22/09/2026
Defenders coalition ni Podcast inayoangazia masuala ya haki za binadamu nchini Kenya, kwa kuzungumzia changamoto, mafanikio na mchango wa watetezi wa haki za binadamu katika kulinda haki na uhuru wa wananchi.
Pia, inalenga kutoa elimu, kuhamasisha usalama wa watetezi na kutetea mazingira bora ya kisheria na kitaasisi yanayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa usalama na ufanisi.
Katika kipindi hiki haswa Kevin Mwachiro anazungumza na mwanaharati Francis Auma ukipenda Gambasugu ni mtetezi wa haki za binadamu na mratibu wa shughuli za kijamii kutoka Makupa, jijini Mombasa.
Akiwa na nguvu na uchangamfu wa kipekee unaovutia kila anapoingia, Francis anazungumzia katika kipindi hiki namna ya kuweka uwiano kati ya harakati za kutetea haki za binadamu na maisha ya familia.
Kipindi hiki kiko katika chaneli ya Defenders coalition