SANJA LUPO

SANJA LUPO Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from SANJA LUPO, Environmental conservation organisation, MWANZA, Bariadi.

MARAFIKI HATARIMarafiki zako wanazo sifa hizi?Kuna aina za marafiki ambao tunawaita marafiki hatari kwenye maisha yako, ...
01/01/2026

MARAFIKI HATARI

Marafiki zako wanazo sifa hizi?

Kuna aina za marafiki ambao tunawaita marafiki hatari kwenye maisha yako, wanaweza kuwa ni marafiki ambao upo nao karibu, umetoka nao mbali, mnaishi pamoja, kwa bahati mbaya wakawa ni marafiki ambao hawana mchango wowote kwenye maisha yako na wanaweza kuwa na madhara baadae.

Inashauriwa, ni muhimu sana kwa kila rafiki ulienae umpitishe kwenye vipimo maalum ambavyo vitakusaidia k**a huyo rafiki unaweza kuendelea kumuamini au uendelee kuwa nae bila kumtegemea sana.

1. Hawawezi kukutaja kwenye fursa, ni rafiki kweli, anazo fursa fursa nyingi lakini hawezi kukutaja licha ya kufahamu Uwezo na Uzoefu wako. Ukweli ni kwamba yupo tayari kuwa-recommend/Kuwataja/Kuwasemea wengi lakini sio wewe, anahisi akikutaja atakuwa amekupendelea sana, wapo na wewe tu kutokana na kwamba kuna kitu wanapata kwako ila kiukweli hawafurahii kukua kwako.

2. Hawaamini katika Ndoto Zako, ukiwashirikisha kuhusu ndoto zako/malengo yako, hawaamini kabisa, wanaku-doubt sana, hawakupi sapoti yoyote, kila siku wanakukosoa, wanakukatisha tamaa, hawaamini ndoto zako.

3. Hawapatikani kwenye changamoto zako, ukiwa na changamoto hawapatikani, una kesi polisi/umefukuzwa kazi/Huna hela n.k, Yaani ukiwa na changamoto hawapatikani kabisa, wapo bize. Hawapo tayari kukusaidia, hawapo tayari kuambatana na wewe ukipitia changamoto fulani. Watakuwa na wewe tu ukiwa unang'ara na watakukana ukiwa kwenye changamoto.

4. Wanaamini ni lazima wakuzidi, wanataka wakuzidi katika kila kitu, Hela/Umaarufu/Akili/Kimawazo n.k, ukianza kuwazidi tu basi ni tatizo. Wanaamini kuwa siku zite lazima uwe chini yao, ukianza kuwazidi tu wanachukia, wazo lao wanaamini lazima lishinde, wanaamini hutakiwi kuwa mtu mkuu au mtu mkubwa zaidi yao.

Asanteni kwa kuendelea kuwa pamoja na sisi katika programmes zetu.

Subscribe: https://www.youtube.com/channel/UC38VdUM5jqXy2d7gDQSXyYg

Muda wowote ukiwa tayari kujifunza kwa kina kutoka kwangu Bofya hapa
>>>

Entertainments and Educational programmes

01/01/2026

MADHARA YA KUNYWA SOFT DRINKS ( SODA JUICE NA KADHARIKA)

Kunywa soft drinks mara kwa mara kunaweza kuwa na madhara kwa afya kwa sababu hizi kuu:

(Kwa kifupi, soft drinks ni vinywaji vyenye: Gesi (carbonation), Sukari nyingi au sweeteners, na caffeine hapa tunaongelea soda zote na baadhi ya juisi)

1. Sukari nyingi sana
Soft drinks nyingi zina sukari nyingi, ambayo:
Huongeza hatari ya unene
Huongeza uwezekano wa kisukari (diabetes type 2)
Husababisha kuchoka haraka baada ya muda mfupi
I
2. Huharibu meno 🦷
Sukari + asidi kwenye soft drinks:
Huoza meno na Hupunguza uimara wa enamel ya meno

3. Huathiri mifupa🦴
Baadhi ya soft drinks (hasa coca cola):
Hupunguza kiwango cha calcium
Huongeza hatari ya mifupa kuwa dhaifu (osteoporosis)

4. Hakuna virutubisho muhimu
Soft drinks: Hazina vitamini, madini, wala protini Ni “kalori tupu” — zinaongeza uzito bila kujenga mwili

5. Huongeza hatari ya matatizo ya moyo ❤️
Kunywa mara kwa mara Huongeza shinikizo la damu na hatari ya magonjwa ya moyo

6. Husababisha utegemezi (addiction)
Mchanganyiko wa sukari na caffeine hufanya mtu atamani kunywa tena na tena
Kuacha ghafla kunaweza kusababisha maumivu ya kichwa au uchovu
Nini mbadala bora?

