20/03/2026
FUNGUO ZA MFALME SULEMAN NA MAFUNDISHO YAKE
ALAMA ZA ULINi ZA SULEMAN
Alama za ulinzi zinazo husishwa na Mfalme Suleman ni k**a vile: Muhuri wa Sulemani (Seal of Solomon), na Pentakali (nyota ya ncha tano) ya Sulemani, Alama hizi zilitokana na vitabu vya kale vya Uchawi (Grimoires) vya ulaya ya kati vilivyo kuja kurithiwa na tamaduni za Kiyahudi na za kiislamu.
Vitabu k**a vile "Key of solomon" na "Lemegeton", vimeelezea alama hizi k**a zikitumiwa kwa madhumuni au nia ya Kutaka kujikinga dhidi ya nguvu ovu,Kudhibiti roho au mapepo, na kutafuta hekima.
Katika mafundisho ya uchawi pamoja na sayansi ya mapepo (demonology), alama hizo zinachukuliwa kuwa na mamlaka makubwa ya kuweza kufunga na kudhibiti mapepo. Katika matumizi ya kisasa kwenye tamaduni mbalimbali za hivi leo alama hizo hutumika k**a hirizi za Ulinzi.
ASILI NA UMUHIMU WAKE.
~MUHURI WA SULEMAN (PETE YA SULEMAN)
Katika hadithi maarufu inaelezwa luwa Malaika mkuu Raphael alimpa Suleman pete yenye alama ya kimungu iliyo muwezesha kuwadhibiti mapepo. Inaelezwa kuwa alitumia uwezo huo kuwadhibiti mapepo ili wafanye kazi katika ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu.
~FUNGUO ZA SULEMAN (KEYS OF SOLOMON THE KING)
Key of Solomon The King, ni kitabu cha uchawi kilicho andikwa Ulaya kati ya karne 14 hadi karne ya 17 kikiwa kimekusanya alama nyingi za kichawi (sigils) zinazo daiwa kuwa ni za Sulemani.
~MUUNDO WA ALAMA ZA SULEMANI
Alama hizo za Suleman mara nyingi huonekana k**a; Nyota yenye ncha sita (Hexagram), pamoja na nyota yenye ncha tano (Pentagramu).
MAANA YA SIRI YA ALAMA HIZO
Alama hizi za Sulemani zinawakilisha; Muunganiko wa vitu vinavyo pingana ama nguvu mbili kinzani (mbingu na dunia), pia zinawakilisha Hekima ya Kimungi, pia ni alama zinazo wakilisha Muumganiko wa vipengele muhimu vya ulimwengu yaani Element za uumbaji ambazo ni Maji, ardhi, moto, hewa na Roho.
NGUVU ZAKE NA MATUMIZI YAKE KATIKA UCHAWI.
KUDHIBITI ROHO /MAPEPO
Alama hizi za Sulemani hutumika kudhibiti Roho au mapepo. Katika sehemu fulani kutoka katika Kitabu cha kale cha Uchawi (Grimoire) kinacho julikana k**a "Ars Goetia", inaelezwa kuwa alama hizi hutumika katika ibada za kuita na kudhibiti mapepo 72.
HIRIZI ZA ULINZI
Alama hizi za sulemani hutumika katika ulinzi kujilinda.
Alama za Suleman hutumiwa katika ibada au k**a Hirizi ili, Kufukuza nguvu hasi, kutulinda dhidi ya Roho wabaya.
MIHURI 44 YA SULEMANI
Katika kitabu cha Funguo za Suleman kuna Pentakali maalumu zinazo husishwa na sayari tofauti zikiambatanishwa na malengo yake togauti kulingana na sayari katika uchawi ..mfano
Jupita ...Inahusishwa na Utajiri, Heshima na Afya.
Mars..inahusishwa na ulinzi pamoja na Ujasiri
Sun (Jua).....Inahusishwa na utukufu pamoja na uwezo wa kujificha.
Saturn....inahusishwa na Kudhibiti Roho
MUKTADHA WAKE KWA UJUMLA
Katika Uyahudi na Kabbalah , Alama hizi zinahusishwa na hekima na mamlaka ya sulemani, na pia zinahusishwa na mafundisho ya siri ya Kabbalah.
Katika Mila za Kiislamu; hasa katika simulizi za waislamu, Muhuri wa Suleman unatajwa k**a ishara ya mamlaka aliyo tumia Sulemani kutawala Majini.
Katika Uchawi wa Magharibi; katika sherehe za uchawi wa Ulaya (Ceremonial magic) ya uamsho/Renaissance wa kisasa, alama hizi ni za muhimu sana katika ibada za uchawi
Katika Tamaduni za Kale za Mashariki ya kati, ingawa hazikutokea moja kwa moja huko, dhana ya alama za kichawi (sigils) kutumika katika kudhibiti roho ilikuwepo katika ustaarabu wa kale wa Mesopotamia na Misri, ambapo ilikuja kuathiri hadithi za baadaye za Sulemani
Katika Upagani wa Kisasa (Modern Paganism)
katika baadhi ya mila za kipagani za kisasa, hexagramu/nyota ya ncha sita hutumiwa k**a alama ya Ulinzi na usawa wa nguvu ya asili.
ATHARI YA ALAMA HIZO ZA SULEMAN KATIKA HISTORIA NA JAMII
Kihistoria, Muhuri wa Sulemani uliwahi kuonekana kwenye sarafu na kwenye alama za falme za kiislamu k**a vile Seljuk na Ottoman, na hata kwenye bendera ya mwanamaji mashuhuri aitwaye Barbaros Hayreddin Pasha. Hili linaonyesha kuwa alama hiyo ilihusishwa na Mamlaka, nguvu na Utawala.
Katika dunia ya leo alama hizi hutumika k**a vito vya mapambo, hirizi za Ulinzi pia hutumika k**a ishara ya uhusiano wa kitamaduni na mila za kale za uchawi na mafumbo