22/05/2026
Karibu FUTURE PILLARS MOVEMENT
Tunapenda kukukaribisha kwa heshima kubwa katika familia ya Future Pillars Movement — kundi lililoanzishwa kwa maono ya kujenga vijana wenye msingi imara kiroho, kijamii, kielimu na kiuchumi.
Group hili limeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kujifunza, kuelimishana na kusaidiana katika maeneo mbalimbali muhimu ya maisha, ikiwa ni pamoja na:
📖 Kujifunza Neno la Mungu
🩺 Elimu ya afya na maisha bora
❤️ Mahusiano yenye afya na maadili mema
💼 Ujasiriamali na kujitegemea
🤝 Kupeana taarifa za kazi na fursa mbalimbali
🎯 Kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji pamoja na karama za watu
Lengo kuu la Future Pillars Movement ni kuifikisha Injili ya Kristo kwa watu mbalimbali na kuwajenga vijana katika misingi sahihi ya maisha kwa kuzingatia agizo la Bwana Yesu Kristo katika Injili ya Mathayo 28:19–20:
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
Kundi hili linawakutanisha pamoja:
• Wachungaji waliopo mafunzoni
• Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania
• Vijana wanaojishughulisha na ujasiriamali pamoja na shughuli nyingine za maendeleo
Katika familia hii hakuna anayekuwa mkubwa wala mdogo; sisi sote ni watu wenye lengo moja la kujifunza, kujijenga, kuinuana na kuwa baraka kwa wengine.
Tunawasihi washiriki wote:
✔ Kuheshimu sheria na taratibu za group
✔ Kushiriki mijadala yenye kujenga
✔ Kutunza upendo, heshima na umoja
✔ Kutumia nafasi hii kujifunza na kukuza uwezo binafsi pamoja na kuwasaidia wengine
Karibu sana Future Pillars Movement
Mahali pa kujifunza, kuunganishwa, kuhamasishwa na kujengwa kwa ajili ya maisha yenye kusudi.