12/02/2026
Kevo na Shiro.💔⛓️💥
Mambo inazidi kuwa nzito Nairobi.
Siku ya Sato, Kevo aliamua kum-surprise Shiro na 'luku' mpya na dinner ya nguvu, lakini surprise ikamgeukia yeye. Alipofika home mapema, alipata Shiro hayuko, na simu yake ilikuwa imebaki kwa meza ikilia bila mpango. Kufungua, akakutana na mapicha na ma-voice note za "mubaba" fulani wa Westy wakipanga vile wata-fly out weekend. Ile imani yote Kevo alikuwa nayo kwa Shiro ikaanguka k**a ghorofa ya mjengo mbaya. Kevo alikumbuka vile walikuwa wanakula ugali-mali wakiwa mamburush, akashindwa ni lini Shiro alibadilisha ile "pure love" yao akaiuza kwa bei ya jioni kwa ajili ya sherehe ya kitambo kidogo. Kila jasho alimwaga Gikomba na kila deal alipiga kusetia bibi yake life poa, ilionekana k**a upuuzi mbele ya ule usaliti.
Shiro alipofika home saa nane ya usiku akiwa na 'kakitu' kichwani, alipata Kevo amekaa kwa giza, macho yamejaa uchungu yenye huwezi elezea. Hakukuwa na kelele, ni ule ukimya wa "game over" wenye unakata kuliko kisu. Shiro alijaribu kutoa ma-excuse za "ni marafiki tu wa biz," lakini Kevo alikuwa ameshafika mwisho; ile ndoto yao ya utotoni ilikuwa imekuwa majivu. Yale maisha walijenga kwa miaka kumi, kuanzia kutembea kwa miguu mpaka kuendesha mashine kubwa, ilivunjika sekunde moja kwa sababu ya tamaa ya "soft life" ya uongo. Shiro alibaki amepiga magoti akilia akijua amempoteza yule msee pekee alikuwa radhi kumpea dunia yote, huku Kevo akitoka nje ya hiyo nyumba, akiacha nyuma si tu mwanamke, bali ahadi zote walizopeana wakiwa watoto wa miaka kumi na tisa.
tu?