yowedfoundation2019

yowedfoundation2019 Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from yowedfoundation2019, Non-Governmental Organization (NGO), Mbezi luis mwisho, Makao Makuu, Dar es Salaam.

  every visit to a health facility, there is a story, a fear, and a hope for care 🤍No woman or girl should ever feel jud...
09/04/2026

every visit to a health facility, there is a story, a fear, and a hope for care 🤍

No woman or girl should ever feel judged, unsafe, or silenced when seeking the services that could save her life. Respect, privacy, and compassion are not optional—they are rights.

Let’s break the barriers of stigma and build a system where every voice is heard, every choice is respected, and every life is valued.

Together, we can create safe spaces for all.

HerVoiceMatters

Kila msichana ana haki ya kuchagua lini na k**a anataka kuwa na mtoto. 💙Lakini bado wengi wanakosa taarifa sahihi na hud...
09/04/2026

Kila msichana ana haki ya kuchagua lini na k**a anataka kuwa na mtoto. 💙

Lakini bado wengi wanakosa taarifa sahihi na huduma rafiki za uzazi wa mpango—hali inayowaweka kwenye hatari ya mimba zisizotarajiwa na changamoto za kiafya.

Tuache ukimya, tuvunje unyanyapaa, na tuhakikishe huduma za afya zinapatikana kwa wote bila hukumu. Elimu na upatikanaji wa huduma ni ufunguo wa maisha salama na yenye heshima. ✨
YouthMatter

Uimarishaji wa huduma baada ya mimba kuharibika si chaguo—ni haki ya kila mwanamke. 💙Vituo vya afya vinapaswa kuwa na da...
09/04/2026

Uimarishaji wa huduma baada ya mimba kuharibika si chaguo—ni haki ya kila mwanamke. 💙

Vituo vya afya vinapaswa kuwa na dawa, vifaa, na wahudumu wenye ujuzi ili kuhakikisha huduma salama, yenye heshima, na inayookoa maisha.
Tujenge mfumo wa afya unaojali, unaosikiliza, na unaotoa matumaini. ✨

Pamoja na Binti Salha na Catalysts tunaendelea kusukuma mabadiliko chanya kwa afya na haki za uzazi.

WomenMatter

Ukweli huu hauzungumzwi mara nyingi.Utoaji mimba usio salama unaendelea kuhatarisha maisha ya wanawake wengi—ukichangia ...
16/03/2026

Ukweli huu hauzungumzwi mara nyingi.

Utoaji mimba usio salama unaendelea kuhatarisha maisha ya wanawake wengi—ukichangia sehemu kubwa ya wanaolazwa hospitalini kutokana na matatizo ya ujauzito na hata vifo vya uzazi.

Ndiyo maana taarifa sahihi, elimu ya SRHR, na mazungumzo ya wazi ni muhimu. Ukimya hauwalindi wanawake—uelewa ndio kinga.

Tuondoe dhana, tujenge uelewa.

Uelewa wa sheria ni sehemu muhimu ya kufanya maamuzi salama. Mara nyingi ukimya na hofu hutufanya tuamini dhana badala y...
16/03/2026

Uelewa wa sheria ni sehemu muhimu ya kufanya maamuzi salama. Mara nyingi ukimya na hofu hutufanya tuamini dhana badala ya ukweli.

Tafuta taarifa sahihi, uliza maswali, na elewa haki zako kabla ya kufanya maamuzi yanayohusu Afya ya uzazi na maisha yako.

Mazungumzo ya wazi yanajenga uelewa na kuondoa hukumu zisizo na msingi.

Mazungumzo ya wazi yana nguvu ya kubadilisha jamii.Tukiondoa dhana potofu na kuhukumu, tunafungua nafasi ya kuelewana, k...
15/03/2026

Mazungumzo ya wazi yana nguvu ya kubadilisha jamii.
Tukiondoa dhana potofu na kuhukumu, tunafungua nafasi ya kuelewana, kujifunza na kukua pamoja.

Tuongee. Tujifunze. Tujenge jamii yenye uelewa zaidi.

Equality is not charity — it’s an investment.Every chance given to a woman multiplies into progress for society.This Wom...
08/03/2026

Equality is not charity — it’s an investment.
Every chance given to a woman multiplies into progress for society.
This Women’s Day: Give to women. The world will gain. ✨

Masuala ya afya ya uzazi kwa vijana bado yamezungukwa na ukimya na taarifa zisizo sahihi.Je, ni kwa namna gani tunaweza ...
08/03/2026

Masuala ya afya ya uzazi kwa vijana bado yamezungukwa na ukimya na taarifa zisizo sahihi.
Je, ni kwa namna gani tunaweza kuhakikisha vijana wanapata elimu rafiki na sahihi kuhusu SRHR!?

