15/05/2026
Leo tumesherehekea zaidi ya kuhitimu darasa — tumeshuhudia mwanzo wa safari mpya ya maisha yenye mwelekeo, nidhamu, na uhuru wa kifedha.
Hongereni sana Wahitimu 19 wa Financial Freedom Class 3 kwa kujitoa kwenu, uvumilivu, nidhamu, na moyo wa kujifunza. Mmeonyesha kuwa mafanikio ya kweli hayaanzi na pesa nyingi, bali huanza kwa kubadilisha FIKRA, kujenga MFUMO sahihi, na kuishi kwa NIDHAMU ya kila siku.
Katika safari hii mmejifunza: ✅ Kutengeneza na kusimamia bajeti
✅ Kujenga tabia ya akiba
✅ Kuwekeza kwa hekima
✅ Kusimamia madeni
✅ Kufuatilia matumizi ya fedha
✅ Kujenga urithi na maisha yenye kusudi
Mmekubali ukweli kwamba: 🔹 Mtazamo huamua maamuzi
🔹 Mfumo huamua mwelekeo
🔹 Nidhamu huamua matokeo
🔹 Kusudi huamua matumizi ya fedha
🔹 Mungu ndiye msingi wa hekima na mafanikio ya kweli
Tunaamini wahitimu hawa sasa ni mabalozi wa Uhuru wa Kifedha katika familia, makanisa, biashara, na jamii zao. Tunatarajia kuona maisha yaliyobadilika, maamuzi yenye hekima, biashara zinazokua, familia zenye amani ya kifedha, na viongozi watakaoleta mabadiliko chanya katika jamii.
📖 “Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.” — Mithali 21:5
Safari ya kweli inaanza sasa.
Toka kwenye hustle kwenda kwenye freedom.
Toka kwenye matumizi yasiyo na mpango kwenda kwenye mfumo.
Toka kwenye hofu ya fedha kwenda kwenye amani na utawala.