17/06/2026
UKWELI MCHUNGU KWA MAFUNDI UJENZI:
Naomba niseme jambo ambalo huenda wengi wetu hatupendi kulisikia lakini nalisema.
Kwa miaka mingi baadhi ya mafundi ujenzi wanaamini kwamba kila wanachohitaji ili kufanikiwa katika taaluma hii ni kuwa na mwiko, mkono bao, kabiro, kamba line,steel,futi mpya na pima maji basi.
Kisha mtu huyo anakaa mahali akilalamika kwamba wateja hawawathamini.Mafundi wanachukuliwa kwa bei ya chini na jamii haiheshimu taaluma yao.
Lakini nauliza swali moja tu:
Kwa nini mteja akulipe k**a mtaalamu wa kisasa wakati wewe bado unafanya kazi k**a fundi wa miaka ya 1980 ???
Sekta ya ujenzi inabadilika kila siku je wewe umebadilika?
Zana mpya, mashine mpya, mbinu mpya na njia mpya zinaanzishwa kote ulimwenguni.Je ni wangapi miongoni mwetu tumeongeza maarifa hata kidogo kuhusu hayo yanayoendelea huko ulimwenguni ???
Yaani , baadhi yetu bado tunabeba zana zetu kwenye mufuka ya cement , K**a ni begi limechakaa kabisa. Haya tukitoka huko tunakotokea, tumevaa viatu,tukifika kwenye eneo la kazi tunavua viatu na kuanza kutembea miguu chuma ama tuvae viatu vilivyotoboka. Wengine wanavua mpaka mashati wanajenga kifua wazi. Unafikiri kuna mteja atakayekuona unakanyaga cementi miguu chuma akuthamini? Yaani sisi wenyewe hatujithamini unatarajia nani aje atuthamini?
Haya mambo walifanya wazee wetu zamani enzinza ukoloni siyo sisi vijana wa kisasa .
Hakuna kitu kibaya k**a kukataa kujiboresha. Nunua zana za kukuongezea kasi zaidi. Nunua buti, Overall ,gloves,kofia za kujilinda nk.
Boresha utendaji kazi wako punguza makosa.
Ukweli unaoumiza ni kwamba mafundi wengi wa ujenzi tumekaa miaka mingi tukilalamikia kipato chetu kuwa cha chini lakini tujiulize ni wangapi kati yetu tunaojiongeza kwenye kupata maarifa mapya.
Wengine wananiambia tuwe na chama cha kudai mishahara mizuri. Nikajiuliza mimi niliyejiajiri namdai nani?
Mafundi wanaweza kununua simu za bei ghali.
Wengine wanaweza kutumia pesa kwa vitu visivyo vya lazima.
Lakini linapokuja suala la kujifunza mbinu za kisasa afadhali aende kwa Pombe.