Miaka 30 ya Tume ya Kimataifa ya Idadi ya Watu na Maendeleo (ICPD) imekuwa na matunda makubwa, hasa katika upatikanaji w...
30/11/2025

Miaka 30 ya Tume ya Kimataifa ya Idadi ya Watu na Maendeleo (ICPD) imekuwa na matunda makubwa, hasa katika upatikanaji wa Huduma za Afya ya Uzazi! Sasa, kuna uwezo zaidi na ruhusa kwa wanawake na vijana kupata taarifa sahihi na huduma wanazohitaji pamoja na kua na uwezo wa kuchagua na kupanga uzazi hii inamaanisha kua wanawake na vijana wanaweza kujiamulia kuhusu:
* Wakati wa kuanzisha familia.
* Ukubwa wa familia.
* Kufuatilia masomo au kazi bila vikwazo.
Pia kila mtu anastahili huduma za afya za uzazi ambazo ni salama, za heshima, na zinazopatikana kirahisi. Huu ni msingi wa haki za binadamu na maendeleo endelevu.
> "Kupanga uzazi si tu kuhusu idadi ya watoto; ni kuhusu kutoa uwezo wa kupanga maisha, ndoto, na mustakabali wako."

Tusisahau kwamba bado kuna kazi ya kufanya, lakini tunasherehekea hatua kubwa zilizopigwa!
Je, unaweza kushiriki kwa namna gani ufikiaji wa huduma za afya ya uzazi umesaidia katika maisha yako au ya mtu unayemjua? Tuambie kwenye comments! 👇

ICPD30 sio tu inalenga Afya ya Uzazi, bali ni kichocheo kikuu cha kufikia Malengo yote ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Aha...
30/11/2025

ICPD30 sio tu inalenga Afya ya Uzazi, bali ni kichocheo kikuu cha kufikia Malengo yote ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Ahadi hii inahakikisha kwamba tunajumuisha makundi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiachwa nyuma na kweka watu na haki zao katikati ya maendeleo yote. Tunapoelekea 2030, ushirikishwaji wa kila mwanamke na kijana ndiyo njia pekee ya kufikia SDGs zote — kutoka Kupunguza Umaskini (SDG 1) hadi Usawa wa Kijinsia (SDG 5) na Afya Bora (SDG 3).
e, jamii yako inatekeleza vipi kaulimbiu ya "Kutomuacha Mtu Nyuma"? 👇

Miaka 30 ya utekelezaji wa Ajenda ya ICPD (Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo) imewezesha mabadiliko mak...
30/11/2025

Miaka 30 ya utekelezaji wa Ajenda ya ICPD (Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo) imewezesha mabadiliko makubwa duniani, hasa katika kulinda maisha ya akina mama.
Ahadi ya Cairo (ICPD) ililenga sana katika kuwapa wanawake uwezo wa kujifungua salama na kupata huduma bora za afya ya uzazi. Tumepiga hatua kubwa katika kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ujauzito na kujifungua mafanikio haya yamechangiwa na upanuzi wa uzaz salama kituoni , upangaji uzaz na kua na wahudumu waliohitimu kwa kiwango kizur ili kutoa huduma bora na kupunguza vifo na maambukiz mapya ya magonjwa.

Je, wewe au jamii yako inatumiaje huduma za uzazi salama zinazopatikana? Tushirikishe uzoefu wako! 👇

Tanzania imejitolea kikamilifu kwenye ajenda ya ICPD, na katika miaka 30 hii, tumechukua hatua za kihistoria kuhakikisha...
30/11/2025

Tanzania imejitolea kikamilifu kwenye ajenda ya ICPD, na katika miaka 30 hii, tumechukua hatua za kihistoria kuhakikisha elimu inakuwa daraja la fursa kwa wasichana na vijana wote.
Ahadi Kuu za Tanzania Katika Elimu (Kufikia Malengo ya ICPD30):
Rudi shulen; wamama, vijana na wasichana wajawazito kurudi shuleni na kuendelea na masomo yao katika shule za umma. Hii inawapa wasichana fursa ya pili ya kimaisha, na kuvunja mnyororo wa umaskini.

Ahadi ya kuendelea kuwekeza katika kutoa Elimu Kamili ya Ujinsia (CSE) kupitia somo la Stadi za Maisha, ili kuwapa vijana maarifa sahihi, uwezo wa kufanya maamuzi ya busara kuhusu miili yao, na kupunguza mimba za utotoni.

Tujenge utamaduni wa kuunga mkono kurudi shuleni kwa vijana hawa. Je, jamii yako inatekeleza vipi miongozo hii? Tueleze kwenye maoni! 👇

Address

Mbezi Luis Mwisho, Makao Makuu
Dar Es Salaam

Telephone

+255688945176

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when yowedfoundation2019 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to yowedfoundation2019:

Share