hasa soseji.

Tuambie, wewe unakula soseji mara ngapi kwa wiki?

15/09/2026

Dalili za minyoo kwa watoto na umuhimu wa kuwapa dawa mapema

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Veriafya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share