Compassion International Tanzania

Compassion International Tanzania We currently work with more than 580 churches in 22 regions of Tanzania.

Compassion International Tanzania is one of the largest faith based development organizations in Tanzania committed to releasing children from poverty in Jesus' name.

WASHIRIKI WA MDAHALO WA WADAU KUHUSU KUIMARISHA MALEZI NCHINI TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟWashiriki wa Mdahalo wa Wadau kuhusu Kuimarisha...
04/09/2026

WASHIRIKI WA MDAHALO WA WADAU KUHUSU KUIMARISHA MALEZI NCHINI TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Washiriki wa Mdahalo wa Wadau kuhusu Kuimarisha Afua za Malezi nchini Tanzania katika picha ya pamoja baada ya kushiriki katika majadiliano yenye lengo la kujadili changamoto za malezi, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha malezi bora, salama na chanya kwa watoto nchini Tanzania.

Pamoja tunaweza kujenga jamii inayolinda, kulea na kuendeleza kila mtoto.

Mwanza

Kuelekea Siku ya Mbio za Hisani   ni Malezi Fun Run 2026 ,Wadau wa maendeleo  kutoka mashirika mbalimbali wameshiriki Md...
04/09/2026

Kuelekea Siku ya Mbio za Hisani ni Malezi Fun Run 2026 ,Wadau wa maendeleo kutoka mashirika mbalimbali wameshiriki Mdahalo wa Wadau kuhusu Kuimarisha Afua za Malezi nchini Tanzania . Lengo likiwa ni kujadili changamoto za malezi, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha malezi bora na chanya kwa watoto nchini Tanzania.

Mdahalo huo utaibua maazimio muhimu yatakayotokana na mijadala ya wadau, ambayo yatakusanywa na baadaye kukabidhiwa kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika kilele cha Mbio na Matembezi ya Hisani ya Mtoto ni Malezi Fun Run, tarehe 5 Septemba 2026 Jijini Mwanza.

03/09/2026

Shamra Shamra kuelekea Mbio za hisani ni Malezi Fun Run 2026

WADAU KUJADILI NAMNA YA KUIMARISHA MALEZI NCHINI TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟShirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikian...
03/09/2026

WADAU KUJADILI NAMNA YA KUIMARISHA MALEZI NCHINI TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Shirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo limeandaa Mdahalo wa Wadau kuhusu Kuimarisha Afua za Malezi nchini Tanzania, utakaofanyika tarehe 4 Septemba 2026 Jijini Mwanza, katika Ukumbi wa Ilemela DC.

Mdahalo huo unatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya mashirika 20, viongozi wa dini, viongozi wa serikali, vijana, wazazi pamoja na watoto, kwa lengo la kujadili changamoto za malezi, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha malezi bora na chanya kwa watoto nchini Tanzania.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bw. Eliakim Chacha Maswi.

Mdahalo huo utaibua maazimio muhimu yatakayotokana na mijadala ya wadau, ambayo yatakusanywa na baadaye kukabidhiwa kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika kilele cha Mbio na Matembezi ya Hisani ya Mtoto ni Malezi Fun Run, tarehe 5 Septemba 2026 Jijini Mwanza.

Pamoja tunaweza kujenga jamii inayotoa malezi bora, salama na chanya kwa kila mtoto.

Mwanza

Mtoto ni Malezi Fun Run 2026
03/09/2026

Mtoto ni Malezi Fun Run 2026

  ni Malezi Fun Run 2026
02/09/2026

ni Malezi Fun Run 2026

02/09/2026

WAZAZI WAMEJIPANGA KUSHIRIKI ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ

  ni Malezi Fun Run 2026 ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ
28/08/2026

ni Malezi Fun Run 2026 ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ

Address

Olorien Street
Arusha
P.O.BOX3064

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Compassion International Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Compassion International Tanzania:

Shortcuts

Share