18/09/2026
*‼️ MITANDAO YA KIJAMII ‼️*
*Mema yake yanaweza kuwa k**a milima, na mabaya yake pia yanaweza kuwa k**a milima—hata baada ya mtu kufariki.*
*Kwa baadhi ya watu, mitandao yao itakuwa sababu ya kupata milima ya thawabu. Na kwa wengine, itakuwa sababu ya kubeba milima ya madhambi.*
*Basi, zitumie akaunti zako za mitandao ya kijamii kueneza kheri miongoni mwa Waislamu. 📚*
Na unajuaje?
*Huenda mtu akanufaika na ujumbe uliouchapisha, nawe ukawa umelala lakini daftari lako la thawabu likiendelea kuandikwa kwa sababu ya machapisho, jumbe au akaunti inayowafikishia Waislamu manufaa.*
*Ikiwa huwezi kuwa mlinganiaji wa kheri, basi angalau izuie shari yako isiwaendee watu.*
*⚠️ Jihadhari, kisha jihadhari sana, usiwe mlinganiaji wa shari. Kwa sababu siku moja utaondoka na kuacha nyuma yako yale yaliyoandikwa na vidole vyako.*
*Utaondoka, lakini yatabaki yale yaliyotamkwa na ulimi wako. Na mbele yako utakuta kitabu cha matendo ambacho Allaah, Mmoja Mwenye kulipa, amekuhifadhia na kuyahesabu yote.*
*Kitabu hicho kinaweza kuwa sababu ya kukuinua mpaka daraja za juu za Jannah, au kikawa sababu ya kukuangusha katika kina cha Moto. 🔥*
*⚘️Basi kabla hujaandika, chapisha au kutuma chochote, jiulize: Je, hiki kitakuwa sababu ya thawabu zinazoendelea, au madhambi yanayoendelea? ⚘️*