01/09/2026
Leo, BUFADESO imepokea timu kutoka Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) – Kituo cha Meatu kwa ajili ya kikao kifupi cha kujifunza kuhusu majukumu ya taasisi zetu, kubadilishana uzoefu na kuchunguza fursa za kuimarisha ushirikiano.
Mkutano huu pia ulitoa fursa ya kuhusianisha kazi zetu na Programu ya Agroforestry for Sustainable Livelihoods, Biodiversity and Climate Change (ASILIB-CC), hususan katika kuendeleza mifumo ya UFUGAJI bora na inayostahimili changamoto, inayoboresha maisha ya wakulima huku ikisaidia kulinda mazingira.
Pia tulipata fursa ya kuwaalika TVLA–Meatu kushiriki katika Maonesho ya Kilimo, yatakayofanyika tarehe 19–21 Oktoba 2026 katika Agroforestry Training Centre (ATC), Bweri, Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara.
Maonesho hayo yatawakutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kuonesha maarifa ya vitendo, ubunifu, teknolojia na uzoefu unaoweza kuchangia katika kuboresha maisha, kujenga ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuongeza uwekezaji katika kilimo-misitu.
TVLA–Meatu imealikwa kushiriki kupitia banda la maonesho au jukwaa lingine linalofaa, ili kutoa nafasi ya kushirikisha wakulima na washiriki wengine maarifa na taarifa muhimu kuhusu afya na huduma za mifugo.