Maji 💧
Maji ya matunda asilia (bila sukari)
Maziwa
Chai bila sukari

UTAJUAJE KINYWAJI UNACHOKUNYWA NI SOFT DRINK UKIACHANA NA SODA👍
➡️Hivi ndivyo jinsi ya kusoma lebo ya kinywaji ili ujue k**a ni soft drink au la:
1️⃣ Angalia Sukari (Sugar)
Ikiandikwa Sugar, Sucrose, Glucose, Fructose, Corn syrup
Zaidi ya 5g kwa 100ml → hiyo ni soft drink Ina maanisha kwamba Chupa moja inaweza kuwa na vijiko 6–10 vya sukari 😬
2️⃣ Angalia Kalori (Calories)
Kalori nyingi lakini hakuna virutubisho → soft drink Mfano ukikuta imeandikwa : 120–150 kcal bila protini au vitamini
3️⃣ Angalia Asidi
Maneno k**a: Citric acid na Phosphoric acid hii 👉 Huonyesha ni kinywaji chenye asidi (soft drink)
4️⃣ Angalia Caffeine
Ikiwa ipo mara nyingi ni soft drink
5️⃣ Angalia Carbonated
Ikiandikwa Carbonated / Fizzy / Spa

BABA 😭Baba, mwanaume pekee anayekupenda kwa moyo wake wote ni Baba, mengi magumu moyoni kwa Baba ni ngumu kusema, leo ma...
01/01/2026

BABA 😭

Baba, mwanaume pekee anayekupenda kwa moyo wake wote ni Baba, mengi magumu moyoni kwa Baba ni ngumu kusema, leo makosa ya Baba ni rahisi kuwa maarufu kwani wazee wameamua kukaa kimya tu.

Ni kweli Mama ni muhimu, na nafasi yake ni kubwa sana, na mdomo wake unambeba, Baba wanakufa mapema kutokana na kubeba vitu vingi moyoni.

Inashangaza, kadri muda unavyokwenda, upweke kwa Baba unazidi, watoto wanazidi kujenga urafiki na Mama, sheria zipo upande wa Mama kuliko Baba, Dunia haiwapendi akina Baba.

Tazama, vifo vingi vya ghafla ni vya Baba, nyumba nyingi zina wajane, Baba amefariki, Mama anadunda.

Kimsingi, watu wengi wana bibi zao kuliko babu zao.

Baba, Dunia haitupendi, ni rahisi watu na mashirika kusimama pamoja kumtetea Mama lakini sio Baba. Mashirika yameundwa kumpa nguvu Mama, na hata kufikia kuchukua hata haki za Baba.

Baba, tupo njia panda, k**a vifaranga, muda wowote tunachukuliwa na mwewe. Jambo baya likimtokea Baba, ni haki yake ya msingi, tazama Dunia imekuwa dhidi ya Baba, Dunia haicheki na Baba.

Nani k**a mama, waachieni waimbe nani k**a Mama, kwani hakuna wa kuvaa viatu vya Baba.

Maisha mkononi, roho rehani, kuyapa maisha ahueni. Mshua hakutoka kwenye familia tajiri, na bado alihakikisha hatulali njaa na kutupeleka shule, tulitibiwa kila tukipata homa.

Baba, kuna wakati unakaa kimya, sio kwamba huna cha kuongea bali huna uhakika k**a dunia itakuelewa. Tumechagua kucheka wakati wa shida kuonyesha kila kitu kipo sawa. Tunyime kila kitu na tutese kadri uwezavyo, bado tutakuonyesha kuwa sisi ni wanaume.

Kimbiza kwani nakuaminia Baba, hatujaja duniani kulalamika, wanaokuamini acha wabaki, wasiokuamini acha waende.

Kesho tena, tutakuwa na nguvu kuliko jana Baba.

Tusikitike kidogo, nimeshindwa kuendelea kuandika moyo unaumia Baba! 😭😭

Tuwakumbuke Baba zetu.

Entertainments and Educational programmes

Address

MWANZA
Bariadi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SANJA LUPO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share